A
Anonymous
Guest
Katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kuna wanafunzi ambao tulisaini makubaliano ya ada kulipwa kupitia HESLB, lakini fedha hizo zilirudishwa HESLB. Tulipowasiliana na HESLB, tuliambiwa ni hitilafu ya mfumo na kwamba suala hilo linashughulikiwa, hivyo tusiwe na wasiwasi.
Hata hivyo, kwa sasa tunashindwa kuchapisha examination ticket kwa sababu mfumo unaonyesha tuna deni la ada. Pia hatuwezi kuona coursework zetu. Tulipolifikisha suala hili chuoni, tumeambiwa tulipe ada hiyo sisi wenyewe.
Je, hii ni haki? Tatizo ni nini hasa katika chuo hiki? Je, wanafunzi wa vyuo vingine pia wanakumbana na changamoto kama hii? Kwa nini wanafunzi wanaotegemea mikopo ya HESLB waathirike kutokana na hitilafu ambazo si zao?
Naomba mtusaidie kulifanya suala hili lijulikane ili mamlaka husika zilifanyie kazi haraka.