A
Anonymous
Guest
Ni kwa muda mrefu sasa wanafunzi wa Udaktari Bingwa wa Mifupa Bugando wamekuwa wakipitia mazingira magumu pamoja na kufelishwa makusudi katika idara yao bila uongozi wa chuo kuchukua hatua, ilhali wanafahamu matatizo yaliyopo kwenye idara hii.
Chuo kimekuwa kikidahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa kozi ya mifupa kwa wastani wa wanafunzi 17 mpaka 20, lakini wanaofanikiwa kumaliza kila mwaka hawafiki hata wanafunzi 8. Hii sio sifa nzuri kwa chuo.
Wengi wanaishia kuacha chuo, kuhamia vyuo vingine au kulazimika kusoma kwa miaka 4 mpaka 5.
Wanapokuwa masomoni wanatumia pesa nyingi kugharamia ada na mahitaji mengine, ambapo wanafunzi wanapofelishwa makusudi gharama zinaongezeka mara dufu. Mfano, mwanafunzi aliyerudishwa mwaka (retake) atatakiwa kulipa gharama ya shilingi milioni 1.6 ili afanye mtihani kwa somo moja. Fikiria ana masomo manne au zaidi. Fikiria Mtanzania wa kawaida upo masomoni, utawezaje kumudu hizi gharama?
Wanafunzi wanaojisomesha na serikali pia imewekeza pesa nyingi kusomesha hawa madaktari, na mwisho wa siku wanaishia kufeli na kuacha chuo. Tunapoteza madaktari bingwa wengi ambao wangeweza kusaidia Watanzania kwa wakati.
Kwa hali ya kawaida, ikiwa hata nusu ya darasa la wanafunzi hawana uhakika wa kumaliza masomo yao mpaka mwisho, kwa nini wanadahili wanafunzi wengi?
Hivyo ni vema serikali na TCU kufanya uchunguzi huru na wa kina kusaidia wanafunzi hawa wanaopitia mazingira magumu na kulazimika kuacha chuo wanapokuwa masomoni, kwa kuwa uongozi wa chuo umelifumbia macho jambo hili.