DOKEZO Wanafunzi wa Udaktari Bingwa Bugando wanaosomea Mifupa walalamikia kufelishwa makusudi, waomba mamlaka kuingilia kati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Ni kwa muda mrefu sasa wanafunzi wa Udaktari Bingwa wa Mifupa Bugando wamekuwa wakipitia mazingira magumu pamoja na kufelishwa makusudi katika idara yao bila uongozi wa chuo kuchukua hatua, ilhali wanafahamu matatizo yaliyopo kwenye idara hii.

Chuo kimekuwa kikidahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa kozi ya mifupa kwa wastani wa wanafunzi 17 mpaka 20, lakini wanaofanikiwa kumaliza kila mwaka hawafiki hata wanafunzi 8. Hii sio sifa nzuri kwa chuo.

Wengi wanaishia kuacha chuo, kuhamia vyuo vingine au kulazimika kusoma kwa miaka 4 mpaka 5.

Wanapokuwa masomoni wanatumia pesa nyingi kugharamia ada na mahitaji mengine, ambapo wanafunzi wanapofelishwa makusudi gharama zinaongezeka mara dufu. Mfano, mwanafunzi aliyerudishwa mwaka (retake) atatakiwa kulipa gharama ya shilingi milioni 1.6 ili afanye mtihani kwa somo moja. Fikiria ana masomo manne au zaidi. Fikiria Mtanzania wa kawaida upo masomoni, utawezaje kumudu hizi gharama?

Wanafunzi wanaojisomesha na serikali pia imewekeza pesa nyingi kusomesha hawa madaktari, na mwisho wa siku wanaishia kufeli na kuacha chuo. Tunapoteza madaktari bingwa wengi ambao wangeweza kusaidia Watanzania kwa wakati.

Kwa hali ya kawaida, ikiwa hata nusu ya darasa la wanafunzi hawana uhakika wa kumaliza masomo yao mpaka mwisho, kwa nini wanadahili wanafunzi wengi?

Hivyo ni vema serikali na TCU kufanya uchunguzi huru na wa kina kusaidia wanafunzi hawa wanaopitia mazingira magumu na kulazimika kuacha chuo wanapokuwa masomoni, kwa kuwa uongozi wa chuo umelifumbia macho jambo hili.
 
Kiafrika Afrika ni kawaida Sana hii
 
Maprofesa wa kiafrika ovyo sana wanapenda mno kuabudiwa.. Niulize swali, hao wanafunzi wa udaktari bingwa wa mifupa wanakuwa tayari na MD hapo amekuja tu ku specialize kwenye mifupa au ndio anakuwa fresh from form six?
 
Hakuna daktari bingwa fresh from form six..
daktari bingwa ni resident doctor yaani Daktari mkazi..yaani tayari ni daktari MD ambaye tayari amekwishafaya kazi zaidi ya miaka mitatu au minne ndo akaamua aende kuongeza elimu sehemu fulani yaani kwa mfano umefanuya kazi miaka 20 ukasema uende kuongeza uwezo kwenye upande ambao unaona umebobea sana
 
Ahaa afadhali bana
 
Ma professor wa upande huo ni mizinguo, kuna mzee mmoja ni Daktari wa upasuaji alikua ananisimulia miaka hiyo yupo muhimbili prof akaingia darasani walikua wapo wanafunzi 13 tuu ila alishangaa mbona wapo wengi sana 😀😀😀😀

Mwisho yule mzee ananiambia walihitimu wanafunzi wanne tuu na wengine wawili mwaka uliofuata jumla ni 6
 
Maprofesa wa kiafrika ovyo sana wanapenda mno kuabudiwa.. Niulize swali, hao wanafunzi wa udaktari bingwa wa mifupa wanakuwa tayari na MD hapo amekuja tu ku specialize kwenye mifupa au ndio anakuwa fresh from form six?
Stupid question.
 
Waafrica wengi tunaamini sana kwenye complexity na kupenda kuabudiwa sana.
 
Kutokana na mahitaji makubwa ya wataalam wa mifupa,serikali ingeingilia kati kuona jinsi ya kuzalisha wataalam wengi wenye viwango,hata kupata mabingwa wa kigeni wenye uelewa mpana wa kuwasaidia wanafunzi wao kufanya vizuri,kuliko hao wanaofelisha kwa makusidi kuonyesha ubingwa wao.
 
Ni kwa muda mrefu sasa wanafunzi wa Udaktari Bingwa wa Mifupa Bugando wamekuwa wakipitia mazingira magumu pamoja na kufelishwa makusudi katika idara yao bila uongozi wa chuo kuchukua hatua, ilhali wanafahamu matatizo yaliyopo kwenye idara hii.

Chuo kimekuwa kikidahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa kozi ya mifupa kwa wastani wa wanafunzi 17 mpaka 20, lakini wanaofanikiwa kumaliza kila mwaka hawafiki hata wanafunzi 8. Hii sio sifa nzuri kwa chuo.

Wengi wanaishia kuacha chuo, kuhamia vyuo vingine au kulazimika kusoma kwa miaka 4 mpaka 5.

Wanapokuwa masomoni wanatumia pesa nyingi kugharamia ada na mahitaji mengine, ambapo wanafunzi wanapofelishwa makusudi gharama zinaongezeka mara dufu. Mfano, mwanafunzi aliyerudishwa mwaka (retake) atatakiwa kulipa gharama ya shilingi milioni 1.6 ili afanye mtihani kwa somo moja. Fikiria ana masomo manne au zaidi. Fikiria Mtanzania wa kawaida upo masomoni, utawezaje kumudu hizi gharama?

Wanafunzi wanaojisomesha na serikali pia imewekeza pesa nyingi kusomesha hawa madaktari, na mwisho wa siku wanaishia kufeli na kuacha chuo. Tunapoteza madaktari bingwa wengi ambao wangeweza kusaidia Watanzania kwa wakati.

Kwa hali ya kawaida, ikiwa hata nusu ya darasa la wanafunzi hawana uhakika wa kumaliza masomo yao mpaka mwisho, kwa nini wanadahili wanafunzi wengi?

Hivyo ni vema serikali na TCU kufanya uchunguzi huru na wa kina kusaidia wanafunzi hawa wanaopitia mazingira magumu na kulazimika kuacha chuo wanapokuwa masomoni, kwa kuwa uongozi wa chuo umelifumbia macho jambo hili.
POLENI, UMELIFIKISHA SWALA HILI UONGOZI WA CHUO, TUNATAMBUA KUNA DEANS, DIRECTORS, VC AND EVEN COUNCILLOR MWENYEWE NA KWA CHUO CHENU CHA KIKATORIKI NI RAIS WA TEC, PROF. KAMUGISHA MBONA NI MTU MUELEWA SANA AMESHINDWA KUSIMAMIA JAMBO HILI....MPAKA LINAVUKA NA LINAKUJA HUKU.
 
Vyuo vya private ni takataka gharama kubwa mno
 
Bora ungesema ubora ndio Hakuna kwa vyuo vya GVT 3 tu nchi nzima tutawezaje kupunguza uhitaji wa Wabobezi kwneye Fani yw Afya na kwa Taarufa tu Private/GvT. Upande wa Masters tofauti ya gharama ni kidgo sana
 
Kulazimisha kila aliyeingia chuoni atoke na degree kunaiporomosha sana elimu nchini, maana sasa watu wanataka KUCHUKUA degree badala ya KUSOMEA degree!
MTU ANAPATA SHAHADA KAMA DAKTARI BINGWA LAKINI KAZI HAWEZI, KUMBE LENGO AKAFANYE KAZI ZA KIUTAWALA NA ANAPORUDI KAZINI OMBWE LINABAKI KAMA HAKUENDA CHUO!
 
Back
Top Bottom