Pre GE2025 Wanafunzi wa vyuo wamchangia Rais Samia na Rais Mwinyi fedha ya fomu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Your browser is not able to display this video.


Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wamefanya harambee ya kuwachangia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani pamoja na Rais wa zanziba Dkt.Hussein Mwinyi Fedha za kuchukua fomu ya ugombea Urais 2025 ikiwa ni katika hatua za kuwaonga mkono kutokana na kazi nzuri walizozifanya tangu kuingia madarajani.

Kwa vimbwanga na vituko vingine kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ruka hapa: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Wakiongozwa na rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini Zaynab Kitima kupitia kikao cha seneti kilichofanyika jijini Mbeya wanafunzi hao wamesema moja kati ya sababu zilizowafanya kumuunga mkono Dkt Samia ni pamoja na mazingira bora aliyoyaweka kwa wanafunzi ikiwemo bajeti ya fedha ya mikopo kuongezeka zaidi sambamba na wanafunzi wa vyuo vya kati kupata mikopo ya elimu ya juu.

Katika harambee hiyo wanafunzi hao wamefanikiwa kukusanya shilingi milioni moja ambayo wamesema wataikabidhi kwa mkuu wa mkoa wa mbeya Juma homera ili aweze kuzikabidhi kwa Rais Dkt Samia.
 
Hao wanafunzi enzi za nyerere wote wangefukuzwa chuo warudi nyumbani kwao maana hawajui umuhimu wa elimu yao
 
Hivi kweli SSH anakosa pesa ya form mpaka achangiwe? Tuache upumbavu
 
Takataka zinazo tumika na CCM hizo, ngoja zirudi huku mtaani ndio zitajua
 
Halafu warudi mtaani tusisikie kelele za hatuna ajira, tunasomesha mijitu mijinga kabisa
 
Kuna mtu kaumia๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ