Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi kweli pocket money za wanafunzi zinatumika kumchangia Samia fedha?Wakuu,
View attachment 3215090
Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wamefanya harambee ya kuwachangia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani pamoja na Rais wa zanziba Dkt.Hussein Mwinyi Fedha za kuchukua fomu ya ugombea Urais 2025 ikiwa ni katika hatua za kuwaonga mkono kutokana na kazi nzuri walizozifanya tangu kuingia madarajani.
Kwa vimbwanga na vituko vingine kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ruka hapa: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Wakiongozwa na rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini Zaynab Kitima kupitia kikao cha seneti kilichofanyika jijini Mbeya wanafunzi hao wamesema moja kati ya sababu zilizowafanya kumuunga mkono Dkt Samia ni pamoja na mazingira bora aliyoyaweka kwa wanafunzi ikiwemo bajeti ya fedha ya mikopo kuongezeka zaidi sambamba na wanafunzi wa vyuo vya kati kupata mikopo ya elimu ya juu.
Katika harambee hiyo wanafunzi hao wamefanikiwa kukusanya shilingi milioni moja ambayo wamesema wataikabidhi kwa mkuu wa mkoa wa mbeya Juma homera ili aweze kuzikabidhi kwa Rais Dkt Samia.
Hao njia pekee wanayo ona ya wao kuajiriwa au kupata kazi ni kupitia kujikomba hao hata kushikishwa ukuta ni rahisi sanaHawa wanafunzi ambao wengi wao wanashindia mandazi na maji halafu wanarubuniwa kutoa fedha zao adimu kuchanga fedha kwa ajili ya kulipia fomu za kugombea urais? Hawa wanachuo wengi wao hata fedha za kujikimu hawapati kutoka serikalini! Haya mambo tunaona kama ni kawaida lakini sio sawa. https://www.jamiiforums.com/data/video/5942/5942120-0e045276283a14d698a806c5c877fcc0.mp4
Adui namba moja wa nchi yetu ni chawa. Bila kupata dawa ya chawa tutaendelea kupiga mark time tu!Hawa wanafunzi ambao wengi wao wanashindia mandazi na maji halafu wanarubuniwa kutoa fedha zao adimu kuchanga fedha kwa ajili ya kulipia fomu za kugombea urais? Hawa wanachuo wengi wao hata fedha za kujikimu hawapati kutoka serikalini! Haya mambo tunaona kama ni kawaida lakini sio sawa. https://www.jamiiforums.com/data/video/5942/5942120-0e045276283a14d698a806c5c877fcc0.mp4
Mkuu Mimi nakuhakikishia hakuna chuo nnachokijua Dar mzima kilichopitisha michango..hao ni vijana wao wa chama walio vyuoni lkn kutujumuisha wte hatamimi sijapenda 🥹Ndio maana nikiona kijana msomi kakosa ajira nafurahi.
Vijana wa kulikomboa Taifa wao wanamuunga mkono muuza rasilimali zao
Ni zaidi ya upumbavu!Hivi kweli SSH anakosa pesa ya form mpaka achangiwe? Tuache upumbavu
sahivi hatuna vyuo tuna shule za msingi zilizochangamka, mtu ana degree hawezi hata kujieleza yeye mwenyewe hata akiambiwa aeleze historia yake mwenyewe kwa kiswahili achana na kiingireza.Mtu aliyeanzisha mchango kusaidia walioangukiwa na jengo Kariakoo alikamatwa na polis kwa kuchangisha. Wasomi wanachangishana kwa ajili ya fom, polisi wapo kimyaaaa.
Hii ndio Tanzania.
Uchawa ata best. Pesa yenyewe inatokana ima na uchawa, umalaya au kujikomba mbali na mikopo ya kuvutana. Namna hii, hakuna wasomi bali watu wanaopoteza muda darasani bila kuelimika. Huwa naita hii education for ignorance vinginevyo hiyo pesa wawe wapewa na yule wanaye 'changia' kupata ujiko.Wakuu,
View attachment 3215090
Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wamefanya harambee ya kuwachangia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani pamoja na Rais wa zanziba Dkt.Hussein Mwinyi Fedha za kuchukua fomu ya ugombea Urais 2025 ikiwa ni katika hatua za kuwaonga mkono kutokana na kazi nzuri walizozifanya tangu kuingia madarajani.
Kwa vimbwanga na vituko vingine kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ruka hapa: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Wakiongozwa na rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini Zaynab Kitima kupitia kikao cha seneti kilichofanyika jijini Mbeya wanafunzi hao wamesema moja kati ya sababu zilizowafanya kumuunga mkono Dkt Samia ni pamoja na mazingira bora aliyoyaweka kwa wanafunzi ikiwemo bajeti ya fedha ya mikopo kuongezeka zaidi sambamba na wanafunzi wa vyuo vya kati kupata mikopo ya elimu ya juu.
Katika harambee hiyo wanafunzi hao wamefanikiwa kukusanya shilingi milioni moja ambayo wamesema wataikabidhi kwa mkuu wa mkoa wa mbeya Juma homera ili aweze kuzikabidhi kwa Rais Dkt Samia.
Wewe ni umenizidi yaan -1 - 1 = ?