Fortyseven
JF-Expert Member
- Oct 30, 2020
- 1,518
- 2,834
Yesu kwa kiarabu ni yasu'a na sio isa usidanganye unaelewa maana ya jina Yesu??Biblia ya Kingereza nao Jina la Yesu wameandika Yesu ?
وَإِذۡ قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ يَٰبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُم مُّصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيَّ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَمُبَشِّرَۢا بِرَسُولٖ يَأۡتِي مِنۢ بَعۡدِي ٱسۡمُهُۥٓ أَحۡمَدُۖ فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ قَالُواْ هَٰذَا
Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri! (61 : 6 )
1. Aliposema yeye ni Mtume wa Mungu ; Shahada kuhuhu yeye na Mungu
2. Akataja kuja kwa Mtume na akasema jina lake ni Ahmad (Muhammad) : hapo Yesu mwenyewe (Amani iwe juu yake) kashakubali utume wa Muhammad (Peace and blessings be upon Him) na akiwaambia Wanafunzi wake wakubali .
Uilsamu maana yake ; kujisalimisha kwa Moka mlezi muumba kwa kumpwekesha yeye (kumuabudu peke yake ) , kumtii yeye , kufuata mitume yake na kuachana na washirikina na watu wake.
Mtu awe enzi ya Adam , Nuh , Yusuph , Yakubu nk ni Muislamu ilimradi tu hafanyi ushirikina kwa kuabudu Miungu wengine au kuabudu mwenyewezi Mungu pamoja na Miungu wengine
2. Akawafuata mafundisho wa Mitume katika zama mfano watu wa Yesu wasikilize na kumfuata Yeye au Nuh nk
3. Wakatii maarisho yake mfano kuswali , zaka , kusaidia nk kuacha makatazo mfano zinaa , mauaji nk Kutokana na mafundisho ya MaNabii wao katika wakati husika watahesabika Waislamu.
Ndio maana Wakristo wa Najran Uarabuni kipindi Cha Mtume Muhammad walipokuja na msafara wao kumuona baada kusomewa mafundisho ya Uislamu walikubali na kusema kuwa walikuwa Waislamu toka zamani
ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِهِۦ هُم بِهِۦ يُؤۡمِنُونَ
Wale tulio wapa Kitabu kabla yake (mfano watu wa Yesu injili) wawanakiamini hiki. (Qur'an)
وَإِذَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِهِۦٓ إِنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّنَآ إِنَّا كُنَّا مِن قَبۡلِهِۦ مُسۡلِمِينَ
Na wanapo somewa wanasema: Tunaiamini. Hakika hii ni Haki inayo toka kwa Mola wetu Mlezi. Hakika sisi kabla yake tulikuwa ni Waislamu, tulio nyenyekea. (28 : 52 - 53 )
☝️☝️ Hizo Aya zilishuka sababu ya tukio la ujionwa Wakristo wa Najran , walikuwa kama Orthodox sio Wakristo wa utatu mtakatifu baada ya kuona Uislamu na mafundisho yake kuwa hakuna kumshirikisha Mungu unakataza maovu na kuiamrisha mema wakasema misingi hiyo ndio walikuwa wanafuata na kama huo ndio Uislamu basi wao walikuwa Waislamu toka kitambo na wakakubali kumfuata Mtume Muhammad peace and blessings be upon Him
Wana wa Israeli na Waebrania kuwa Waislamu inategemea kama waliowafuata Manabii wao au waliwakataa , kwa waliowakataa Manabii wao mfano Daudi , Suleyman , Musa , Harun , Ibrahiim nk (Amani iwe juu yao wote ) hawahesabiki kuwa Waislamu (walionyenyekea kwa mwenyewezi Mungu)Je Kuna sehem nyingne nje ya Quran inasema wayahudi na waebrania ni waislam?
Wana wa Israeli na Waebrania kuwa Waislamu inategemea kama waliowafuata Manabii wao au waliwakataa , kwa waliowakataa Manabii wao mfano Daudi , Suleyman , Musa , Harun , Ibrahiim nk (Amani iwe juu yao wote ) hawahesabiki kuwa Waislamu (walionyenyekea kwa mwenyewezi Mungu)
Kwa waliowakubali na kuwatii ndio wanahesabika ni Waislamu regardless na zama zipi . Kama sisi wote Tunahesabika Watanzania bila kujali ulizaliwa wakati wa Magufuli au Nyerere.
Kuhusu sememu nyingine nje na Qu'ran sifahamu
Quran tukufu isiyo na chembe ya shaka inasema
Quran 3 :52
"Isa alipo hisi kuwa kati yao pana ukafiri alisema: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu.
Sasa Unabisha ulikuwepooo 😂😂😂😂
Ila Quran ya kiwaki sana.
Kwa namna Mudy alivyoiset Quran , itasomba wajinga weng sana.
Wazolee
Dumas the terrible
Je Kuna sehem nyingne nje ya Quran inasema wayahudi na waebrania ni waislam?
Nimekuelewa. Na umejibu kiungwana. Na mm ntakuhoji hivyo hivyo.
Kunyenyekea kwa Mungu mmoja ndio unaitwa Uislamu.
Na Uislam ni neno la Kiarabu.
Je Kama kukiwa na neno la kiebrania lenye maana ya kunyenyekea na kujisalimisha kwq Mungu mmoja . Ni sawa tukuwaita watu hao pamoja na waarabu wote kwa jina hilo?.
Jina hilo la kiebrania?
Ndio , ni sawa kabisaNimekuelewa. Na umejibu kiungwana. Na mm ntakuhoji hivyo hivyo.
Kunyenyekea kwa Mungu mmoja ndio unaitwa Uislamu.
Na Uislam ni neno la Kiarabu.
Je Kama kukiwa na neno la kiebrania lenye maana ya kunyenyekea na kujisalimisha kwq Mungu mmoja . Ni sawa tukuwaita watu hao pamoja na waarabu wote kwa jina hilo?.
Jina hilo la kiebrania?
Ndio , ni sawa kabisa
Mohamed alitajwa kwenye vitabu vyao? Sehemu gani? Quran haijui hata Yesu aliishi wapi,alikuwa na wanafunzi wangapi,majina yao.Ndio walishahadia Shahada ya kwanza ni ya kumkubali Mungu na ya pili na ya kumkubali Mtume aliyeletwa kwao ambaye ni Yesu (Amani iwe juu yake ) sasa watawezaje kutoa shahada ya kumkubali Muhammad (Peace and blessings be upon Him) kuwa Mtume wao wakati alikuwa bado hajaletwa ? Baada ya kuleta Mtume Muhammad na kuja wale wafuasi wa Yesu hapo ndio lazima kumfuata Mtume mpya maana ndio amekuja kuendeleza chain ya Manabii wa Allaah . Baada ya kuja yeye haikubaliki tena Mila yeyote.
Ila kwenye Qu'ran na hadithi Kuna viashiria kuwa Wanafunzi wa Yesu na waliomfuata mafundisho yake kiukweli walishahadia hata kabla ya ujio wa Mtume Muhammad (Peace and blessings be upon Him ) na kuweka nia kuwa akija watamfuata kwani alitajwa kwenye vitabu vyao na ikawa unafahamika kuwa Kuna Mtume mpya atatokea bara la Uarabuni.
Ndio maana Kuna Swahaba Salmani Al Farsi(Allaah amridhie )yeye alikuwa kwenye dini ya kuabudu moto huko Syria kama sikosei siku ulivyokuja msafara Wakristo nchini kwao akaipenda hiyo dini na akatoroka kuishi na kiongozi mkubwa wa Kikiristo wakati huo alipo kufa alihamia kwa kiongozi mwengine mpaka wa mwisho alipokaribia kufa alimwambia kuwa Zama za kufika Mtume mpya zimekaribia akamuelekeza alama zake na maeneo atayapatikana huyo Swahaba akafika mpaka Madina akahakiki zile alama alizoambiwa na huyo kiongozi wa kikiristo akawa Muislamu . (Soma historia yake Swahaba Salman Al Farsi Allaah amridhie ipo hata gugo)
Nitarudi nikuonyeshe Shahada kwenye Qu'ran
Sababu wamepoteza dini yao, baada ya kufa Manabii viongozi wao wakachezea dini kubadilisha Sheria mwanzo ilikuwa kila pakitokea uharibifu analetwa Nabii mwingine kuwarudisha kwenye mstari mpka akaja na Yesu baada ya hapo ikapita miaka mingi uharibifu mkubwa ukatokea sio Taurat wala Injili hakuna kilicho salimika vitu vingi vikaongezwa na kuondolewa .Sawa.
Kwanini sasa wayahudi na Waebrania waliokuwa wanawaumini mitume ya mwenyezi Mungu mnawaita makafiri wakat ni imani ile ile . Kasoro ni kuwa hawamuamini Mtume.
Wana dini yao. Na iman zao.
Na wamekataa kuamini iman ya kiarabu.
Ndio quran iseme wataenda motoni?.
Yesu (Amani iwe juu yake ) na Wanafunzi wake waliomfuata wote walikuwa Waislamu, ukiristo ulibuniwa baada ya yeye kuondoka na watu wakapotosha mafundisho yake na kuweka utatu , Yeye ni Mungu na mengineyo
Sababu wamepoteza dini yao, baada ya kufa Manabii viongozi wao wakachezea dini kubadilisha Sheria mwanzo ilikuwa kila pakitokea uharibifu analetwa Nabii mwingine kuwarudisha kwenye mstari mpka akaja na Yesu baada ya hapo ikapita miaka mingi uharibifu mkubwa ukatokea sio Taurat wala Injili hakuna kilicho salimika vitu vingi vikaongezwa na kuondolewa .
Hata sisi Muislamu yeyote akimkataa Mtume hata mmoja anahesabika Kafiri kwa mfano Muislamu amakatae Yesu , Ibrahiim, Nuhu , Daudi nk aseme mmoja wao au wote hawakuwa Manabii wa Mungu huyo sio Muislamu.
Kumkataa kwao Mtume wa mwisho wa mwenyewezi Mungu Muhammad peace and blessings be upon baada ya kuwajia ni kufuru .
Sababu wamepoteza dini yao, baada ya kufa Manabii viongozi wao wakachezea dini kubadilisha Sheria mwanzo ilikuwa kila pakitokea uharibifu analetwa Nabii mwingine kuwarudisha kwenye mstari mpka akaja na Yesu baada ya hapo ikapita miaka mingi uharibifu mkubwa ukatokea sio Taurat wala Injili hakuna kilicho salimika vitu vingi vikaongezwa na kuondolewa .
Hata sisi Muislamu yeyote akimkataa Mtume hata mmoja anahesabika Kafiri kwa mfano Muislamu amakatae Yesu , Ibrahiim, Nuhu , Daudi nk aseme mmoja wao au wote hawakuwa Manabii wa Mungu huyo sio Muislamu.
Kumkataa kwao Mtume wa mwisho wa mwenyewezi Mungu Muhammad peace and blessings be upon baada ya kuwajia ni kufuru .
Inajulikana ukristo ulikuwepo miaka 600 kabla ya uislam kuanza, sasa inawezekana vipi hao wanafunzi wawe waislam dini ambayo haikuwepo? au ndio story za back to the future,kobazi mjiongeze kidogo mnalishwa sana matango pori
Kwamba Petro huyu tunayemfahamu alikuwa muislamu?Yesu (Amani iwe juu yake ) na Wanafunzi wake waliomfuata wote walikuwa Waislamu, ukiristo ulibuniwa baada ya yeye kuondoka na watu wakapotosha mafundisho yake na kuweka utatu , Yeye ni Mungu na mengineyo