Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Wewe acha upoyoyo, Weka uthibitisho wa kitabu hata kimoja kilichomtaja Mudy kabla ya kuleta Quran yake.Ndio walishahadia Shahada ya kwanza ni ya kumkubali Mungu na ya pili na ya kumkubali Mtume aliyeletwa kwao ambaye ni Yesu (Amani iwe juu yake ) sasa watawezaje kutoa shahada ya kumkubali Muhammad (Peace and blessings be upon Him) kuwa Mtume wao wakati alikuwa bado hajaletwa ? Baada ya kuleta Mtume Muhammad na kuja wale wafuasi wa Yesu hapo ndio lazima kumfuata Mtume mpya maana ndio amekuja kuendeleza chain ya Manabii wa Allaah . Baada ya kuja yeye haikubaliki tena Mila yeyote.
Ila kwenye Qu'ran na hadithi Kuna viashiria kuwa Wanafunzi wa Yesu na waliomfuata mafundisho yake kiukweli walishahadia hata kabla ya ujio wa Mtume Muhammad (Peace and blessings be upon Him ) na kuweka nia kuwa akija watamfuata kwani alitajwa kwenye vitabu vyao na ikawa unafahamika kuwa Kuna Mtume mpya atatokea bara la Uarabuni.
Ndio maana Kuna Swahaba Salmani Al Farsi(Allaah amridhie )yeye alikuwa kwenye dini ya kuabudu moto huko Syria kama sikosei siku ulivyokuja msafara Wakristo nchini kwao akaipenda hiyo dini na akatoroka kuishi na kiongozi mkubwa wa Kikiristo wakati huo alipo kufa alihamia kwa kiongozi mwengine mpaka wa mwisho alipokaribia kufa alimwambia kuwa Zama za kufika Mtume mpya zimekaribia akamuelekeza alama zake na maeneo atayapatikana huyo Swahaba akafika mpaka Madina akahakiki zile alama alizoambiwa na huyo kiongozi wa kikiristo akawa Muislamu . (Soma historia yake Swahaba Salman Al Farsi Allaah amridhie ipo hata gugo)
Nitarudi nikuonyeshe Shahada kwenye Qu'ran
