Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Wanafunzi sita wa shule ya mtakatifu John Paul II ya mkoani Shinyanga walienda kutoa mahindi kwenye kihenge cha shule lakini yalishindwa kutoka wakiwa na mwalimu wa zamu katika usimamizi wa chakula, mwalimu alielekeza wanafunzi watatu waingie ndani kutafuta namna ya kuyafungulia kisha akaenda kunywa chai. Baada ya muda kupita, wanafunzi watatu waliobaki nje wakaona wenzao hawatoki na kutoa taarifa kwa walimu.
Walimu walipofika waliita bila mafanikio, wakavunja kihenge na kukuta wamezirai. Baada ya kufikishwa zahanati ya shule matibabu hayakuleta majibu na kukimbizwa hospitali ya Kahama ikathibitishwa wamefariki kutokana na kukosa hewa safi.
Kaimu kamanda wa Polisi, ACP Kennedy Mgani amesema Mwalimu wa zamu, Morris Sileo anashkiliwa na Jeshi la Polisi kwa kushindwa kusimamia vyema ili kubaini uchunguzi na chanzo cha vifo cha wanafunzi hao.