Wanafunzi watatu wafariki kwa kukosa hewa wakati wanatoa mahindi kwenye kihenge cha shule, mwalimu aliwaacha na kwenda kunywa chai

Wanafunzi watatu wafariki kwa kukosa hewa wakati wanatoa mahindi kwenye kihenge cha shule, mwalimu aliwaacha na kwenda kunywa chai

Wanafunzi sita wa shule ya mtakatifu John Paul II ya mkoani Shinyanga walienda kutoa mahindi kwenye kihenge cha shule lakini yalishindwa kutoka wakiwa na mwalimu wa zamu katika usimamizi wa chakula, mwalimu alielekeza wanafunzi watatu waingie ndani kutafuta namna ya kuyafungulia kisha akaenda kunywa chai. Baada ya muda kupita, wanafunzi watatu waliobaki nje wakaona wenzao hawatoki na kutoa taarifa kwa walimu.

Walimu walipofika waliita bila mafanikio, wakavunja kihenge na kukuta wamezirai. Baada ya kufikishwa zahanati ya shule matibabu hayakuleta majibu na kukimbizwa hospitali ya Kahama ikathibitishwa wamefariki kutokana na kukosa hewa safi.

Kaimu kamanda wa Polisi, ACP Kennedy Mgani amesema Mwalimu wa zamu, Morris Sileo anashkiliwa na Jeshi la Polisi kwa kushindwa kusimamia vyema ili kubaini uchunguzi na chanzo cha vifo cha wanafunzi hao.
Kila sekta ni majanga.

Mungu awafariji familia
 
Huko Moshi itabidi huo mfumo wa kuhifadhi mahindi/Maharage kwenye hayo mapipa wayakataze.

Maana hii ni case ya 2 kwenye Mkoa mmoja.
It seems kuna shule nyingi wanatumia huo mfumo.

Ni hatari kwa wanafunzi.
 
Mwaka jana vilitokea vifo vya wanafunzi kupitia kihenge,
Sijui huwa nini hasa,
Polee kwa wafiwa, Rip wapendwaa. [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Kwenye vihenge wengi huweka dawa ya kuua wadudu ili mazao yasibunguliwe - sasa sumu ile ndiyo hatari kwa watu
 
Sijui unafikishaje habari za kifo kwa mzazi kuwa mwanae kafa kwa kukosa hewa ndani ya bakuli la kuhifadhia mahindi na mwalimu alimuacha huko sababu hajanywa chai.
 
kuna uzembe mkubwa kwa walimu.
walimu wote wa shule hiyo ni wazembe.
 
Mwaka jana vilitokea vifo vya wanafunzi kupitia kihenge,
Sijui huwa nini hasa,
Polee kwa wafiwa, Rip wapendwaa. [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Probably ni kwasababu mahindi yaliwekwa dawa ya kuyahifadhi yasiharibike... Kuna dawa kama kidonge inawekwa mahali inasambaa kama hewa ndani ya chumba cha kuhifadhia mazao... Sasa ukikaa humo muda mrefu lazima ikuathiri
 
Inabidi awareness training za kutosha zifanyike
Yes exactly; Halafu awareness iwe ni kwa waalimu wote na wanafunzi katika shule zote. Na zaidi; waalimu wasisitizwe kupata ushauri wa Kitaalam (au wawashirikishe wataalam kila inapowezekana) kutoka kwa Wataalam husika e.g. Mtaalam wa kilimo (Agricultural extension officers) aliye karibu kabla ya kufanya shughuli yoyote inayohusu shughuli au jambo lolote linalohusu Kilimo, mifugo n.k. kwa sababu wahanga hao wamevuta hewa ya sumu (wamejisumisha = self intoxicated)lakini waalimu na baadhi ya wadau wengine hapo juu wanasema eti wamekosa hewa - kitu ambacho sio kweli hata kidogo.
Inasikitisha mno. Poleni sana wazazi na jamii husika.
 
Probably ni kwasababu mahindi yaliwekwa dawa ya kuyahifadhi yasiharibike... Kuna dawa kama kidonge inawekwa mahali inasambaa kama hewa ndani ya chumba cha kuhifadhia mazao... Sasa ukikaa humo muda mrefu lazima ikuathiri
Upo sahihi kabisa mkuu.
 
Sijui unafikishaje habari za kifo kwa mzazi kuwa mwanae kafa kwa kukosa hewa ndani ya bakuli la kuhifadhia mahindi na mwalimu alimuacha huko sababu hajanywa chai.
Habari itafikishwa kwa wazazi kwa vyovyote vile kwa kutumia busara na hekima lakini bila kuelekeza shutuma dhidi ya mwalimu eti aliwaacha wanafunzi akaenda kunywa chai - hii statement inaamsha hisia za kujenga chuki baina ya Waalimu na Wazazi na sio vizuri. Yaliyopita yamepita; tugange yaliyopo na yajayo.
 
Ok boss, Wewe ndo mwalimu unaemsemea mwalimu wa zamu aliekwenda kunywa chai akaacha watoto bahati mbaya wakafa. Wazazi wamefika ofisini kwako, embu waeleze kilichotokea kwa kutumia busara ya kuwawezesha kuganga yajayo na pasiwepo chuki ili nijifunze kitu. Maana nachakata namna ya kuelezea ukweli wa hilo tukio sipati maneno.

Haya twende mkuu, unaanzia wapi?
 
Huko Moshi itabidi huo mfumo wa kuhifadhi mahindi/Maharage kwenye hayo mapipa wayakataze.

Maana hii ni case ya 2 kwenye Mkoa mmoja.
It seems kuna shule nyingi wanatumia huo mfumo.

Ni hatari kwa wanafunzi.
Mkuu; huo mfumo hauna tatizo . Tatizo lipo kwa WATUMIAJI. Kama mtumiaji anashindwa kufuata maelekezo na Tahadhari zilizotolewa au kuelekezwa namna mfumo huo unavyofanya kazi na ni Tahadhari gani za kuzingatiwa, hiyo inakuwa ni uzembe wa mtumiaji na kwa mantiki hiyo sio sahihi kusema Mfumo huo ukatazwe. Wakatazwe wale wazembe wanaoutumia mfumo huo bila ya kuuelewa vizuri au kuwashirikisha wataalam husika.
 
Wanafunzi wameenda kusoma au kufanya kazi😕
Ni jambo la kawaida kwa shule zetu, mfano unasoma shule ina mchepuo wa kilimo, unategemea nani aende shambani..?? nani avune..?? nani ahifadhi mahindi..??

Tushalima sana, kuvuna na kuhifadhi mahindi mashuleni... Na nyingi ya shule hizi ni zile za bweni
 
Back
Top Bottom