Hawasimamiwi wala kulazimishwa kusoma kama wenzao wanaosimamiwa kuanzia saa 11 alfajri hadi usiku, wao tayari wamejiongeza wenyewe kwa akili za ziada
Wana msaada kidogo kutoka kwa walimu wanaofika mara chache madarasani, vitabu vichache, n.k. kwa asilimia kubwa hujisomea kivyao ila wana IQ kubwa sana ya kujindisha kwa materials chache. unaweza kumpa notes chache akamzidi yule aliesoma vitabu vitano
Wana IQ kubwa ya kutatua maswali mapya, ni tofauti na wenzao wanasolve maswali ya pastpapers kama yote, swali moja mwalimu anazoesha wanafunzi namna ya kulijibu mara nyingi, mitihani ya taifa ikija hakuna maswali mapya, wanatiririka tu.
Hawa watu ni multi purpose, Wana IQ kubwa ya kufanya mambo mengi kwa wakati moja, Nje ya kusoma wanafanya shughuli kadhaa za kuongeza kipato cha familia kama kulima, wanajipikia, wanatembea kila siku kwenda shuleni, mambo kibao ya mtaani wakiwa nyumbani, n.k. ni tofauti na wenzao asubuhi mpaka usiku ni kusoma tu