N:B: shule za kata nyingi bado zina changamoto kibao, ukiwa na uwezo peleka mtoto shule nzuri umpunguzie changamoto zinazoingilia elimu yake.
Mtu aliyesoma kwenye mazingira duni na bado akawa zaidi, sawa au kuwakaribia hawa waliosoma kwenye mazingira wezeshi na yenye kila nyenzo zinazohitajika kupata elimu bora, haina mjadala mtu huyo ana uwezo mkubwa sana wa kiakili, ni sawa na darasani kuna watu uwezo unaishia table ya 12 lakini kuna watu wana upeo binafsi wanatiririka hadi table ya 50.
Hawasimamiwi wala kulazimishwa kusoma kama wenzao wanaosimamiwa kuanzia saa 11 alfajri hadi usiku, wana uwezo wa kuji manage wenyewe, kuanzia ratiba, kuhandle presha, kuji motivate, n.k.
Wana msaada kidogo kutoka kwa walimu wanaofika mara chache madarasani, vitabu vichache, n.k. kwa asilimia kubwa hujisomea kivyao ila wana IQ kubwa sana ya kujindisha kwa materials chache. unaweza kumpa notes chache akamzidi yule aliesoma vitabu vitano
Wana IQ kubwa ya kutatua maswali mapya, ni tofauti na wenzao wanataftiwa maswali kibao ya kusolve na walimu wao hasa pastpapers, swali moja linarudiwa mara nyingi kwenye vipindi, solvings za alfajiri, test za kila wiki, kila mwezi, mitihani yamuhula, n.k. mitihani ya taifa ikija hakuna maswali mapya, wanatiririka tu.
Hawa watu ni multi purpose, Wana IQ kubwa ya kufanya mambo mengi kwa wakati moja, Nje ya kusoma wanafanya shughuli kadhaa za kuongeza kipato cha familia kama kulima, wanajipikia, wanatembea kila siku kwenda shuleni, mambo kibao ya mtaani wakiwa nyumbani, n.k. ni tofauti na wenzao asubuhi mpaka usiku ni kusoma tu