Wanafunzi wote waache shule na vyuo: Ushauri wa tahadhari

Wanafunzi wote waache shule na vyuo: Ushauri wa tahadhari

Bichwa komwe bichwa komwe nakuitaa kwa mara ya pili tena..
 
Hii ni tahadhari nawapa, kwa wazazi na wanafunzi kwa ujumla.

Ewe mzazi, usipoteze mamilioni kusomesha mtoto wako kwa uchungu na kwa jasho halafu akarudi nyumbani kukaanga chips na kuendesha bajaji.

Ewe mzazi, usiuze ng'ombe zako, usiuze ardhi yako, usifilisi biashara zako kwa ajili ya kupeleka hela shuleni. Unapoteza muda na fedha nyingi, utashangazwa mwanao atarudi nyumbani na makaratasi matupu akaanze kuendesha bodaboda na kuuza mwili wake kwenye madanguro.

Ewe mwanafunzi, usipoteza muda wako wa miaka zaidi ya ishirini unahangaika kusoma kwa tabu na uchungu mkubwa, utashangazwa. Utarudi mtaani kuwa boda boda.

Ewe mwanafunzi, kama uko shule achana nayo, kimbia haraka kaanze kujihangaikia.

Ewe mwanachuo, achana na habari hizo, ondoka hapo unapoteza muda. Unapoteza fedha nyingi kwenye sifuri.

Changamka. Ubodaboda hauhitaji digrii au cheti cha form four.

Achana na hiyo shule, anza sasa hivi kujifunza bodaboda utanishukuru. Usisubiri mpaka miaka 10 ijayo ukiwa umechoka na umeshapoteza fedha nyingi kwenye hamna.

Wenye masikio na wasikie. Wazazi amkeni. Shule ni ujinga.
Ili watoto wa watawaliwa waweze kupata kazi iwepo sheria ya kuwahasi viongozi wa CCM ili wasiwe na watoto wa kuwapa ajira, hii itawezesha watoto wa watawaliwa kupata kazi.
 
Hii ni tahadhari nawapa, kwa wazazi na wanafunzi kwa ujumla.

Ewe mzazi, usipoteze mamilioni kusomesha mtoto wako kwa uchungu na kwa jasho halafu akarudi nyumbani kukaanga chips na kuendesha bajaji.

Ewe mzazi, usiuze ng'ombe zako, usiuze ardhi yako, usifilisi biashara zako kwa ajili ya kupeleka hela shuleni. Unapoteza muda na fedha nyingi, utashangazwa mwanao atarudi nyumbani na makaratasi matupu akaanze kuendesha bodaboda na kuuza mwili wake kwenye madanguro.

Ewe mwanafunzi, usipoteza muda wako wa miaka zaidi ya ishirini unahangaika kusoma kwa tabu na uchungu mkubwa, utashangazwa. Utarudi mtaani kuwa boda boda.

Ewe mwanafunzi, kama uko shule achana nayo, kimbia haraka kaanze kujihangaikia.

Ewe mwanachuo, achana na habari hizo, ondoka hapo unapoteza muda. Unapoteza fedha nyingi kwenye sifuri.

Changamka. Ubodaboda hauhitaji digrii au cheti cha form four.

Achana na hiyo shule, anza sasa hivi kujifunza bodaboda utanishukuru. Usisubiri mpaka miaka 10 ijayo ukiwa umechoka na umeshapoteza fedha nyingi kwenye hamna.

Wenye masikio na wasikie. Wazazi amkeni. Shule ni ujinga.
Elimu sio ujinga lakini kwa mitaala inayotolewa hapa nchini haimuandai kijana kujiajiri.
 
Mtu asiyesoma hata angekuwa na fedha vipi... kuna alama fulani hivi huwa haitoki. Ni kama mtu anakuwa amepigwa chapa ya ujinga. Msomi na mwenye pesa, utamuona anavyoonekana. Somesha watoto wako, sio ili waepuke umaskini ila wajikomboe kifikra na waishi kwa uhuru na kuyamudu mazingira yao. ACHANA NA HUU USHAURI WA KIJINGA KWENYE HII SLEDI. Hapa chini naomba nikupe baadhi ya faida za elimu: -

1. Kupata Elimu: Hii ndiyo sababu ya msingi kabisa ya kwenda shule. Shuleni unajifunza vitu vingi vinavyokusaidia kuelewa dunia inayokuzunguka na jinsi ya kuishi maisha yako kwa mafanikio. Unajifunza kusoma, kuandika, kuhesabu, na masomo mengine muhimu kama historia, sayansi, lugha, na sanaa. Elimu hii inakufungua macho na kukupa uwezo wa kufikiria kwa kina (Critical thinking), kutatua matatizo, na kufanya maamuzi sahihi.

2. Kujiendeleza: Shule sio tu inahusu kupata elimu ya vitabu, bali pia inahusu kujiendeleza mwenyewe. Shuleni unakutana na watu kutoka sehemu mbalimbali na unajifunza kuishi na kufanya kazi pamoja nao. Unajifunza kujieleza, kujiamini, na kuwa na nidhamu. Pia unapata nafasi ya kujaribu vitu vipya na kugundua vipaji vyako.

3. Kupata Fursa Bora: Elimu na ujuzi unayopata shuleni unakufungua milango ya fursa nyingi maishani. Unaweza kuendelea kusoma chuo kikuu na kupata kazi nzuri/ au kupata maarifa ya kuanzisha biashara yako ambayo utaiendesha kwa tija zaidi na muendelezo na ikakuingizia kipato bora. Pia unakuwa na uwezo wa kujitegemea na kuwahudumia familia yako na jamii Yako vizuri zaidi.

4. Kuboresha Jamii: Watu wenye elimu ni muhimu kwa ujenzi wa jamii imara na yenye maendeleo. Hebu fikiria aliebuni Injini inayokimbia spidi 300 na kuwafikisha watu na Mizigo na kuchangia maendeleo. Shule inakufundisha kuwa raia mwema, kuheshimu sheria, na kuchangia katika maendeleo ya jamii yako. Unajifunza pia kuhusu haki za binadamu na jinsi ya kutetea haki za wengine. Anaekwambia usiende shule ni mou mbinafsi ambre hafikirii kwamba WAJIBU WA BINADAMU NI PAMOJA NA KUWAFAIDIA BINADAMU WENZIE. Aliebuni ndege inayofikisha watu na mizigo alienda shule.

5. Kufurahia Maisha: Shule sio tu mahali pa kusoma, bali pia mahali pa kujifurahisha na kupata marafiki. Unaweza kushiriki katika michezo, shughuli za ziada, na shughuli nyingine za kufurahisha. Marafiki unaowapata shuleni watakuwa sehemu muhimu ya maisha yako na wataweza kukusaidia na kukutia moyo katika nyakati ngumu. Shule na Chuo ni mahali ambapo vijana wanafahamiana vizuri zaidi na kung'amua vipawa vya wenzao wanaofaa kuwa wenza wa Maisha, wafanyakazi wenza, wafanyabiashara wenza nk...

Kwa hiyo, sababu za kwenda shule ni nyingi na zote ni muhimu. Usikose fursa ya kujifunza, kujiendeleza, na kufurahia maisha shuleni! MTU YEYOTE ANAEPINGANA NA SHULE NI MBINAFSI. Dunia inaendeshwa kwa Maarifa ya kuhamishiana yanayopatikana shuleni pekee. Uholela wa binadamu hutokana na kutokuwa na Elimu au kuwa na elimu na kuamua kutoitumia eg mipango miji mibovu.

N'yadikwa
 
Wengi hawawezi kukuelewa ila ulichokiandika hapa kina ukweli. Kwa hapa tz elimu inatupotezea muda tu, haituandai kukabiliana na maisha halisi. Kwa upande wangu naona elimu ya form 4 inatosha sana.

Kama mtu atasoma vizuri, ajifunze kiingereza cha kuongea na kuandika, ujanja wa technojia. Kisha aje mtaani aanze kujifunza life skills na namna watu wanavyojipatia rizki kwa njia mbali mbali.

Hapo akiongezea na elimu yake aliyopata basi atakuwa na asilimia kubwa ya kufanikiwa kimaisha.
Mpo sahihi wote wote , mana mpaka Sasa walio ishia la saba na form 4 wametupiga gepu, sisi tunaangaika na kusambaza bahasha wenzetu wanapigwa hatua na biashara na mambo mengine
 
Hii ni tahadhari nawapa, kwa wazazi na wanafunzi kwa ujumla.

Ewe mzazi, usipoteze mamilioni kusomesha mtoto wako kwa uchungu na kwa jasho halafu akarudi nyumbani kukaanga chips na kuendesha bajaji.

Ewe mzazi, usiuze ng'ombe zako, usiuze ardhi yako, usifilisi biashara zako kwa ajili ya kupeleka hela shuleni. Unapoteza muda na fedha nyingi, utashangazwa mwanao atarudi nyumbani na makaratasi matupu akaanze kuendesha bodaboda na kuuza mwili wake kwenye madanguro.

Ewe mwanafunzi, usipoteza muda wako wa miaka zaidi ya ishirini unahangaika kusoma kwa tabu na uchungu mkubwa, utashangazwa. Utarudi mtaani kuwa boda boda.

Ewe mwanafunzi, kama uko shule achana nayo, kimbia haraka kaanze kujihangaikia.

Ewe mwanachuo, achana na habari hizo, ondoka hapo unapoteza muda. Unapoteza fedha nyingi kwenye sifuri.

Changamka. Ubodaboda hauhitaji digrii au cheti cha form four.

Achana na hiyo shule, anza sasa hivi kujifunza bodaboda utanishukuru. Usisubiri mpaka miaka 10 ijayo ukiwa umechoka na umeshapoteza fedha nyingi kwenye hamna.

Wenye masikio na wasikie. Wazazi amkeni. Shule ni ujinga.
Bro dunia ni pana,dunia haiishii kwenye mipaka ya bongo tu, huko kwenye bodaboda na Bajaj!
Ni Bora Uwe na graduate kibao wanaendesha bodaboda, kuliko kuwa na darasa LA Saba kibao wanaoendesha bodaboda!
Maisha kama uwanja wa Vita, kila silaha ni muhimu,ujuzi wa kukaanga chips, na shahada, vyote muhimu.
Mwenye shahada ya ufundi mitambo, akiendesha bodaboda! Atajifunza zaidi kutengeneza, atafungua gereji nk,
Dunia Ina fulsa nyingi, sie wabongo bado tunawaza kujitafuta hapa hapa bongo, umeishawahi kuona dakitari wa upasuaji, anaacha kazi, anaanzisha kampuni ya IT!, au, aliyesoma sheria anafungua kampuni ya video production!? Huo ndio u muhimu wa elimu,inakupa option kibao za kujipata! Acha mawazo mgando!
Fungua mtandao uone wanaijeria wanavyofanya! Wao wapo milioni 200+na bado wanasoma elimu ya juu! Sie tupo milioni 60 tu! Unataka vijana waache kusoma elimu ya juu!
Ushauri wangu, kwa vijana, soma vzr, faulu vzr, kizungu kipande vzr Sana, tafuta passport! Tafuta ajira ndani na nje ya mipaka!
Unaweza, ukawa umesoma sheria, au uhandisi, kuna short kozi za IT, piga hizo, ukipata pa kujishikiza, iwe ngazi, ya, kupandia tu.
 
Ungeshauri wachukuwe masomo yenye soko. Huwezi kuacha elimu kwani ni ufunguo wa maisha.
 
Back
Top Bottom