Harakati za ukombozi zina mambo mengi sana.
Na kwa vile huhusisha watu wengi wenye mawazo na mitazamo tofauti, kukwaruzana kwa hapa na pale ni jambo la kawaida sana na ni jambo linalotarajika.
Katika kufuatilia historia za harakati mbalimbali hapa duniani, sijawahi kuona popote pale ambako hakukuwa na tofauti miongoni mwa wanaharakati.
Ni harakati gani za ukombozi hapa Afrika ambazo wanaharakati wake hawakuwa na tofauti?
Wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika Kusini, si kila mtaka ukombozi alikubaliana na ANC.
Vilikuwepo vyama vingine ambavyo havikukubaliana na ANC.
Mojawapo ya hivyo vyama ni PAC [Pan Africanist Congress of Azania].
Hiki chama kiliundwa na wanachama wa ANC ambao hawakukubaliana na falsafa za hicho chama. Ndo mwaka 1959 wakajitoa na kuunda PAC.
Hata mwanzilishi wa Inkatha Freedom Party, Chief Mangosuthu Buthelezi, naye alikuwa mwanachama wa ANC aliyejitoa na kuunda IFP mwaka 1975.
Vyama vyote hivyo vilikuwa vinapingana na utawala wa kibaguzi wa makaburu.
Twende Marekani kwenye harakati za kupinga ubaguzi wa rangi.
Walikuwepo wanaharakati wengi tu ambao walikuwa hawakubaliani kwenye mambo mengi.
Baadhi yao wakaunda makundi yao ya kiuanaharaki.
Maarufu zaidi kuliko wengi walikuwa ni Martin Luther King Jr. na Malcolm X.
Kilikuwepo chama cha Black Panthers pia.
Baadaye kukaja kuwepo na Operation Breadbasket, Rainbow Push coalition, National Action Network, na kadhalika.
Martin Luther King Jr na Malcolm X walipingana katika baadhi ya mambo.
Kuna wakati mpaka Malcolm X akawa anamwita MLK “uncle Martin” [akimaanisha uncle Tom].
Jesse Jackson alijitoa kwenye Operation Breadbasket na kuunda Operation Push baada ya kukwazana na msaidizi wa MLK, Ralph D. Abernathy.
Hiyo ni mifano michache kati ya mingi iliyopo inayoonyesha kwamba wanaharakati kutofautiana, ni jambo la kawaida na hakumaanishi ni kupoteza mwelekeo.
Kwenu wanaharakati wa Tanzania, msiruhusi tofauti ndogo ndogo zichukue nafasi.
Tofauti za kimtazamo ni jambo la kawaida sana katika maisha ya binadamu.
Kuwa na mitazamo anuai ni jambo lenye afya. Walau linaonyesha mna ubongo unaofanya kazi.
Wanaharakati kwenye jamii ni watu muhimu sana. Wanafanya kazi zinazohitajika.
Huwa hakuna mabadiliko ya kijamii ambayo wanaharakati hawahusiki.
Shime wanaharakati wote wa Kitanzania. Nawaunga mkono.
Big man.
Wanaharakati kukosana ni kawaida, si kukosa muelekeo. Naelewa hili.
Ukimsoma mwanafalsafa maarufu wa Martinique, Frantz Fanon, aliyeandika sana kuhusu harakati za mapinduzi, hususan za vita ya ukombozi wa Algeria kutoka Wafaransa, kaandika jambo hili sana akiwapa moyo wanaharakati wasife moyo wanapokosana, hilo ni la kawaida.
Katika kitabu chake "The Wretched of The Earth" kuna chapter inaitwa "The Pitfalls of National Consciousness" kaelezea sana hili jambo katika muktadha wa kupigana dhidi ya ukoloni, akieleza kuwa hili jambo halitokei hivihivi tu mara nyingi linapandikizwa kimkakati na wakoloni (kwetu wakoloni weusi/ CCM).
Fanon kaelezea dominant power inavyogawanya watu kidini, kikabila, kikanda na kwa kuwagawa competing elites.
Ila pia, wanaharakati wanaweza kukosana, kukosana huko kukawa si kupoteza muelekeo, lakini wakawa wao wenyewe wanakosa muelekeo kwa kukosa focus kwenye mambo muhimu na kuwa easily distracted na sideshows.
Wanaharakati wa Tanzania wana tabia ya kushindwa ku stay on message, kushindwa ku focus kwenye big ticket items kama mabadiliko ya katiba na tume huru ya uchaguzi, kushindwa kuangalia big picture.
Wanataka kuwa commentators kwenye every breaking news, kutukana maadui zao personally kwenye every petty rumor, kuishia ku alienate hata potential allies in a way that shows lack of strategy.
Mfano, Maria Sarungi ukimsikiliza kwenye speech yake alivyopewa tuzo Oslo Norway, aliongea vizuri kama mtu anayeielewa dunia, akakemea udhalimu Tanzania. Akatoa a personal story yeye alivyobaguliwa wakati anakua Tanzania kwa sababu mama yake ametoka Hungary.
Alikemea ubaguzi, wa rangi, wa kabila etc. It was a powerful speech. Watanzania wakiongea majukwaa ya kimataifa huwa napata tabu sana ku hold my breath kwa jinsi wanavyoshindwa content and delivery. But Maria killed it, content, delivery, poise, kila kitu.
Fast forward karudi nyumbani, amekuwa unhinged against Wazanzibari kila siku X/Twitter. Ubaguzi usio hata na qualification kwamba kuna Wazanzibari wengine wa CUF/ ACT pia hawaipendi CCM na hawaupendi Muungano pengine anaweza kushirikiana nao kuitoa CCM au hata kuuvunja muungano.
Najua tumeumizwa, tuna machungu, ni rahisi kuwa na kneejerk reaction, kusema fvck it, it's on. But that is not the character of a leader of a political movement.
Kawa unhinged against Wazanzibari in a very simplistic way. Wafuasi wake ana wa egg on badala ya yeye kuwa moderate.
Mimi ninaona this is racist, simplistic, not strategic and it contradicts her Oslo message. Anaonekana si activist wa principle, ni wa convenience tu. The end justifies the means, whatever works, hata unnecessarily incendiary racist language
Na hapo utaona watu kama Fatma Karume hawapo sana kwenye kumsema Samia sasa maana labda wanaona si Wazanzibari wote tunajumuishwa na Samia, so why bother? Fatma mwanzo alikuwa anamsema Samia, kuna siku aliambiwa Samia kaaibisha wanawake wa Tanzania hawatapewa urais tena, akajibu akasema Samia kajiaibisha mwenyewe, hawawakilishi wanawake wa Tanzania. Kuna Wazanzibari wengi hawaipendi CCM, hawa wa CUF/ ACT, lakini wanaona wanabaguliwa na kina Maria Sarungi.
Wameshindwa kuingia katika a big tent coalition against CCM na Maria.
Kwa hiyo, in her zeal for Tanganyika, she is sacrificing core principles against discrimination alizozisema yeye mwenyewe Oslo.
Even if Fatma is a sellout/coward/collaborator, as some are bound to say, bado kuna Wazanzibari wengi tu hawampendi Samia, hawaipendi CCM, hawaupendi muungano, na hawahusiki na mabaya yoyote yanayoendelea. These people should be her allies in her goal, she is alienating them. Na hawa wapo wengi tu huko Pemba, Unguja, tangu CUF na sasa ACT na mpaka CCM.
Na kuna watu wa bara wengi tu wanafanya kazi na Samia na kumu enable.
Maria and Mange are sympathizing with Mwigulu Nchemba because of this Uzanzibari vs Utanganyika bullshit, while Mwigulu is a Samia enabler and a CCM cadre through and through. Wameshindwa ku focus kuona CCM ndiyo tatizo hapa.
So this whole "Wazanzibari" blatant discrimination is a counterproductive sideshow.
These are Samia's cronies. Call them out for that, not Uzanzibari.
Na uninga zaidi, kabla ya kuwamaliza Wazanzibari, tushaanza kuwarukia Wachaga. Watu wanapoteza focus ya kutaka kuitoa CCM, wanaanza kuwaandama Wazanzibari, na sasa Wachaga.
Naona kuna hasira fulani hivi ya ku personalize mambo against Samia, wakati tatizo ni systemic, ni CCM, si Samia tu. Sasa hawa wanaharakati wanaokuwa gung ho against Samia with all these ad hominem attacks against her, wanamuita kimama, kibibi, bila ku follow the money sufficiently, bila kudai transparency sufficiently, bila policy critiques, bila ku underline kuwa hata angeondoka Samia na kuja Nchimbi CCM ni ile ile, wanakuwa wamepoteza muelekeo tu. Hata mmoja mmoja bila kuangalia kama wanakosana.
Wanadandia any latest headline na kuifanya hoja, ndiyo maana vita za ndani ya CCM kama ya Polepole na Samia imewafanya wamuone Polepole hero wao. Polepole was trying to bring back Magufulism for fvcks sake!
Na sasa Nchimbi aliyeshiriki kuiba uchaguzi na Samia kapotezwa, washamfanya hero wao mwingine.
Wanapoteza focus mmoja mmoja (bila kujali suala la kufarakana wao kwa wao) hata kama kukosana ni jambo la kawaida.