Wanajeshi 60 wa Tanzania huko Afrika ya kati kurejeshwa nyumbani kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono

Ubakaji unaozungumzwa hapo sio ule wakutumia nguvu kumwingilia mwanamke bali hata kama amekubali lakini yuko chini ya ulinzi wako then umebaka. Wanaweza wakawa walikubaliana kabisa kufanya tendo la ndoa lakini kwa kuwa hao wanajeshi walikuwa kwenye mission ya UN basi kisheria za kimataifa watakuwa wanahesabika wamebaka.
Soma taarifa hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza,kuna hadi watoto,mtoto huwezi kufanya makubaliano nae.Kuna mengi yanafanyika katika utendaji kazi wa watu wanaopewa dhamana flani kwenye jamii flani.Hukuwahi kumsikia MAMA akisisitiza kuwe na siri maofisini,we unafikiri mangapi yanafanyika maofisini,yanamalizwa kimyakimya?
Vipi mdada ambaye yupo JKT na ni mzuri,unadhani hawatakwi na baadhi ya askari na mwishowe wanaliwa,ulishasikia inaripotiwa?Tulia.
 
Naona umechanganya mambo mengi mara JKT, maofisini, watoto. Sasa sijui nikujibu vipi? Ngoja nianze na watoto uelewe kuwa mtoto kwa mujibu wa sheria za kimataifa ni yule ambaye hajatimiza miaka 18 kama sikosei. Sasa niambie kwa watoto wa kike wa Kiafrika kwa maumbo yao unaweza kugundua kuwa ana umri chini ya miaka 18? Ukitilia maanani kama yeye amekubali? Kwa hao wa JKT na Maofisini wengi wao wanapenda ili wapate unafuu kwenye shughuli zao.
 
JKT watu wanabakwa sana ila wengi huogopa sema wamebakwa wanaamua kukaa kimya na hiyo siri
2017 nikiwa mujibu wa sheria 821KJ bulombora CO kanole kuna mujibu alibakwa na service man sema ishu ikafichwa ikaonekana kama mwana alitaka kumbaka ndio watu wakatokea hahahaha hii story haikuongia akilini na hata demu aliyebakwa sikuwahi kumjuaa kama alifichwa hv ila kimazingira ni mzigo uliliwa

JkT mujibu ni kweli kuna manyanyaso ya kingono kwa watt wa kike
 
na mjadara wetu wa jkt kunyanyasa watoto wa kike wale wa mujibu wa sheria uendelee, kuna ukweli hapa....jeshi likishakuwa la kujuana tayari uadilifu unapungua.... by the way wanajeshi siyo watumishi wa umma mikataba yao ya ajira isitishwe mara moja na wahukumiwe mara moja.
Umma ninini?Mi najua umma kwa tafasiri isiyo rasmi,ni sisi wananchi,ukijumuisha na majeshi yetu,inakuaje watu wa majeshi kua siyo watumishi wa umma?
 
Wamesema usimamiz wao ulikuwa wa kiwango kidogo,wacha warudi home wakaripot kambin kufyeka nyasi Sasa🤣si wamezikataa dollars za mmarekani🤔 ngoja waje waanze kunywa vya kupima🤣🤣

Mule mule yaani huku makambini bakabaka ndio shughuli zetu hizi makapera kufyeka nyasi tukisimamiwa na maafisa
 
Hivi wewe una akili timamu??
Wewe ndio una akili timamu!? Badala ya kushangaa waliobaka unanishangaa mimi!? Any way hata kuwa mwanajeshi huwezi kujitenga na matamanio ya mwili ila Cha Muhimu ni makubaliano ya wawili!!, Ila kufanya bila ridhaa ni big no!! Unakumbula enzi za Rahabu, kwenye Holy books
 
Nina wasiwasi Hawa UN wakiona kikosi frani kina fanya vizuri kudhibiti uharamia eneo husika basi huwa taftia sababu au case ili waondoke
Kwani ni mwiba kwao
 
Wewe ndio una akili timamu!? Badala ya kushangaa waliobaka unanishangaa mimi!? Any way hata kuwa mwanajeshi huwezi kujitenga na matamanio ya mwili ila Cha Muhimu ni makubaliano ya wawili!!, Ila kufanya bila ridhaa ni big no!! Unakumbula enzi za Rahabu, kwenye Holy books
Uelewa wenu mdogo,hao hawajafanya mapenzi bila ridhaa wala hawajaforce..ukiwa Mlinda amani wa UN hurusiwi kufanya mapenzi na raia wa nchi hyo mnaowalinda Kwa makubaliano yenu,ikijulikana au kuonekana wao wanahesabu umebaka..umetumia kipato chako au uwezo wako wa kijeshi kulazmisha
 
Walinda amani wa Tanzania kurejeshwa nyumbani kutokana na madai ya utovu wa nidhamu CAR

9 Juni 2023Haki za binadamu

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) chenye makao yake makuu mjini Bangui, kimetangaza uamuzi wa Sekretarieti, kuwarudisha nyumbani kikosi cha wanajeshi 60 wa Tanzania, waliokuwa wametumwa katika kambi ya muda ya operesheni katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo kufuatia madai makubwa ya matendo ya unyanyasaji wa kingono yanayodaiwa kutekelezwa na walinda amani hao, msemaji wa Umoja wa Mataifa amewaeleza walinda waandishi wa Habari hii katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Stéphane Dujarric, amesema, "Uamuzi huo unakuja baada ya uchunguzi wa awali ambao ulipata ushahidi wa kuaminika kwamba walinda amani 11 wa kitengo hicho walidaiwa kujihusisha na unyanyasaji wa kingono kwa waathirika wanne.”

Akifafanua zaidi Dujarric amesema, “Waathiriwa waliotambuliwa wanapatiwa matunzo na usaidizi kutoka kwa wadau wa operesheni za kibinadamu. MINUSCA pia imetuma timu ili kuzungumza zaidi na jamii.

Tanzania imetuma wachunguzi

Kwa mujibu wa Dujarric, “Mamlaka za Tanzania zimearifiwa rasmi na zimetuma maafisa wa uchunguzi wa kitaifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Katika kuthibitisha dhamira yao ya kutovumilia kabisa unyanyasaji wa kijinsia na kingono, mamlaka za Tanzania zilibaini uzito wa tuhuma hizo na wamejitolea kuchukua hatua zinazohitajika kushughulikia masuala haya.”

Msemaji huyo amesema, “Kikosi kimehamishwa na kupelekwa katika kambi nyingine huku uchunguzi ukiendelea, na wahusika wa kitengo hicho wamezuiliwa kwenye kambi, hii ni kwa ajili ya kuwalinda waathirika na bila shaka uadilifu wa uchunguzi. Kikosi hicho kitarejeshwa nyumbani pindi ambapo uwepo wao hautahitajika tena kwa wachunguzi.”

Vilevile Dujarric ameeleza, “Uamuzi wa Sekretarieti kurudisha kikosi hiki ni kwa mujibu wa azimio namba 2272 la Baraza la Usalama, ambapo Baraza 'linaidhinisha uamuzi wa Katibu Mkuu wa kurudisha nyumbani kikosi fulani cha kijeshi au kuunda kitengo cha polisi cha kikosi wakati kuna ushahidi wa kuaminika wa unyanyasaji wa kingono ulioenea au wa kimfumo unaofanywa na kitengo hicho'.

Msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, "Umoja wa Mataifa unasalia na nia ya kutekeleza kwa dhati sera ya Katibu Mkuu ya kutovumilia kabisa unyonyaji na unyanyasaji wa kijinsia."

=====
The United Nations will send home a unit of 60 Tanzanian peacekeepers over allegations of sexual exploitation and abuse in the Central African Republic, the UN announced on Friday.

A preliminary investigation found “credible evidence” that eleven members of the unit were involved in sexual exploitation and abuse of four victims, UN spokesman Stephane Dujarric said.

Two of the alleged victims are children, according to UN figures.

Investigators also identified a breakdown in commanders’ authority and management of staff, according to a press release by the UN’s mission in the country.

The victims have received care from humanitarian groups working with the UN, according to their “medical, psychosocial and protection” needs, it said.

The UN has had a mission in the conflict-torn Central African Republic since 2014, where thousands of peacekeepers have been deployed.

The eleven suspects had been working at a temporary base in the west of the country. The Tanzanian unit has now been relocated to another base and its members confined to the barracks.

“The unit will be repatriated once their presence is no longer required by the investigation,” Dujarric said.

Tanzanian authorities have also dispatched investigation officers to the Central African Republic.

There have been allegations of sexual abuse or exploitation against Tanzanian peacekeepers – largely in the Democratic Republic of Congo – every year since at least 2015, UN figures show.

Hii taswira mbaya sana kwa Jeshi letu.
Kitu pekee watanganyika wanakimudu ni zinaa, ushabiki wa mipira, uchawi na chuki.
 
Anaekurupuka ni wewe unaebaka haki za watu na hutaki ukweli ujulikane Tanzania ngono ndio kipaumbele na ukimwi umeshamiri ndio nchi ya wajinga mpaka leo bado wanaanbukizana ukimwi wakati duniani kote maambukizi yamepungua
😀😀😀😀aisee
 
Umma ninini?Mi najua umma kwa tafasiri isiyo rasmi,ni sisi wananchi,ukijumuisha na majeshi yetu,inakuaje watu wa majeshi kua siyo watumishi wa umma?
wale siyo watumishi wa umma, sema upumbavu wa wanasiasa kuwapa nyazifa za kisiasa, mpaka wakuu wa mashirika ya umma...
 
Walinda amani wa Tanzania kurejeshwa nyumbani kutokana na madai ya utovu wa nidhamu CAR

9 Juni 2023Haki za binadamu

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) chenye makao yake makuu mjini Bangui, kimetangaza uamuzi wa Sekretarieti, kuwarudisha nyumbani kikosi cha wanajeshi 60 wa Tanzania, waliokuwa wametumwa katika kambi ya muda ya operesheni katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo kufuatia madai makubwa ya matendo ya unyanyasaji wa kingono yanayodaiwa kutekelezwa na walinda amani hao, msemaji wa Umoja wa Mataifa amewaeleza walinda waandishi wa Habari hii katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Stéphane Dujarric, amesema, "Uamuzi huo unakuja baada ya uchunguzi wa awali ambao ulipata ushahidi wa kuaminika kwamba walinda amani 11 wa kitengo hicho walidaiwa kujihusisha na unyanyasaji wa kingono kwa waathirika wanne.”

Akifafanua zaidi Dujarric amesema, “Waathiriwa waliotambuliwa wanapatiwa matunzo na usaidizi kutoka kwa wadau wa operesheni za kibinadamu. MINUSCA pia imetuma timu ili kuzungumza zaidi na jamii.

Tanzania imetuma wachunguzi

Kwa mujibu wa Dujarric, “Mamlaka za Tanzania zimearifiwa rasmi na zimetuma maafisa wa uchunguzi wa kitaifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Katika kuthibitisha dhamira yao ya kutovumilia kabisa unyanyasaji wa kijinsia na kingono, mamlaka za Tanzania zilibaini uzito wa tuhuma hizo na wamejitolea kuchukua hatua zinazohitajika kushughulikia masuala haya.”

Msemaji huyo amesema, “Kikosi kimehamishwa na kupelekwa katika kambi nyingine huku uchunguzi ukiendelea, na wahusika wa kitengo hicho wamezuiliwa kwenye kambi, hii ni kwa ajili ya kuwalinda waathirika na bila shaka uadilifu wa uchunguzi. Kikosi hicho kitarejeshwa nyumbani pindi ambapo uwepo wao hautahitajika tena kwa wachunguzi.”

Vilevile Dujarric ameeleza, “Uamuzi wa Sekretarieti kurudisha kikosi hiki ni kwa mujibu wa azimio namba 2272 la Baraza la Usalama, ambapo Baraza 'linaidhinisha uamuzi wa Katibu Mkuu wa kurudisha nyumbani kikosi fulani cha kijeshi au kuunda kitengo cha polisi cha kikosi wakati kuna ushahidi wa kuaminika wa unyanyasaji wa kingono ulioenea au wa kimfumo unaofanywa na kitengo hicho'.

Msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, "Umoja wa Mataifa unasalia na nia ya kutekeleza kwa dhati sera ya Katibu Mkuu ya kutovumilia kabisa unyonyaji na unyanyasaji wa kijinsia."

=====
The United Nations will send home a unit of 60 Tanzanian peacekeepers over allegations of sexual exploitation and abuse in the Central African Republic, the UN announced on Friday.

A preliminary investigation found “credible evidence” that eleven members of the unit were involved in sexual exploitation and abuse of four victims, UN spokesman Stephane Dujarric said.

Two of the alleged victims are children, according to UN figures.

Investigators also identified a breakdown in commanders’ authority and management of staff, according to a press release by the UN’s mission in the country.

The victims have received care from humanitarian groups working with the UN, according to their “medical, psychosocial and protection” needs, it said.

The UN has had a mission in the conflict-torn Central African Republic since 2014, where thousands of peacekeepers have been deployed.

The eleven suspects had been working at a temporary base in the west of the country. The Tanzanian unit has now been relocated to another base and its members confined to the barracks.

“The unit will be repatriated once their presence is no longer required by the investigation,” Dujarric said.

Tanzanian authorities have also dispatched investigation officers to the Central African Republic.

There have been allegations of sexual abuse or exploitation against Tanzanian peacekeepers – largely in the Democratic Republic of Congo – every year since at least 2015, UN figures show.

Hii taswira mbaya sana kwa Jeshi letu.
Siyo kwa jeshi tuu ni kwa Taifa kwa ujumla
 
Back
Top Bottom