Wanajeshi 60 wa Tanzania huko Afrika ya kati kurejeshwa nyumbani kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono

Wanajeshi 60 wa Tanzania huko Afrika ya kati kurejeshwa nyumbani kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono

Anaekurupuka ni wewe unaebaka haki za watu na hutaki ukweli ujulikane Tanzania ngono ndio kipaumbele na ukimwi umeshamiri ndio nchi ya wajinga mpaka leo bado wanaanbukizana ukimwi wakati duniani kote maambukizi yamepungua
Tatizo lako huna exposure ya kimataifa ndio maana una sema hivyo kijumlajumla tu!
 
""Mlinda Amani,,anamnyanyasa Kingono,,Muhitaji Amani,,,Sidhani kama hiyo AMANI itapatikana??
 
Pamoja na kuikomboa Uganda, lakini jeshi letu lilijizolea sifa ya ukwapuaji huko Uganda . Nilidhani waliacha
Ni kweli kabisa unachosema, nimewahi kuwapo kwenye "mission" fulani sehemu moja mbali huko iliwajumuisha na raia wa Uganda. Hao Waganda waliniambia kwamba hawatumii lugha ya Kiswahili kwa sababu hiyo ni "lugha ya WEZI". Nilipodadisi kwa undani zaidi niligundua kwamba sababu ya wao Waganda kuamini kwamba Kiswahili ni lugha ya wezi ni kutokana na madhila waliyopata kutoka kwa Wanajeshi wa Tanzania wakati wa vita ya Kagera.
 
Wamelichafua jeshi na nchi hao wahuni wakirudi nchini naomba washughulikiwe
 
Anaekurupuka ni wewe unaebaka haki za watu na hutaki ukweli ujulikane Tanzania ngono ndio kipaumbele na ukimwi umeshamiri ndio nchi ya wajinga mpaka leo bado wanaanbukizana ukimwi wakati duniani kote maambukizi yamepungua
Wapi nimetaka ukweli usijulikane? Wapi nimetetea hayo matendo? Acha ukurupukaji.
 
hawawezi kushughulikiwa Kwa sababu jeshi Hilo lilifanya unyanyasaji pale MKIRU,KIBITI
 
Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN, Stéphane Dujarric, amesema, "Uamuzi huo unakuja baada ya uchunguzi wa awali ambao ulipata ushahidi wa kuaminika kwamba walinda amani 11 wa kitengo hicho walidaiwa kujihusisha na unyanyasaji wa kingono kwa waathirika wanne.”

Akifafanua zaidi Dujarric amesema, “Waathiriwa waliotambuliwa wanapatiwa matunzo na usaidizi kutoka kwa wadau wa operesheni za kibinadamu. MINUSCA pia imetuma timu ili kuzungumza zaidi na jamii.

Tanzania imetuma wachunguzi​

Kwa mujibu wa Dujarric, “Mamlaka za Tanzania zimearifiwa rasmi na zimetuma maafisa wa uchunguzi wa kitaifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Katika kuthibitisha dhamira yao ya kutovumilia kabisa unyanyasaji wa kijinsia na kingono, mamlaka za Tanzania zilibaini uzito wa tuhuma hizo na wamejitolea kuchukua hatua zinazohitajika kushughulikia masuala haya.”

Msemaji huyo amesema, “Kikosi kimehamishwa na kupelekwa katika kambi nyingine huku uchunguzi ukiendelea, na wahusika wa kitengo hicho wamezuiliwa kwenye kambi, hii ni kwa ajili ya kuwalinda waathirika na bila shaka uadilifu wa uchunguzi. Kikosi hicho kitarejeshwa nyumbani pindi ambapo uwepo wao hautahitajika tena kwa wachunguzi.”

Vilevile Dujarric ameeleza, “Uamuzi wa Sekretarieti kurudisha kikosi hiki ni kwa mujibu wa azimio namba 2272 la Baraza la Usalama, ambapo Baraza 'linaidhinisha uamuzi wa Katibu Mkuu wa kurudisha nyumbani kikosi fulani cha kijeshi au kuunda kitengo cha polisi cha kikosi wakati kuna ushahidi wa kuaminika wa unyanyasaji wa kingono ulioenea au wa kimfumo unaofanywa na kitengo hicho'.

Msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, "Umoja wa Mataifa unasalia na nia ya kutekeleza kwa dhati sera ya Katibu Mkuu ya kutovumilia kabisa unyonyaji na unyanyasaji wa kijinsia."

Chanzo: Umoja wa Mataifa
 
Hapo utakuta Wanawake wakicongo walifall in love na wajuba toka TZ wakawa wanawatega wahuni wakapiga na kusepa means kuna wengine waliachwa wakiwa na watoto sasa kama unavyojua fitina za single maza hazimuachi mtu salama.
Sio fitna za single mothers, mwanaume kama unacho cha kupoteza jifunze kufunga zipu yako, waza maili kadhaa. Waache watu ambao hawana cha kupoteza wakitembeze.

Kama una kazi reputable utaelewa ninachosema. Ngono ya mara moja inaweza kukucost a thousands..
 
Ni kweli kabisa unachosema, nimewahi kuwapo kwenye "mission" fulani sehemu moja mbali huko iliwajumuisha na raia wa Uganda. Hao Waganda waliniambia kwamba hawatumii lugha ya Kiswahili kwa sababu hiyo ni "lugha ya WEZI". Nilipodadisi kwa undani zaidi niligundua kwamba sababu ya wao Waganda kuamini kwamba Kiswahili ni lugha ya wezi ni kutokana na madhila waliyopata kutoka kwa Wanajeshi wa Tanzania wakati wa vita ya Kagera.
Na wewe ukawaamini kwa maneno yao hayo?
 
Sio fitna za single mothers, mwanaume kama unacho cha kupoteza jifunze kufunga zipu yako, waza maili kadhaa. Waache watu ambao hawana cha kupoteza wakitembeze.

Kama una kazi reputable utaelewa ninachosema. Ngono ya mara moja inaweza kukucost a thousands..
Akili nyingi sana
 
Kwanini wasiwafanyie relocation wawapeleke Somalia?Anyway wamezingua sana,tena kimataifa duuuh! ukiona hivyo ujue imepitiliza.Sijui kwa vijana wa kike wanaoenda JKT inakuaje,watajijua wenyéwe.
 
Kwanini wasiwafanyie relocation wawapeleke Somalia?Anyway wamezingua sana,tena kimataifa duuuh! ukiona hivyo ujue imepitiliza.Sijui kwa vijana wa kike wanaoenda JKT inakuaje,watajijua wenyéwe.
Ubakaji unaozungumzwa hapo sio ule wakutumia nguvu kumwingilia mwanamke bali hata kama amekubali lakini yuko chini ya ulinzi wako then umebaka. Wanaweza wakawa walikubaliana kabisa kufanya tendo la ndoa lakini kwa kuwa hao wanajeshi walikuwa kwenye mission ya UN basi kisheria za kimataifa watakuwa wanahesabika wamebaka.
 
Back
Top Bottom