Wanajeshi 60 wa Tanzania huko Afrika ya kati kurejeshwa nyumbani kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono

Hawabaki, sawasawa na chuoni mwanachuo kuwa na mahusiano na lecture au mkufunzi, kutaka unafuu fulani, kwakuwa wanakuwa watoto ndo kubaka kwenyewe, Kama mtu unabakwa si unakimbia kambi, unatoroka pori kwa pori, unarudi home.
 
jeshi la nchi za kiarabu misri algeria sudan uae kuweit yemen rusia saudia china korea wapi ulisikia jeshi la nchi hizi zinabaka wanawake?
Fuatilia kabla hujataja jeshi la nchi yeyote , kutowasikia haimaanish hawafanyi , bali fuatilia kwanza
 
Mkuu, Una Experience na nchi gan zingine ulowahi fika na kufaham tabia na vipaumbele vyao, hadi uka conclude kuwa Tanzania ndo giant wa ngono?
Sw ila tukemee hao wachache , lasivyo utakemea siku umebakwa ww au kabakwa mtu wa karibu yako
 
Yote haya wameyataka ccm
 
We hujui wale mademu wanatumia kama fursa ya kupata msaada wa UN hawajabakwa hao basi tu jumba bovu ili wapone njaa zao
Kwamb hao wanajeshi hawajui kuwa ni htr kuwa krb na hao wenyej wanaolindwa ?
 
Sio kwamba wanabaka directly Mzee..once ukitoka uku kwenda kulinda amani hutakiwi kufanya mapenzi na raia yeyote wa kule ata kama mmekubaliana inahesabika umebaka,ikijulikana au ukionwa tu kibarua huna tena uko Kwa taratibu zilivyo
Je wao hawaamim kuwa hao wanajeshi wana hisia , au ndo uchochez wa ushoga huu , tungekuwa na kiongoz timamu angekuwa anaomba wanajeshi wake wawe wanapewa muda wa kuja kufurahi na familia ili hisia zipungue
 
Je wao hawaamim kuwa hao wanajeshi wana hisia , au ndo uchochez wa ushoga huu , tungekuwa na kiongoz timamu angekuwa anaomba wanajeshi wake wawe wanapewa muda wa kuja kufurahi na familia ili hisia zipungue
Ndo maana wanapewa likizo kiongozi baada ya miezi.6
 
Umoja wa Mataifa ilitangaza Ijumaa (Juni 9) kuwa kikosi cha walinda amani 60 kutoka Tanzania kitarejeshwa nyumbani kutokana na madai makubwa ya unyanyasaji wa kingono.

Akiongea kutoka New York, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema uchunguzi wa awali ulibaini kuwepo kwa waathirika 4.

"Mamlaka za Tanzania zimearifiwa rasmi na wamewatuma maafisa wa uchunguzi wa kitaifa kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati..."

Ushahidi ulioaminika ulipatikana dhidi ya wanajeshi 11 wa kikosi hicho kilichokuwa katika kituo sehemu ya Magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

"Kikosi hicho kimehamishwa kwenye kambi nyingine wakati uchunguzi unaendelea, na wanajeshi wa kikosi hicho wamezuiliwa kwenye makambi ya kijeshi, hii ni ili kulinda waathirika pamoja na uadilifu wa uchunguzi," alisema Dujarric.

"Kikosi hicho kitarejeshwa nyumbani mara tu uwepo wao hautahitajika tena katika eneo la tukio kwa mujibu wa wachunguzi..."

Dujarric alifafanua: "Uamuzi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kuwarejesha nyumbani wanajeshi hawa" ulizingatia azimio 2272 la Baraza la Usalama "ambapo Baraza linakubali uamuzi wa Katibu Mkuu wa kuwarejesha nyumbani kikosi cha kijeshi au kikosi cha polisi cha kikosi cha walinda amani fulani wakati kuna ushahidi unaokubalika wa unyanyasaji wa kingono uliokithiri au wa mifumo kutoka kwa kikosi hicho."

Umoja wa Mataifa ilirekodi kwenye tovuti yake kuwa tangu 2015, kulikuwa na tuhuma 254 za unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanajeshi wake katika Ujumbe wake wa Umoja wa Mataifa wa Kuhuisha na Kuleta Utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati au MINUSCA.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, alitangaza mapema katika utawala wake sera ya "kutovumilia" unyanyasaji wa kingono na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, akiwataka Mataifa Wanachama kusaini mkataba wa hiari kuhusu kuzuia na kushughulikia janga hilo, mwaka 2017.

Tuhuma za unyonyaji na unyanyasaji wa kingono na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kote duniani ni pana.

Africa News
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…