Tetesi: Wanajeshi wa Tanzania na wenzao wa SADC Washikiliwa Mateka kama Mateka wa Vita na Wanamgambo wa M23 huko Goma

Tetesi: Wanajeshi wa Tanzania na wenzao wa SADC Washikiliwa Mateka kama Mateka wa Vita na Wanamgambo wa M23 huko Goma

Kuhusu majeruhi askari 190 wa SAMIDR SADC wanajeshi kutoka nchi za South Africa, Tanzania na Malawi walivyohudumiwa kiutu na M23 kisha walivyowezeshwa kuvuka mpaka chini ya uangalizi wa M23 kutoka Goma Kivu Mashariki ya Congo hadi Kigali na kuhudumiwa kama mkataba wa Geneva kwa kuheshimu utu ikiwemo kutowapiga picha kwa ajili ya kurusha mitandaoni

25 February 2025
Dar es Salaam, Tanzania

Hakuna jeshi lililokuwa na ndege yenye uwezo wa kuwasafirisha wanajeshi waliojeruhiwa vitani DRC kurudi nyumbani - Theletsane


View: https://m.youtube.com/watch?v=-SLqLuk8rXg
hayo yamebainishwa katika mahojiano.

Mkurugenzi wa Ogani ya Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa SADC Profesa Kula Theletsane anasema hakuna kikosi chochote cha kijeshi cha nchi katika kanda hiyo ya SADC ikiwa ni pamoja na jeshi la ulinzi la South Africa SANDF, kilikuwa na ndege yenye uwezo wa kuwasafirisha kurudi nyumbani wanajeshi waliojeruhiwa vitani kutoka DRC. Anasema badala yake ilitumiwa ndege ya kibinafsi charter .

Habari zaidi zinasema kuwa jijini Dar es Salaam mkutano wa wakuu wa kijeshi wa nchi za SADC wanakutana kutekeleza maazimio ya mkutano wa wakuu wa nchi za SADC na EAC uliofanyika Dar es Salaam 08 February 2025 ambapo wakuu hao wa nchi walikubaliana kuwa sahihi ni kufungua jukwaa la mazungumzo kwa kuwa njia za kijeshi pekee haziwezi kumaliza mzozo wa Mashariki ya Congo...

SADC’s Director of Organ on Politics Defence and Security Affairs Professor Kula Theletsane says none of the military units in the region including SANDF, had a plane with the capacity to transport back home the wounded soldiers from DRC. He says a private plane was used instead.

Kumbukumbu zangu zinaniambia askari wetu wote waliopo east congo,wakimaliza operation zao upitia rwanda kurudi nyumbani,tuache hizi propaganda
 
Hii ni akili matope?
Mhariri ni mnyarwanda unategemwa amkaange Kagame?
Jamaa bwege sana huyo yaani kabisa anatuletea habari ambayo imehaririwa na Mnyarwanda anataka ndio tuiamini? Eti Tshekeds alikuwa anajiandaa kuivamia Rwanda serious? Hata mtoto mdogo anayefuatilia hii battle hawezi kukubqliqnq nq huo uongo.
 
Nchi yoyote inayoendekeza uchawa, inadumaza weledi na ubunifu wa taasisi zote. Kipindi hiki tuombe sana tusivamiwe na nchi yoyote ile, tutapoteza kila kitu.

Hata taasisi zilizotakiwa kuzingatia weledi zimejiingiza kwenye siasa na uchawa, matokeo mengi ya kushindwa na ya aibu, tuyatarajie siku za usoni.
Moja ya vitu ambavyo vinaua uzalendo kwa kasi ni uchawa na ubinafsi.

Naamini kabisa kwa hali ilivyo hapa nchini vijana ambao wako tayari kulisaliti taifa lao wakitangaziwa dau na maadui ni wengi sana, maana kwanza wana hasira na serikali na hali ngumu ya kimaisha wakati huo kuna mafisadi yananeemeka huko juu.
 
Kagame ukiendekeza mazungumzo na yeye ndo anakupanda kichwani. Huyu dawa yake ni kumfanyia mafia tu na baadae kumpotezq kabisa.
Kagame alishatingisha kiberiti akaona sisi ni wepesi na ana tumudu vizuri kabisa, ndio maana huwa anajiamini kupita kiasi dhidi yetu.

Licha ya kwamba sisi ndio tumeshikiria uchumi wa nchi yake kwa asilimia kadhaa(kwenye suala zima la logistics) ila ana kiburi cha kutuvimbia na wala hatuogopi... sidhani kama angekuwa ndio Uhuru au Ruto anatawala hapa kwetu angekuwa na kiburi hicho.
 
Kilichoniuma ni heshima aliyopewa Kagame alipokuja pale Airport wakati vijana wetu wameshikiliwa mateka na vikosi vyake.

Sijui tumekuwaje Tanzania.
Mkuu, Jeshi letu linatumika kisiasa zaidi na ndio maana tumefika hatua hii. Inasikitisha sana kuona tumejiingiza katika mgogoro unaotuvunjia heshima.
 
DR Congo zenye makandokando (complexity) ya kuvuta na kupiganisha majeshi ya nje ndani ya DR Congo huku suluhu ya kudumu ya amani na usalama kushindwa kupatikana kutokana na makundi mengi kushirikishwa.

Pamoja na majeshi ya kigeni Angola, Namibia, Zimbabwe, kuwa na vifaa kibao, pesa ndefu ya askari wa kulinda amani ya Umoja wa Mataifa, morali vita vya Congo, maelfu ya askari wa kulinda Amani chini ya mwamvuli wa UN / SADC / EAC lakini imefahamika kuwa mwenyeji aliyepo madarakani Kinshasa kama mtawala (serikali ya Congo ) ndiyo mchawi mkuu anayetumika kuhujumu juhudi zote za nchi jirani, kikanda na kimataifa

TOKA MAKTABA :
Jeshi imara la South Afrika tangu 2016 misheni zake Congo zimeshindwa pamoja na kuwa wana zana kali za kisasa :

View: https://m.youtube.com/watch?v=x6BYYyukjDI
Hii 𝘀𝘁𝗼𝗿𝘆 ilirushwa mara ya kwanza 𝟭𝟴 𝗦𝗲𝗽𝘁𝗲𝗺𝗯𝗲𝗿 𝟮𝟬𝟭𝟲.

Akisindikizwa na helikopta maarufu ya Rooivalk mfano wa ngome yenye ulinzi uliosheheni silaha kali , Carte Blanche anasafiri hadi kambi ya kijeshi iliyotekwa hivi majuzi ndani ya misitu ya tropiki kaskazini mwa Beni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

John Webb anapata ruhusa ya kipekee kuvifikia vituo vya mstari wa mbele vya jeshi la South Africa SANDF katika eneo maarufu la liliopachikwa jina la kuogofya la Pembe Tatu ya Mauti (Triangle of Death) katika Mkoa wa Kivu Kaskazini tunapowatembelea wanajeshi wetu walio mstari wa mbele katika vita dhidi ya waasi wa ADF.

Tunakutana na wanajeshi ambao uMauti umeshindwa kuchukua roho zao katika uwanja wa vita na vile vile katika majukumu muhimu ya usaidizi wa mapigano, na marubani wa SANDF wanaofanya kazi kama sehemu ya kitengo cha anga cha Umoja wa Mataifa ambao wamekuza sifa ya ustadi na ujasiri wa kufika maeneo haraka kupambana na adui.

Carte Blanche pia anakutana na Jenerali wa SANDF Derrick Mgwebi ambaye aliteuliwa kuongoza operesheni ya jumla ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini DRC - ambayo bado ni Misheni kubwa zaidi ya kulinda amani duniani.
 
Cha kufurahizha kuna wanajeshi wawili wa kike wa South Africa ni wajawazito.
Kati ya kipindi ambacho Rwanda alijiandaa kutufanya SADC kuonekana wajinga ni kipindi hiki.

Na wanatangaza kweli kuwa askari wa Afrika Kusini walipata ujauzito Congo. Intergenerational taswira kama wale wana jeshi la wapigana miti tu ndo mana waliuwawa na kutekwa.

Kagame ni wa kushughulikiwa kwa gharama yeyote ile.
 
Back
Top Bottom