Wanajeshi wa Uingereza wanaacha kazi ya jeshi licha ya malipo bora

uingereza aliwahi kumvamia nani akiwa peke yake?
unaongelea historia ya miaka ya 1900 huko sio?
 
Vita hizo uingereza huzifuata mwenyewe, uingereza ingepakana na ujerumani kama poland, ingekua mhanga wa kwanza,kwa kipindi kile isingewezekana hitler avuke nchi zote aingie uingereza
Lakini Uingereza ikaweza kuvuka bahari kuifuata Ujerumani si ndio?

Hitler alijaribu kuvuka bahari kuifuata Uingereza ila Royal Navy ilikuwa na nguvu kuzidi Kriegsmarine. Royal Airforce iliweza kukabiliana na nguvu za Luftwaffe.
Kasome The Battle of Britain, Hitler alibeba maelfu ya ndege na melivita kupigana Uingereza. Zilikuwepo Britz ambapo Wajerumani wanadondosha mabomu kwenye miji ya Uingereza, nayo ikadondosha mabomu kwenye miji ya Ujerumani kama Dresden na Munich. Na ikalipua mabwawa ya umeme kusababisha mafuriko ya Ruhr industrial region ili silaha zisitengenezwe.

Hitler alivamia nchi alizoona ni wanyonge. Hadi aliivamia USSR baada ya kuona performance yao mbovu kwenye vita na Finland. Uingereza ndio ilitangaza vita kwa Ujerumani, na ilikuwa ya kwanza bila woga kwa kujiamini. Isingetangaza vita wala isingepigana na Ujerumani.
 
uingereza aliwahi kumvamia nani akiwa peke yake?
Na ni nani aliwahi mvamia Uingereza akiwa peke yake?

Anyway, Falklands war mwaka 1982 Uingereza iliendesha melivita na ndege umbali wa kilomita 11,000 kwenda kupigana na Argentina.
unaongelea historia ya miaka ya 1900 huko sio?
Miaka ya 1900 hizo nchi nyingine si zilikuwepo? Na si zilikuwa na majeshi?

Hata tukirudi miaka ya 1700 bado hizo nchi zote zilikuwa na majeshi. Britain ilipigana na kina Napoleon, Russian Empire, France, Ottomans na ilikuwa kwenye alliances nyingi na vita mchanganyiko za wakati mmoja na sometimes adui wa leo ni rafiki wa kesho.

Kuwatishia Waingereza na vita ni sawa na kumtishia Masai kunywa maziwa.
 
Si kweli, bunge la uingereza walikaa vikao kujadili kupambana na ujerumani au waache , kwa maana hadi hapo Uingereza ilijua wazi haitoweza kupambana na ujerumani, ilikuwa mshike mshike bungeni, hawa wakisema hii vita hatuwezi wengine wakisema tupambane.

Haya masuala ya WWII ndio ilipelekea Chamberlain aka resign. ..

Haikuwa vyepesi hivyo, UK ilipambana kufa na kupona ..

Ujerumani ilipomnyong'onyeza UK ikaondoka kwa kufahamu itarudi baadae kummalizia, kipindi hiko UK imepigwa vibaya japo nakubali walikomaa piga nikupige.... Germans ndipo wakahamia kupambana kwa nguvu zote na wasovieti.
 
kuvamia kisiwa na ardhi tambarare ni sawa?
uingereza haiwezi kuvamiwa kirahisi kwa sababu ni kisiwa, na Urusi kuvamiwa na ukraine ni jambo la kawaida maana Urusi mara zote imekuwa ikivamiwa tokea upande huu wa ardhi ya Ukraine.....
Then mbona Uingereza huwa inatoka kwenye visiwa vyake inavamia hizo ardhi tambarare kupitia kwenye fukwe?

Kwani naval landing ya kwenye kisiwa na naval landing ya nchi iliyopo mainland ina tofauti gani? Wanajeshi wanaoenda kutua pwani ya kisiwa cha Unguja wanakumbana na kipi cha tofauti na wale wanaotua pwani ya bara pale Lindi au Mtwara?

Pote kuna mchanga, matumbawe, fukwe zenye kina kirefu na kifupi, wote wanatokea baharini ugumu ni uleule. Sasa mbona Britain always huwa inatoka visiwani inaenda kumpiga mtu kisha inarudi na meli?

Sasa kwa taarifa ni hivi, ni rahisi kuvamia kisiwa maana unakiwekea naval blockade kinakosa supplies. Ila ni vigumu kuivamia nchi kavu sababu ina njia nyingi za kupita, ndio sababu Japan ilipigwa na Marekani.
Na Uingereza ni ndogo kwa size haiifikii hata Tanzania ila inamudu kujilinda.

Tanzania ikipigana na Madagascar (assume wote tuna melivita na nyambizi) ni rahisi sisi kuweka naval blockade hata kwa sea mines tukasumbua meli za mizigo wafe njaa wakose na supplies, mafuta, spare parts, silaha, ammunition, vyakula. Ila wao wakizuia pwani yetu tuna options za kupitisha silaha Rwanda au Kenya au Uganda au Malawi au Congo au Msumbiji. Na hizo zote ni nchi huru ambazo hazingehusika na vita yetu.

Hakuna nchi iliwahi weka naval blockade kwa Britain wakati wako na disadvantage kijiografia.
kisiwa cha uingereza hakiwezi kuichukulia poa urusi kwa sababu hawajawahi kupigana......
btw uingereza haina uwezo mkubwa kijeshi, hata ingetokea akapigana na Ukraine atapigwa tena ukraine asingehitaji msaada kama anavyotegemea msaada leo!
Urusi na Uingereza huwa wanakutana kwenye alliances ambazo Urusi inapoteza wanajeshi wengi sana. Vita ya kwanza ya dunia Urusi ilipigwa na Ujerumani hadi ikakimbia vita mpaka mapinduzi yakafanyika. Walikula hasara kiuchumi na hawakuambulia kitu, hawakutimiza hata lengo moja.
Wakati Uingereza ilibaki na ikashinda.

Kwenye WW2 Urusi ikawa upande uleule wa Uingereza. Warusi wakafa wengi zaidi ya milioni 20 kuliko nchi nyingine wakati walikuwa front moja kwao. Waingereza hata pua ya Mjerumani haikuonekana kwenye ardhi yao. Walipigania North African theater hasa Misri na Tunisia, Mediterranean sea, Atlantic, mainland Europe kwenye Western front kuanzia Ufaransa, Holland, Belgium na Ujerumani kwenyewe.

Na sio Waingereza tu, hata Wafini hawawachukulii Warusi kama wazuri kimedani.
 
Nilichoandika ambacho si kweli ni nini mkuu. Si kweli kwamba Uingereza ndio ilitangaza vita dhidi ya Ujerumani?
Bila Ujerumani kuivamia Uingereza wala kuitishia. Kasome tena.

Chamberlain alijiuzuru sababu alikuwa na Appeasement Policy, ile mtoto wa jirani ni mwizi ila tumuonyeshe upendo tuyazungumze. Wakati Churchill alikuwa anaamini hakuna kucheka na mwizi. Hitler alipovamia Poland ikaonekana Appeasement ni upuuzi, Chamberlain akaachia ngazi na akapendekeza Churchill ndio ashike usukani wakati enzi za amani Churchill alionekana warmonger na bungeni alitolewa.

Ujerumani haikuondoka Uingereza eti itarejea. Iliondoka sababu uwezekano wa kuipiga Uingereza ulikuwa ni sifuri ilikuwa inapoteza ndege na meli bure, wakati Uingereza haina kitu in return endapo itatekwa. Ni visiwa hata kilimo hawana, mafuta hawana, population hawana, madini hawana yani ni hasara na ni wakorofi wako organized. Ikatafutwa nchi yenye kila kitu na ni ya kinyonge ni Urusi, ikavamiwa hiyo.

Ila Uingereza ikawafuata ingawa Hitler alitaka waache vita. Sasa unasemaje iliwekwa kiporo, wakati iliwadhibiti vitani Hitler akaleta mazungumzo tena bila sharti lolote.
 
Si kweli, Nazi Germany haikuiona Soviet kama vibonde, Urusi ndio ilipelekea Hitler na wenzake kujimaliza na familia zao baada ya kusikia msoviet akigonga hodi kutoka eastern front na si Britain wala USA....

WW2 UK haikuwa na uwezo kijeshi kama USSR acheni ushabiki na history ambazo ni biased... UK alipigana akashukuru Mungu Germany ameondoka, lakini USSR akiwa peke yake eastern front aliwasukuma askari wa Germany hadi Berlin na ndio walikuwa wa kwanza kuingia Berlin, Allies wasingeshinda hivyo vita pasipo msoviet...

Britain walikuwa urojo tu mbele ya USSR tuacheni story za kwenye kahawa....
 
Anyway, Falklands war mwaka 1982 Uingereza iliendesha melivita na ndege umbali wa kilomita 11,000 kwenda kupigana na Argentina.
Nina swali kwanini 1982 hawakuendesha melivita mpaka kisiwa cha Hong-Kong kwenda kupigana na China ?
 
Kumekucha
 
Lakini kumbuka, nguvu ya Russia ya wakati wa ww2 hauwezi linganisha na nguvu iiliyonayo leo, sielewi ni mazingira ama utawala!

Iweje Ukraine nchi iliyokuwa ni mkoa wake ihangaike nayo kwa zaidi ya miaka miwili, je ikipambana na Uingereza sasa, jino kwa jino, bado utaitabiria ushindi Russia?
 
Nina swali kwanini 1982 hawakuendesha melivita mpaka kisiwa cha Hong-Kong kwenda kupigana na China ?
Kwa sababu Hong Kong sio sehemu ya Uingereza. Wala China haikuishambulia Uingereza. Wala raia wa Hong Kong hawajawahi omba rescue kutoka kwa Uingereza.

Soma kwanini Uingereza iliingia Falklands.
 
Vita ya chupa bar umetumia icbm
We jamaa heshima Yako kubwa kwangu ktk maswala hayo
Ningependa kujua kwanini wahindi hawaendi jwtz
 
Sio kwamba wote ni mashoga na hawapendi kazi ngumu ni sex tu
 
Mrusi mtu m badi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…