Wanajeshi wa Uingereza wanaacha kazi ya jeshi licha ya malipo bora

1734984961922.png

Hii ndio mishahara ya officers... kwa viwango vya maisha ya UK ni vidogo
 
Si kweli, Nazi Germany haikuiona Soviet kama vibonde, Urusi ndio ilipelekea Hitler na wenzake kujimaliza na familia zao baada ya kusikia msoviet akigonga hodi kutoka eastern front na si Britain wala USA....
USA wala Britain hazikutangaziwa vita na Nazi Germany. Elewa mambo kijana.

Nazi Germany ilitangaza vita dhidi ya Poland na Ufaransa, zikafuata nyingine baadae kina Holland na Sweden na Urusi uko. Uingereza ndio ilitangaza vita dhidi ya Ujerumani. Pia baadae miaka kama mitatu US ikatangaza vita dhidi ya Marekani.

UK na US zilipigana na Ujerumani kwa msaada, kuwasaidia wanyonge wasizidiwe. Hakukuwa na sababu ya msingi ya US kuingia vitani, hakukuwa na sababu ya msingi ya Britain kuingia vitani ila tu kupinga Fascism.

Urusi ilistahili ipigane na Ujerumani sababu ilivamiwa, sasa ulitaka isipigane ipiganiwe na nani baba yake au? Soviets walikuwa vibonde waliteswa na kanchi kamoja ka Finland, Ujerumani ikawaona hamna kitu.
WW2 UK haikuwa na uwezo kijeshi kama USSR acheni ushabiki na history ambazo ni biased... UK alipigana akashukuru Mungu Germany ameondoka
Hakuna cha kushukuru Mungu, Mungu hakuwa vitani. Ujerumani ilipigwa na Uingereza. Get your facts right.

Ujerumani ilienda na ndege zaidi ya 2,500 wakati Uingereza merely ilikuwa na ndege 700 ila matumizi ya akili, mipango, training na valor ya Waingereza (ambavyo nyinyi Warusi huwa hamtaki bali kutumia nguvu nyingi na akili kidogo) ndio uliwafanya ku-inflict casualties nyingi kwa Germany Airforce.

Bombers na fighters zilikuwa zinatoka Ujerumani direct hadi Uingereza kwa miezi kadhaa mfurulizo ila zilipigwa. Warusi wana linchi likubwa ndege za Ujerumani zinakuja zinatua njiani kwanza mara Poland mara nchi gani. Na bado Warusi wakapigwa wakachaa hadi wakafa milioni 20.
lakini USSR akiwa peke yake eastern front aliwasukuma askari wa Germany hadi Berlin na ndio walikuwa wa kwanza kuingia Berlin, Allies wasingeshinda hivyo vita pasipo msoviet...
Ulitaka nani ashirikiane na Soviet Union kule Eastern Front?

Wasovieti walikuwa washamba tu. Wakati Ujerumani inavamiwa Poland mwaka 1939, wao wakaisadia kuvamia Finland kwenye Winter war mwaka huohuo na wakaonekana maboya wamepata casualties nyingi dhidi ya kanchi kadogo.

Mwaka huohuo 1939 Soviets waliivamia Poland wakishirikiana na Ujerumani, wakaigawana nusu. Wakafanya na Katyn massacre kwa kuuwa wafungwa wa kivita 22,000 wa Poland (ni kawaida ya Soviets, they were human scums).

Mwaka huohuo 1939 Soviets na Nazi Germany waliandika mkataba wa kusaidiana kijeshi na kivita. Ulisainiwa na mawaziri wao wa mambo ya nje Molotov-Ribbentrop Pact
1024px-sdelka-veka.jpg

Hawa hapa majangiri Viacheslav Molotov (kushoto) na Joachim von Ribbentrop (kulia) siku wamesaini mkataba wasaidiane kijeshi.

Baadae kutokana na kwamba wachawi hawaaminiani, Ujerumani kwa sababu zilezile ilizoona wengine ni mafala ikagundua Warusi ni mabwege zaidi. Miaka mitatu baadae ikaamua ivamie mabwege.

Sasa unamlaumu nani ambaye angeshirikiana na USSR kule Eastern front. Unashirikiana vipi na fedhuri na mwehu?
Britain walikuwa urojo tu mbele ya USSR tuacheni story za kwenye kahawa....
USSR walisaidiwa kupunguziwa mzigo wa kupigana Western front ili Ujerumani igawane war resources pande mbili izidiwe. UK na US zingeweza kuwaacha Wajerumani wawapige Wasovieti na nchi yao igeuzwe mashamba ya ngano (ndicho Hitler alitaka baada ya kuona UK ni wagumu alafu kilimo chao hata Morogoro ikiamua kulima inawazidi, alafu USSR washamba tu na linchi lina kila kitu).

Marekani ilitoa msaada huu hapa kwa Urusi, sababu kama Urusi ingetekwa basi Marekani ingewajibika kuikomboa. Warusi kwa training za hovyo na kutojali uhai wakawa wanakufakufa tu vitani
20241223_231749.jpg
 
Lakini kumbuka, nguvu ya Russia ya wakati wa ww2 hauwezi linganisha na nguvu iiliyonayo leo, sielewi ni mazingira ama utawala!

Iweje Ukraine nchi iliyokuwa ni mkoa wake ihangaike nayo kwa zaidi ya miaka miwili, je ikipambana na Uingereza sasa, jino kwa jino, bado utaitabiria ushindi Russia?
Elewa kwanza dhamira ya Russia kijeshi hapo Ukraine, Russia haikutaka kuotawala Ukraine, lakini wamesema wazi operation ni kuimaliza nguvu za kijeshi Ukraine na hapo NATO wakiongozwa na US wanatoa msaada wa hali na mali kuanzia makombora, pesa, washauri wa kivita n.k, ndipo ujue Russia sio wa kuwabeza...
 
Mkuu T14 Armata hua unaizungumzia Russia kiudogo sana, sijajua sababu lakini naona una chuki binafsi na hawa watu.

Ukiangalia leo idadi ya sanctions ambazo Russia amewekewa na Collective west ni nyingi, mfano kwa hadi February mwaka huu EU wameweka jumla ya sanctions 200 kwa taasisi na watu binafsi wanaoweza kuisaidia Russia kupata siraha. USA yenyewe imeweka sanctions mpya 500.

Lakini Russia ameendelea kuchukua maeneo zaidi kila siku, mathalan kabla ya mwaka 2022 Russia alikua amechukua maeneo ya Ukraine jumla ya 42,000 sqkm ambayo ni Crimea na baadhi ya maeneo ya Donetsk na Luhansk.
Baada ya full scale invasion Russia amechukua 119,000 sqkm ambapo ukichukua na ile ya mwanzo ni jumla ya 27% ya ardhi ya Ukraine ipo mikononi mwa Russia.

Pamoja na sanctions zote ikiwemo kuzuia jumla ya dollars billions 300 za Russia katika mabenki ya Ulaya na America ila uchumi wa Russia umeendelea kukua zaidi, mwaka jana pekee uchumi wa Russia umekua kwa 3.6% ambayo hii ni zaidi ya America ambayo uchumi umekua kwa 2.5% au Ulaya ambayo imekua kwa 0.4%.

Nakushauri ndugu yangu, Russia ni lidude likubwa sana la kutisha linaoangamiza kila kitu kinachokuja mbele yake, ipende Russia au usiichukie sababu ukiendelea kuichukia utakuja kuumwa presha ya bure kabisa tukupoteze mazima
 
USA wala Britain hazikutangaziwa vita na Nazi Germany. Elewa mambo kijana.

Nazi Germany ilitangaza vita dhidi ya Poland na Ufaransa, zikafuata nyingine baadae kina Holland na Sweden na Urusi uko. Uingereza ndio ilitangaza vita dhidi ya Ujerumani. Pia baadae miaka kama mitatu US ikatangaza vita dhidi ya Marekani.

UK na US zilipigana na Ujerumani kwa msaada, kuwasaidia wanyonge wasizidiwe. Hakukuwa na sababu ya msingi ya US kuingia vitani, hakukuwa na sababu ya msingi ya Britain kuingia vitani ila tu kupinga Fascism.

Urusi ilistahili ipigane na Ujerumani sababu ilivamiwa, sasa ulitaka isipigane ipiganiwe na nani baba yake au? Soviets walikuwa vibonde waliteswa na kanchi kamoja ka Finland, Ujerumani ikawaona hamna kitu.

Hakuna cha kushukuru Mungu, Mungu hakuwa vitani. Ujerumani ilipigwa na Uingereza. Get your facts right.

Ujerumani ilienda na ndege zaidi ya 2,500 wakati Uingereza merely ilikuwa na ndege 700 ila matumizi ya akili, mipango, training na valor ya Waingereza (ambavyo nyinyi Warusi huwa hamtaki bali kutumia nguvu nyingi na akili kidogo) ndio uliwafanya ku-inflict casualties nyingi kwa Germany Airforce.

Bombers na fighters zilikuwa zinatoka Ujerumani direct hadi Uingereza kwa miezi kadhaa mfurulizo ila zilipigwa. Warusi wana linchi likubwa ndege za Ujerumani zinakuja zinatua njiani kwanza mara Poland mara nchi gani. Na bado Warusi wakapigwa wakachaa hadi wakafa milioni 20.

Ulitaka nani ashirikiane na Soviet Union kule Eastern Front?

Wasovieti walikuwa washamba tu. Wakati Ujerumani inavamiwa Poland mwaka 1939, wao wakaisadia kuvamia Finland kwenye Winter war mwaka huohuo na wakaonekana maboya wamepata casualties nyingi dhidi ya kanchi kadogo.

Mwaka huohuo 1939 Soviets waliivamia Poland wakishirikiana na Ujerumani, wakaigawana nusu. Wakafanya na Katyn massacre kwa kuuwa wafungwa wa kivita 22,000 wa Poland (ni kawaida ya Soviets, they were human scums).

Mwaka huohuo 1939 Soviets na Nazi Germany waliandika mkataba wa kusaidiana kijeshi na kivita. Ulisainiwa na mawaziri wao wa mambo ya nje Molotov-Ribbentrop PactView attachment 3183574
Hawa hapa majangiri Viacheslav Molotov (kushoto) na Joachim von Ribbentrop (kulia) siku wamesaini mkataba wasaidiane kijeshi.

Baadae kutokana na kwamba wachawi hawaaminiani, Ujerumani kwa sababu zilezile ilizoona wengine ni mafala ikagundua Warusi ni mabwege zaidi. Miaka mitatu baadae ikaamua ivamie mabwege.

Sasa unamlaumu nani ambaye angeshirikiana na USSR kule Eastern front. Unashirikiana vipi na fedhuri na mwehu?

USSR walisaidiwa kupunguziwa mzigo wa kupigana Western front ili Ujerumani igawane war resources pande mbili izidiwe. UK na US zingeweza kuwaacha Wajerumani wawapige Wasovieti na nchi yao igeuzwe mashamba ya ngano (ndicho Hitler alitaka baada ya kuona UK ni wagumu alafu kilimo chao hata Morogoro ikiamua kulima inawazidi, alafu USSR washamba tu na linchi lina kila kitu).

Marekani ilitoa msaada huu hapa kwa Urusi, sababu kama Urusi ingetekwa basi Marekani ingewajibika kuikomboa. Warusi kwa training za hovyo na kutojali uhai wakawa wanakufakufa tu vitaniView attachment 3183587
Umeandika matango tu na nimeona vichache nikujibu kwa sababu unaongozwa na mahaba....

Kwanza tambua lengo la Soviet kujiunga na Hitler, ndipo ujue intel ya soviet haikuwa ya kitoto, Soviet waliona mapema uwezo wa kijeshi wa Germany haukuwa wa kubezwa, mapema sana akawaomba Britain, US, France waungane kumkabili Germany, wakajifanya wajuajj kwamba wana uwezo kijeshi huku wakimtenga Soviet kisa masuala ya ujamaa na blah blah blah kibao....

Baada ya kuteremshiwa kipondo heavy na Germany ndipo akili ikawakaa sawa na kukumbuka Soviet alisema nini ... Soviet aliona pekee itakuwa ngumu kumkabili Germany akaona kama huwezi shindana nae basi ungana nae...

Battle of Dunkirk hao wafaransa na British walitandikwa askari zaidi ya 338K walitaka kumalizwa pale Dunkirk wamezungukwa na askari wa Hitler, hivi unaelewa kwanza askari laki tatu elfu thelathini na nane ni wengi kiasi gani? Na wame surrender wamezungukwa.... Operation dynamo ndipo hadi raia wenye mitumbwi wanapeleka kuokoa askari hao, ndio maana wakaita miracle of Dunkirk, unaweza kuelewa jeshi la Germany lilikuwa na nguvu kiasi gani kuzunguka hao askari wa France na Britain ...

Acheni ushabiki wa kipuuzi na mahaba....

Nazi Germany walikuwa wanatisha, lakini walikaa kwa Soviet tandikwa hadi kwao....

Ndio maana kutoka Magharibi walijipanga US, France na Britain, huku eastern front chinja chinja wazee wa kazi Soviet wakimmaliza Germany hadi Berlin....

Unaisifia ooooh Britain sijui blah blah blah... Walipigwa hadi askari wao wakaokolewa na mitumbwi ya wananchi wazalendo, tandikwa kweli kweli choka mbaya *****.... Hadi wanaomba msaada....

Kiherehere kikawaisha, na hapo wakakumbuka waSoviet, tena Soviets waliwatahadharisha miaka nyuma, wakakumbuka Sovieta waliwaambia nini kuhusu kuungana kummaliza Germany....

Ndipo wakaanza kushirikiana na Soviet kwa aibu, huku wamechelewa, wamepoteza askari wengi na wengi kukamatwa, wangemsikiliza Soviet hayo yote yasingetokea...

Kijana kasome historia ...
 
Mkuu T14 Armata hua unaizungumzia Russia kiudogo sana, sijajua sababu lakini naona una chuki binafsi na hawa watu.

Ukiangalia leo idadi ya sanctions ambazo Russia amewekewa na Collective west ni nyingi, mfano kwa hadi February mwaka huu EU wameweka jumla ya sanctions 200 kwa taasisi na watu binafsi wanaoweza kuisaidia Russia kupata siraha. USA yenyewe imeweka sanctions mpya 500.

Lakini Russia ameendelea kuchukua maeneo zaidi kila siku, mathalan kabla ya mwaka 2022 Russia alikua amechukua maeneo ya Ukraine jumla ya 42,000 sqkm ambayo ni Crimea na baadhi ya maeneo ya Donetsk na Luhansk.
Baada ya full scale invasion Russia amechukua 119,000 sqkm ambapo ukichukua na ile ya mwanzo ni jumla ya 27% ya ardhi ya Ukraine ipo mikononi mwa Russia.

Pamoja na sanctions zote ikiwemo kuzuia jumla ya dollars billions 300 za Russia katika mabenki ya Ulaya na America ila uchumi wa Russia umeendelea kukua zaidi, mwaka jana pekee uchumi wa Russia umekua kwa 3.6% ambayo hii ni zaidi ya America ambayo uchumi umekua kwa 2.5% au Ulaya ambayo imekua kwa 0.4%.

Nakushauri ndugu yangu, Russia ni lidude likubwa sana la kutisha linaoangamiza kila kitu kinachokuja mbele yake, ipende Russia au usiichukie sababu ukiendelea kuichukia utakuja kuumwa presha ya bure kabisa tukupoteze mazima
Unafikiri hawaelewi ukweli, wanaelewa sana kinachoendelea..

Ukraine inatandikwa hadi huruma huku maeneo yakikamatwa kila siku... NATO na misaada haizuii Russia kuchukua maeneo...

Wanaofahamu ukweli wanaelewa hao ndio wababe wa kivita duniani.

US kuivamia Iraq walialikana karibu ulimwengu mzima... Russia anapambana na NATO...
 
Vita ya chupa bar umetumia icbm
We jamaa heshima Yako kubwa kwangu ktk maswala hayo
Ningependa kujua kwanini wahindi hawaendi jwtz
Sababu za Wahindi kutojiunga na JWTZ au KDF (jeshi la Kenya) ni zilezile.

Wao ni watazama fursa, wakati wabongo wengi walikuwa watazama sifa. Wakati tunapata uhuru kati ya kada zilipelekwa zaidi nje kusoma ni jeshi maana hatukuwa na vyuo vya kijeshi wala uzoefu. Maofisa wetu walienda UK, Urusi China, etc. Na walienda kusoma kozi ngumu za gharama kubwa kulipiwa na mwanafunzi. Wakafaulu wakiwa wataalamu wa mitambo, marubani, wasomi wa political science, wenye exposure nje.

Kwa sababu Wahindi hawawezi kuwa wazalendo wa nchi ya Kiafrika hivyo wakawa wanasomeshwa kwa gharama za serikali ila wanawaza wapate kazi nzuri. Na majeshi hayakulipa vizuri wanaita uzalendo, wakawa wanaacha kazi wanaenda mtaani na elimu zao wanalipwa vizuri zaidi au wanahama nchi.

Vilevile Wahindi wasingepanda sana vyeo, hawaonekani wazawa. Kwahiyo ikakosekana maana ya wao kupenda vyombo vya usalama na ulinzi.
 
Mkuu T14 Armata hua unaizungumzia Russia kiudogo sana, sijajua sababu lakini naona una chuki binafsi na hawa watu.

Ukiangalia leo idadi ya sanctions ambazo Russia amewekewa na Collective west ni nyingi, mfano kwa hadi February mwaka huu EU wameweka jumla ya sanctions 200 kwa taasisi na watu binafsi wanaoweza kuisaidia Russia kupata siraha. USA yenyewe imeweka sanctions mpya 500.

Lakini Russia ameendelea kuchukua maeneo zaidi kila siku, mathalan kabla ya mwaka 2022 Russia alikua amechukua maeneo ya Ukraine jumla ya 42,000 sqkm ambayo ni Crimea na baadhi ya maeneo ya Donetsk na Luhansk.
Baada ya full scale invasion Russia amechukua 119,000 sqkm ambapo ukichukua na ile ya mwanzo ni jumla ya 27% ya ardhi ya Ukraine ipo mikononi mwa Russia.

Pamoja na sanctions zote ikiwemo kuzuia jumla ya dollars billions 300 za Russia katika mabenki ya Ulaya na America ila uchumi wa Russia umeendelea kukua zaidi, mwaka jana pekee uchumi wa Russia umekua kwa 3.6% ambayo hii ni zaidi ya America ambayo uchumi umekua kwa 2.5% au Ulaya ambayo imekua kwa 0.4%.

Nakushauri ndugu yangu, Russia ni lidude likubwa sana la kutisha linaoangamiza kila kitu kinachokuja mbele yake, ipende Russia au usiichukie sababu ukiendelea kuichukia utakuja kuumwa presha ya bure kabisa tukupoteze mazima
Ukraine iliyovamiwa na Urusi mwaka 2022 ingeweza kuvamiwa na Misri ingepigwa.
Its very strange Urusi iko pua na mdomo inapakana na Ukraine mamia ya kilomita mipaka iko wazi, hakuna madaraja, kuna nyika tu wala sio maji alafu inatumia nguvu nyingi sana.
Ndio maana nimewapa mfano wa Falklands war, Uingereza ilitembeza meli na ndege kilomita 11,000 kupigana na Argentina. Ingekuwa Urusi hii ingeweza?

Urusi hii hapa ikihitajika ikapigane na Afrika Kusini, itashindwa. Haina logistics za kupigana vita mbali.

Ukraine haistahili kuwa tishio la Urusi. Ni utaratibu wa Urusi kusumbuliwa na vinchi hata havina majina kwenye vita, sio sifa ya superpower hii. Hata vita za Chechen majeshi ya Jamhuri ya Urusi yalisumbuliwa na vikosi vya waasi.

Sio kwamba naidogosha Urusi, nyinyi ndio mnaikuza kupita uwezo halisi.
 
Uingereza hawalipi vizuri wanajeshi hasa sailors. Report yako inasema "malipo yameongezwa" ila haitokaa itokee malipo ya civilian market yawe juu ya malipo ya defence contractors. Kwa nchi nyingine ni hivyo ila kwa Uingereza ni vibaya zaidi.

Mfano ili mtu awe Royal Navy submarine captain anatakiwa awe na akili sana, experience kubwa, uwezo binafsi wa hali ya juu, ana risk kubwa ya kuachishwa kazi, hana option ya kuhama kazi sababu submarines zinamilikiwa na serikali na hawezi hama jeshi kutoka Uingereza kwenda labda Spain. Na bado submarines ni chache na zina kazi ngumu.

Wakati mtu mwenye uwezo mdogo nusu ya submarine captain anaweza ajiriwa na shirika la ndege la Uingereza, British Airways akalipwa mshahara uleule, kazi nyepesi kabisa, uzoefu wa kawaida, options za kuacha kwenda mashirika mengine zipo nyingi, risks za kuachishwa kazi ni chache, kuna uhuru wa kufanya kazi, na ndege zipo nyingi shirika hilo au mashirika mengine. Na kazi ina bonus.

Popote pale mtu mwenye uwezo mkubwa anaweza kupata kazi nzuri kwenye civilian market kuliko jeshini. Ford, Tesla, BYD, Volkwagen wanatengeneza mamilioni ya magari models mpya kila mwaka na kila miaka kama mitano magari yanaharibika wateja wananunua mengine. Wakati mfano kampuni ya Nexter ya Ufaransa tangu iunde Leclerk main battle tank mwaka 1992 mpaka leo haijawahi unda type nyingine na wateja ni nchi kama tatu tu, na vifaru vyote vilivyoundwa tangu mwaka huo bado vipo. Imagine design engineer wa hiyo kampuni ana miaka kadhaa hajawahi lipwa bonus wakati waliopo Volkwagen wanafyatua magari tu.

Boeing B-52 Stratofortless zimeanza kuundwa tangu 1952 na ya mwisho iliundwa 1962 ila mpaka leo zipo zinafanyiwa upgrade tu. Wakati Boeing za abiria zinauzwa maelfu kila mwaka na kila muongo wanatoa products kadhaa mpya kwenye assembly line na kila miaka kama 20 ndege inaacha kutumika. Hivyo kimauzo huwezi tegemea engineer wa military market alipwe sawa na civilian market. Same thing na jeshini.

Hata kwenye software, engineers waliounda NATO Link 16 walimaliza 1970s, Link 22 ni ya 1980s na mpaka leo ndio zinatumika kwenye communications zote za ndege za NATO. Wakati kwenye civilian market consumers huwa wanachoka kitu bila sababu za msingi. Windows 11 na 10 zina tofauti ndogo sana, ila watu wamelipwa kutoa Windows 11. Android versions kila mwaka, iOS kila mwaka. 3G, 4G, 5G na 6G iko njiani.

Hela zinamwagwa kwenye research na kuna malipo, marupurupu, zawadi, recognition na sense of accomplishment. Kwenye soko huru its likely watu wenye uwezo mkubwa wasiende jeshini.
Kenyan Airforce miaka ya 70s ndio ilikuwa inapeleka marubani kusoma bure ili waendeshe ndegevita, matokeo yake wakirudi wanaenda civilian market kuendesha East African Airways, last week Rais wa Nigeria amesaini sheria maofisa wa jeshi lazima watumikie miaka si chini ya 15. Walikuwa na tabia ya kusomeshwa bure wanapata ujuzi unaolipa vizuri mtaani kisha wanafanya kazi miaka michache jeshini na kuacha kazi. Mnahisi kwanini Wahindi waliacha kujiunga na JWTZ?
Shukrani sana Mkuu kwa madini adimu na chakula Bora Cha ubongo.

Hii ndiyo raha ya jamii forum.

Mkuu tuletee madini kuhusu nguvu za Paul Kagame kijeshi!!

Hivi ni kweli akilianzisha na bongo, TZ itakuwa kama Simba anapocheza na yanga???
 
Kwanza tambua lengo la Soviet kujiunga na Hitler, ndipo ujue intel ya soviet haikuwa ya kitoto, Soviet waliona mapema uwezo wa kijeshi wa Germany haukuwa wa kubezwa, mapema sana akawaomba Britain, US, France waungane kumkabili Germany, wakajifanya wajuajj kwamba wana uwezo kijeshi huku wakimtenga Soviet kisa masuala ya ujamaa na blah blah blah kibao....
Vizuri umetambua kwamba Soviet Union waligeuzwa mafala kuungana na Nazi Germany wenye nia ovu. Sasa ulikuwa unalia nini kwamba USSR ilipigana yenyewe Eastern Front?

USSR iliivamia Poland na Finland kwa kukubaliana na Ujerumani, nani angeungana na USSR pale miaka mitatu baadae ambapo Ujerumani ilivamia?
Baada ya kuteremshiwa kipondo heavy na Germany ndipo akili ikawakaa sawa na kukumbuka Soviet alisema nini ... Soviet aliona pekee itakuwa ngumu kumkabili Germany akaona kama huwezi shindana nae basi ungana nae...
Akili ilimkaa sawa Mjerumani aliposhindwa Battle of Britain, akaanzisha Operation Barbarossa kwa Wasovieti alioona ni wepesi. Wajinga wasio na heshima aliotapeli wamuunge mkono.

Kwa akili yako unaona nani alikuwa na akili zaidi, Uingereza iligoma kuungana na Ujerumani. Urusi ikaungana nao na miaka mitatu baadae ikavamiwa. Hapo bwege nani hata tukiita mtoto wa class one😂

Wasovieti waliokufa na kujeruhiwa vita ya pili ya dunia ni watu milioni 27. Wakati Waingereza waliokufa na kujeruhiwa hawafiki milioni 1.

Nani hapo alipewa kipondo cha mbwa koko?
Battle of Dunkirk hao wafaransa na British walitandikwa askari zaidi ya 338K walitaka kumalizwa pale Dunkirk wamezungukwa na askari wa Hitler, hivi unaelewa kwanza askari laki tatu elfu thelathini na nane ni wengi kiasi gani? Na wame surrender wamezungukwa.... Operation dynamo ndipo hadi raia wenye mitumbwi wanapeleka kuokoa askari hao, ndio maana wakaita miracle of Dunkirk, unaweza kuelewa jeshi la Germany lilikuwa na nguvu kiasi gani kuzunguka hao askari wa France na Britain ...
Aaah kumbe raia wa Uingereza ndio walienda kuokoa wanajeshi wao. Sasa kuna shida gani? Na hawakufa wala kutekwa.

Dunkirk ilikuwa ni move, zilikuwepo moves nyingi kwenye fronts zote mbili. Soviets walipoteza wapiganaji zaidi ya milioni moja kuilinda Stalingrad, na wakapoteza wanajeshi zaidi ya laki tatu kwenye pale Kursk.
Nani alizuia raia wao wasiwaokoe?
Acheni ushabiki wa kipuuzi na mahaba....

Nazi Germany walikuwa wanatisha, lakini walikaa kwa Soviet tandikwa hadi kwao....
Soviets waliungana na Nazi Germany kuvamia. Kilichotokea baada ya wao kuvamiwa ni desperate move in desperate times. Hawana ushujaa wowote, they were fooled by the Nazis, they were working their asses for Hitler. A fool ain't a champion.
Ndio maana kutoka Magharibi walijipanga US, France na Britain, huku eastern front chinja chinja wazee wa kazi Soviet wakimmaliza Germany hadi Berlin....
Marekani haikuvamiwa na Ujerumani. Ilivamiwa na Japan na ndio ilitakiwa ipigane nayo tu. Ila ikagawa misaada kwa Soviet Union. Ningependa ubishe useme haikutoa misaada.
Na pia ikatoa majeshi yake ipigane Ulaya, huku inapigana Pacific kuzikomboa Ufilipino, Korea, China, Burma, New Guinea dhidi ya Japanese occupation.

Uingereza vilevile haikuvamiwa na Ujerumanu. Ilitangaza yenyewe kuivamia Ujerumani baada ya Hitler kuanzisha vita dhidi ya Poland.

Meanwhile, Urusi ilishirikiana na Ujerumani kuipiga Poland wakagawana. Ikaivamia Finland pia. Baadae jinsi ilivyokuwa bwege ikavamiwa na rafiki wa mashaka, fools!

Bila msaada wa Marekani Urusi sahivi ingekuwa inaongea Kijerumani na inatoa malighafi kwa viwanda vya Ujerumani.
Unaisifia ooooh Britain sijui blah blah blah... Walipigwa hadi askari wao wakaokolewa na mitumbwi ya wananchi wazalendo, tandikwa kweli kweli choka mbaya *****.... Hadi wanaomba msaada....
Hao wazalendo si nchi yao ilikuwa vitani? Kumbe raia wa Uingereza walikuwa na uwezo kuokoa wanajeshi wao kwenye mapigano. Sasa mbona kwenye huu uzi mnadai Uingereza watu wanakimbia jeshi, hamuoni hata raia waliweza kupambana na Nazi Germany iliyoua Wasovieti milioni 27. Hamuogopi?
Kiherehere kikawaisha, na hapo wakakumbuka waSoviet, tena Soviets waliwatahadharisha miaka nyuma, wakakumbuka Sovieta waliwaambia nini kuhusu kuungana kummaliza Germany....
Wasovieti walikuwa walamba viatu wa Wajerumani kabla hawajageukana.
Unaandika maneno ya khanga na kijiweni na huna factual data yoyote.

Eti "Sovieti waliwambia nini kuhusu Ujerumani..."😂
Sasa kama Soviets waliwajua sana Wajerumani ilikuwaje wao wakauwawa 27,000,000 alafu Waingereza wasiowajua Germans wakafa 800,000?
Ndipo wakaanza kushirikiana na Soviet kwa aibu, huku wamechelewa, wamepoteza askari wengi na wengi kukamatwa, wangemsikiliza Soviet hayo yote yasingetokea...

Kijana kasome historia ...
Ebu elezea Sovieti walipoteza wanajeshi wangapi na Uingereza wangapi.
Usiandike kama unakunywa wanzuki, andika kwa namba, data, facts, toa picha, link, mikataba, etc.

Alafu Uingereza haikushirikiana na Soviets, ilisaidia wasiojiweza ili wapigane wasizidiwe nguvu, hata US ilifanya hivyo. Bakhresa anakupa bure chakula usife njaa wewe unadai "ameshirikiana na mimi kwenye kula" badala ya useme amenisaidia. Get your facts right.
 
Kwa sababu Hong Kong sio sehemu ya Uingereza. Wala China haikuishambulia Uingereza. Wala raia wa Hong Kong hawajawahi omba rescue kutoka kwa Uingereza.

Soma kwanini Uingereza iliingia Falklands.
Uingereza ilitaka kuendeleza utawala wake Hong-Kong guess what Deng alichomuambia Thatcher

Kwani Falklands ni sehemu ya Uingereza ?

Tuje pia 2019 vijana wa Hong-Kong walikuwa wakipeperusha bendera za makoloni ya Uingereza kuomba support ya Uingereza dhidi ya Beijing
 
Umesema "ilitaka".

Ilitaka kivipi, bunge au Waziri Mkuu gani alitaka au Monarchy gani alitaka. Unajua Uingereza tawala zake zote zilikuwa na decree na claims zimeandikwa. Ni decree gani ilitolewa ya kuitaka Hong Kong miaka hiyo.

Suala la Falklands kuwa au kutokuwa sehemu ya Uingereza ni mgogoro.
Argentina inayoidai Falklands haina hata 2% ya population ya raia pale, last time kura za maoni raia waliamua ama wawe huru, au sehemu ya UK, au Argentina.

99.8% waliamua kuwa sehemu ya UK.

Na hiyo 2019 aliyekwambia Uingereza wanatawala nchi endapo vijana wake watapeperusha bendera yake mtaani nani. Kwamba kisa walokole uchwara wanapeperusha bendera ya Israel, basi Israel ije itawale Tanzania?
 
Vizuri umetambua kwamba Soviet Union waligeuzwa mafala kuungana na Nazi Germany wenye nia ovu. Sasa ulikuwa unalia nini kwamba USSR ilipigana yenyewe Eastern Front?

USSR iliivamia Poland na Finland kwa kukubaliana na Ujerumani, nani angeungana na USSR pale miaka mitatu baadae ambapo Ujerumani ilivamia?

Akili ilimkaa sawa Mjeeumani aliposhindwa Battle of Britain, akaanzisha Operation Barbarossa kwa Wasovieti alioona ni wepesi. Wajinga wasio na heshima aliotapeli wamuunge mkono.

Kwa akili yako unaona nani alikuwa na akili zaidi, Uingereza iligoma kuungana na Ujerumani. Urusi ikaungana nao na miaka mitatu baadae ikavamiwa. Hapo bwege nani hata tukiita mtoto wa class one😂

Wasovieti waliokufa na kujeruhiwa vita ya pili ya dunia ni watu milioni 27. Wakati Waingereza waliokufa na kujeruhiwa hawafiki milioni 1.

Nani hapo alipewa kipondo cha mbwa koko?

Aaah kumbe raia wa Uingereza ndio walienda kuokoa wanajeshi wao. Sasa kuna shida gani? Na hawakufa wala kutekwa.

Dunkirk ilikuwa ni move, zilikuwepo moves nyingi kwenye fronts zote mbili. Soviets walipoteza wapiganaji zaidi ya milioni moja kuilinda Stalingrad, na wakapoteza wanajeshi zaidi ya laki tatu kwenye pale Kursk.
Nani alizuia raia wao wasiwaokoe?

Soviets waliungana na Nazi Germany kuvamia. Kilichotokea baada ya wao kuvamiwa ni desperate move in desperate times. Hawana ushujaa wowote, they were fooled by the Nazis, they were working their asses for Hitler. A fool ain't a champion.

Marekani haikuvamiwa na Ujerumani. Ilivamiwa na Japan na ndio ilitakiwa ipigane nayo tu. Ila ikagawa misaada kwa Soviet Union. Ningependa ubishe useme haikutoa misaada.
Na pia ikatoa majeshi yake ipigane Ulaya, huku inapigana Pacific kuzikomboa Ufilipino, Korea, China, Burma, New Guinea dhidi ya Japanese occupation.

Uingereza vilevile haikuvamiwa na Ujerumanu. Ilitangaza yenyewe kuivamia Ujerumani baada ya Hitler kuanzisha vita dhidi ya Poland.

Meanwhile, Urusi ilishirikiana na Ujerumani kuipiga Poland wakagawana. Ikaivamia Finland pia. Baadae jinsi ilivyokuwa bwege ikavamiwa na rafiki wa mashaka, fools!

Bila msaada wa Marekani Urusi sahivi ingekuwa inaongea Kijerumani na inatoa malighafi kwa viwanda vya Ujerumani.

Hao wazalendo si nchi yao ilikuwa vitani? Kumbe raia wa Uingereza walikuwa na uwezo kuokoa wanajeshi wao kwenye mapigano. Sasa mbona kwenye huu uzi mnadai Uingereza watu wanakimbia jeshi, hamuoni hata raia waliweza kupambana na Nazi Germany iliyoua Wasovieti milioni 27. Hamuogopi?

Wasovieti walikuwa walamba viatu wa Wajerumani kabla hawajageukana.
Unaandika maneno ya khanga na kijiweni na huna factual data yoyote.

Eti "Sovieti waliwambia nini kuhusu Ujerumani..."😂
Sasa kama Soviets waliwajua sana Wajerumani ilikuwaje wao wakauwawa milioni 27,000,000 alafu Waingereza wasiowajua Germans wakafa 800,000?

Ebu elezea Sovieti walipoteza wanajeshi wangapi na Uingereza wangapi.
Usiandike kama unakunywa wanzuki, andika kwa namba, data, facts, toa picha, link, mikataba, etc.

Alafu Uingereza haikushirikiana na Soviets, ilisaidia wasiojiweza ili wapigane wasizidiwe nguvu, hata US ilifanya hivyo. Bakhresa anakupa bure chakula usife njaa wewe unadai "ameshirikiana na mimi kwenye kula" badala ya useme amenisaidia. Get your facts right.
Unaandika maelezo meengi lakini hoja ni mbili ama tatu ..

Nimekuambia hapo Uingereza na Ufaransa walijitia kiherehere kwenda kupambana na Hitler kilichowakuta ilibidi wananchi wapige kasia za mikono hadi Dunkirk kuokoa askari wao.... Tandikwa sana na mjerumani.... Intel ya Soviet iliona hilo mapema sana...

Kiherehere cha US kutoa misaada ni baada ya kuona alichosema Soviet miaka ya nyuma ni sahihi kwamba waungane ni sahihi, naweza kukuambia Soviet walikuwa na intel makini kuliko Uingereza ama US... Soviet hakuomba misaada ni US walipeleka wenyewe kama walivyopeleka Uingereza, France n.k....

Soviet walipambana man to man, hilo battle la Kursk hakuna raia walijitokeza kusaidia jeshi walipambana wakawazidi wajerumani na wakawafuata hadi kwao.... Soviet askari wake waliuawa wengi kwa sababu hao ndio washindi namba moja wa WW2... Hao ndio walimmaliza mjerumani US, France na Britain wakaja baadae wanajikongoja....

Soviets walipigana kiume, sio kama Britain wanakimbizwa kutoka Poland hadi wanakuja kuokolewa Dunkirk na mitumbwi ya wananchi...

Hakuna sehemu Soviets walizungukwa wakarudi nyuma , walipambana mbele kwa mbele, kila mjerumani akifanya mbinu na kujipanga jamaa wanakuja..

Ndio maana nikakuambia Hitler alijimaliza alipofahamu Soviets wanakaribia Berlin na si France wala Britain au baba yao US....

Soviets roho ya paka, nguvu aliyotumia Germany east kumkabili Soviet ilikuwa ni nyingi mno kiliko aliyotumia kuwakabili west , lakini Soviet wakawa wa kwanza kugonga hodi Berlin ... m@mae...

Kuhusu kupoteza askari wengi nimesema hapo Germany waliongeza nguvu kadri ilivyowezekana mashariki wakipunguza nguvu magharibi lakini haikusaidia...

Unapozungumzia vita Russia ndio viumbe wenye damu za vita hilo hata NATO wanatambua... Hawana useng3 sijui air superiority imefanya nini mara blah blah blah, wenyewe ni mguu kwa mguu unatandikwa hadi unakimbia mwenyewe .... Aliyemmaliza Germany ni Soviet hilo lipo wazi ....

Soviets sio waoga elewa hilo kwanza, Germany ilidhani ingewatisha kwa kuwaua wengi pale Kursk lakini kila wanapokufa jamaa wengine wanakuja na mzuka wanaanza moja , m@mae... Germans wakaona hawa ni alien ama watu, wakaanza kurudi nyuma wenyewe....

Britain walikuwa wanakimbia vita, vita ya ujanja ujanja, ndio maana France shoga yake alipigwa akafuatwa hadi kwake Paris huku Britain yupo hoi akitizama shoga yake anaolewa ndoa ya mkeka na mjerumanj na jamaa kaufyata....

Hitler ujanja wake na nguvu zake ziliishia kwa Soviets...

Ndio maana hadi leo hakuna mpuuzi na NATO yote atajitoa akili mbele yao.
 
Lakini kumbuka, nguvu ya Russia ya wakati wa ww2 hauwezi linganisha na nguvu iiliyonayo leo, sielewi ni mazingira ama utawala!

Iweje Ukraine nchi iliyokuwa ni mkoa wake ihangaike nayo kwa zaidi ya miaka miwili, je ikipambana na Uingereza sasa, jino kwa jino, bado utaitabiria ushindi Russia?
Btw Ukraine ilikuwa sehemu muhimu sana ya jeshi la USSR kwa wapiganaji hasa professionals na teknolojia za kijeshi.

Ndio maana hadi leo Putin anashindwa kuelewa kwa nini Ukraine iwe nje ya Russia na kuambatana na mahasimu wa EU/NATO. Anataka sana kusahihisha hilo kosa la viongozi waliomtangulia.
 
Shukrani sana Mkuu kwa madini adimu na chakula Bora Cha ubongo.

Hii ndiyo raha ya jamii forum.

Mkuu tuletee madini kuhusu nguvu za Paul Kagame kijeshi!!

Hivi ni kweli akilianzisha na bongo, TZ itakuwa kama Simba anapocheza na yanga???
Paul Kagame hana resources za kupigana na kuishinda Tanzania. Kwa kiasi fulani ana troops wazuri, ila vita sio troops pekee. Uchumi, landmass, population, political stability, landlockedness, weapons vinamkataa.
 
Umeandika matango tu na nimeona vichache nikujibu kwa sababu unaongozwa na mahaba....

Kwanza tambua lengo la Soviet kujiunga na Hitler, ndipo ujue intel ya soviet haikuwa ya kitoto, Soviet waliona mapema uwezo wa kijeshi wa Germany haukuwa wa kubezwa, mapema sana akawaomba Britain, US, France waungane kumkabili Germany, wakajifanya wajuajj kwamba wana uwezo kijeshi huku wakimtenga Soviet kisa masuala ya ujamaa na blah blah blah kibao....

Baada ya kuteremshiwa kipondo heavy na Germany ndipo akili ikawakaa sawa na kukumbuka Soviet alisema nini ... Soviet aliona pekee itakuwa ngumu kumkabili Germany akaona kama huwezi shindana nae basi ungana nae...

Battle of Dunkirk hao wafaransa na British walitandikwa askari zaidi ya 338K walitaka kumalizwa pale Dunkirk wamezungukwa na askari wa Hitler, hivi unaelewa kwanza askari laki tatu elfu thelathini na nane ni wengi kiasi gani? Na wame surrender wamezungukwa.... Operation dynamo ndipo hadi raia wenye mitumbwi wanapeleka kuokoa askari hao, ndio maana wakaita miracle of Dunkirk, unaweza kuelewa jeshi la Germany lilikuwa na nguvu kiasi gani kuzunguka hao askari wa France na Britain ...

Acheni ushabiki wa kipuuzi na mahaba....

Nazi Germany walikuwa wanatisha, lakini walikaa kwa Soviet tandikwa hadi kwao....

Ndio maana kutoka Magharibi walijipanga US, France na Britain, huku eastern front chinja chinja wazee wa kazi Soviet wakimmaliza Germany hadi Berlin....

Unaisifia ooooh Britain sijui blah blah blah... Walipigwa hadi askari wao wakaokolewa na mitumbwi ya wananchi wazalendo, tandikwa kweli kweli choka mbaya *****.... Hadi wanaomba msaada....

Kiherehere kikawaisha, na hapo wakakumbuka waSoviet, tena Soviets waliwatahadharisha miaka nyuma, wakakumbuka Sovieta waliwaambia nini kuhusu kuungana kummaliza Germany....

Ndipo wakaanza kushirikiana na Soviet kwa aibu, huku wamechelewa, wamepoteza askari wengi na wengi kukamatwa, wangemsikiliza Soviet hayo yote yasingetokea...

Kijana kasome historia ...
Ni upofu tu huyo na chuki yake dhidi ya Russia inayomfanya anashindwa kusimamia ukweli.

UK alichakazwa akatulia hakuwa na nguvu yoyote ya kuleta mapinduzu dhidi ya Germany.

France alipigwa ndani ya miezi 6 na Hitler jeshi lake lina pita mitaani raia wanaona jeshi la Nazi likipita mitaani kwa ushindi.

Nguvu kubwa sana Hitler akiipeleka Russia. Na akitaka ajue hili aangalie idadi ya kikosi alichokipeleka Hitler kwa mara ya kwanza Russia.

Alipeleka jeshi kubwa ambalo hakupeleka nchi yoyote tangu aanze mashambulizi yake.
 
Mkuu T14 Armata hua unaizungumzia Russia kiudogo sana, sijajua sababu lakini naona una chuki binafsi na hawa watu.

Ukiangalia leo idadi ya sanctions ambazo Russia amewekewa na Collective west ni nyingi, mfano kwa hadi February mwaka huu EU wameweka jumla ya sanctions 200 kwa taasisi na watu binafsi wanaoweza kuisaidia Russia kupata siraha. USA yenyewe imeweka sanctions mpya 500.

Lakini Russia ameendelea kuchukua maeneo zaidi kila siku, mathalan kabla ya mwaka 2022 Russia alikua amechukua maeneo ya Ukraine jumla ya 42,000 sqkm ambayo ni Crimea na baadhi ya maeneo ya Donetsk na Luhansk.
Baada ya full scale invasion Russia amechukua 119,000 sqkm ambapo ukichukua na ile ya mwanzo ni jumla ya 27% ya ardhi ya Ukraine ipo mikononi mwa Russia.

Pamoja na sanctions zote ikiwemo kuzuia jumla ya dollars billions 300 za Russia katika mabenki ya Ulaya na America ila uchumi wa Russia umeendelea kukua zaidi, mwaka jana pekee uchumi wa Russia umekua kwa 3.6% ambayo hii ni zaidi ya America ambayo uchumi umekua kwa 2.5% au Ulaya ambayo imekua kwa 0.4%.

Nakushauri ndugu yangu, Russia ni lidude likubwa sana la kutisha linaoangamiza kila kitu kinachokuja mbele yake, ipende Russia au usiichukie sababu ukiendelea kuichukia utakuja kuumwa presha ya bure kabisa tukupoteze mazima
umewahi kuwafuatilia watu wanaofanya jihad (kina Al shabab et al) jinsi saikolojia zao zilivyo? huwa wakilishwa propagabda wamelishwa,...... hili ndio linawasumbua baadhi ya prowest humu jukwaan akiwepo huyo uliomtag!

NATO iliundwa kupambana na Mrusi, mpk leo wanapambana na mrusi lakini wao hata hawaelewi,..

hii vita ya Ukraine ukiwaambia anaepigana ni NATO (akitumia wanajeshi wa Ukraine) wanakupinga, sasa unajiuliza, mtu anatoa vifaa vita, pesa, logistic, anacontrol intelligence, anatumia satelite zake, anakuwaje hapigani? wanabaki kuzunguka na ngonjera nyingi!

sometimes ni kuwaelewa tu kwamba wamekua too much programmed, watu kama hawa ni hatari kuwa viongozi kwenye nchi yenu!
 
Sababu za Wahindi kutojiunga na JWTZ au KDF (jeshi la Kenya) ni zilezile.

Wao ni watazama fursa, wakati wabongo wengi walikuwa watazama sifa. Wakati tunapata uhuru kati ya kada zilipelekwa zaidi nje kusoma ni jeshi maana hatukuwa na vyuo vya kijeshi wala uzoefu. Maofisa wetu walienda UK, Urusi China, etc. Na walienda kusoma kozi ngumu za gharama kubwa kulipiwa na mwanafunzi. Wakafaulu wakiwa wataalamu wa mitambo, marubani, wasomi wa political science, wenye exposure nje.

Kwa sababu Wahindi hawawezi kuwa wazalendo wa nchi ya Kiafrika hivyo wakawa wanasomeshwa kwa gharama za serikali ila wanawaza wapate kazi nzuri. Na majeshi hayakulipa vizuri wanaita uzalendo, wakawa wanaacha kazi wanaenda mtaani na elimu zao wanalipwa vizuri zaidi au wanahama nchi.

Vilevile Wahindi wasingepanda sana vyeo, hawaonekani wazawa. Kwahiyo ikakosekana maana ya wao kupenda vyombo vya usalama na ulinzi.
Hivi unafahamu miaka ya nyuma ya mwanzoni wa uhuru wahindi walikuwepo jeshini? Na wengine walistaafu kabisa na vyeo vyao vya juu?

Na machotara wengineo walikuwepo jeshini?
 
Soviets roho ya paka, nguvu aliyotumia Germany east kumkabili Soviet ilikuwa ni nyingi mno kiliko aliyotumia kuwakabili west , lakini Soviet wakawa wa kwanza kugonga hodi Berlin ... m@mae...
Mpaka makamanda wa Germany wakawa wanasema maiti ya warusi iuwe mara 2.

Yaani umepiga risasi kafa iuwe tena maiti, ukipiga mara 1 Mrusi anaweza akafufuka.
Kuhusu kupoteza askari wengi nimesema hapo Germany waliongeza nguvu kadri ilivyowezekana mashariki wakipunguza nguvu magharibi lakini haikusaidia...
Defensive line ya mwisho wanapambana na jeshi la Hitler wanauliwa wanabaki 28. Makamanda wanaomba reinforcement wanaambiwa hakuna nyinyi ndiyo line ya mwisho. Baada ya nyinyi inayofuata ni Moscow.

Warusi walipambana walibaki 6 tu! Wengine wote walikufa. Mpaka leo wamejenga masananu yao kuwaenzi hao askari 6 waliyobaki.

West kwa vile hawawapendi Russia wanabaki kusema ni myth! Ila ingelikuwa wao wangejipamba kwa maneno matamu na mazuri mengi.
 
Back
Top Bottom