Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,440
- 8,149
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anasema majeshi yake yanasonga mbele ‘’hatua kwa hatua’’ katika eneo la kusini linalokaliwa la Kherson.
Mji wa Kherson ulitekwa na Urusi mapema katika vita na unakaa kwenye eneo la kimkakati magharibi mwa mto Dnipro.
Siku ya Jumamosi, maafisa wa ulinzi wa Uingereza waliripoti mapigano makali karibu na Kherson.
Hatua hiyo ya mapema ya Ukraine ilimaanisha kuwa njia za usambazaji bidhaa za Urusi magharibi mwa mto zilikuwa ‘’hatarini zaidi’’, kulingana na tathmini yao.
Mapema mwezi huu, Naibu Waziri Mkuu wa Ukrainia Iryna Vereshchuk aliwataka wakaazi wa Kherson kuhama mji huo haraka iwezekanavyo ili kuepuka kunaswa katika jiji hilo wakati wa makabiliano makali Ukraine kusini.
‘’Ni muhimu kufanya hivyo kwa vikosi vya wanajeshi vya Ukraine kutohatarisha raia wakati wa operesheni za kukera,’’ aliiambia TV ya serikali.