johnthebaptist,
Vyama vya upinzani vinatambulika kisheria na msajili wa vyama vya siasa.
Hivyo mtanzania yeyote hatakuwa amefanya kosa akijiunga na chama chochote cha siasa chenye usajili wa muda au chenye usajili wa kudumu katika daftari la Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania. Kisha kushiriki katika shughuli halali za chama hicho kwa namna yoyote ile iwe ya kisiasa , utumishi, kujitolea, uongozi n.k
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Karibu kwenye tovuti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa . Kupitia tovuti hii, utapata taarifa za uhakika juu ya shughuli za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini na taarifa za uhakika juu ya Vyama vya Siasa.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imejikita katika usimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa Na 5 ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 ili kuhakikisha uwepo na ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini.
SOMA ZAIDI KUHUSU OFISI HII :bofya
Source :
ORPP Website