Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Ombi hilo limetolewa Seotemba 23, 2026 baada ya Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado kumaliza kuzungumza na wananchi hao katika ziara yake ya Kijiji kwa Kijiji, ambapo wananchi waliongozana naye hadi kwenye kisima wanachokitumia kwa shughuli zao za kila siku.
Wananchi hao wamemweleza Ado kuwa hali ya kisima hicho ni changamoto, huku wakidai kuwa matumizi ya maji hayo wakati mwingine yamekuwa yakisababisha matatizo ya kiafya.
“Hayo ndo maji tunayokunywa tuna visima vitatu hali yake ndo hiyo na tukinywa haya maji muda mwengine tunaharisha”
Akijibu kilio hicho, Mbunge Ado ameahidi kulifikisha suala hilo kwa Waziri mwenye dhamana ya Maji, Jumaa Aweso kwa lengo la kutafuta suluhisho la changamoto hiyo na kuwawezesha wananchi kupata maji safi na salama.
Pia soma ~ Ado ampigia simu Waziri Aweso kuhusu shida ya maji Tunduru, asema atatuma timu kutoka Wizarani