DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Ni katika mtaa wa Sokoni One, kata ya Sinoni jijini Arusha, ambapo asubuhi ya leo Februari 1, 2026, wananchi wa eneo hilo wameandamana na kufunga barabara inayotoka Sinoni kuelekea Ngusero kwa takribani masaa matatu.
Wananchi hao wanapaza sauti wakiiomba Serikali na mamlaka husika kuweka bamsi katika barabara hiyo, wakisema kutokuwepo kwa bamsi kumesababisha ajali za mara kwa mara zilizopelekea vifo, majeraha pamoja na vilema vya kudumu.
Wakizungumza na Jambo TV, wananchi hao wamesema kuwa kukosekana kwa bamsi katika eneo hilo kunasababisha vyombo vya moto kupita kwa kasi, hali inayochangia kuongezeka kwa ajali hizo.
Hata hivyo, baada ya muda mfupi, Jeshi la Polisi lilifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kutuliza hali ya taharuki, ambapo kwa kushirikiana na baadhi ya wananchi walianza kuondoa vizuizi vilivyowekwa barabarani, ikiwemo mawe, yaliyokuwa yamesababisha vyombo vya usafiri kushindwa kupita.
Taharuki hiyo ilitulia zaidi baada ya kufika Diwani wa Kata ya Sinoni, Peter Enyasi, ambaye aliwahakikishia wananchi kuwa ndani ya siku saba atashughulikia changamoto hiyo kwa kushirikiana na mamlaka husika.
Baada ya ahadi hiyo, wananchi hao wamesema kuwa endapo ahadi hiyo haitatekelezwa, wako tayari kurudi barabarani hadi pale bamsi litakapowekwa katika eneo hilo.