DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Baadhi ya wakazi wanaoishi karibu na eneo linalodaiwa kujengwa Kanisa la Arise and Shine (Kawe), linaloongozwa na Apostle Boniface Mwamposa, wameeleza malalamiko yao kuhusu athari zinazodaiwa kusababishwa na ujenzi huo.
Wakizungumza Julai 1, 2025, Saa tatu asubuhi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, wananchi hao wamedai kuwa tangu ujenzi wa Kanisa hilo uanze, baadhi ya maeneo yamekumbwa na matatizo ya upatikanaji wa maji, hali inayotokana na uharibifu wa miundombinu unaodaiwa kufanywa na wakandarasi wa mradi huo wa ujenzi.
Mbali na suala la maji, Wananchi hao pia wamelalamikia kutaka kufungwa kwa barabara waliyokuwa wakitumia, baada ya sehemu ya njia hiyo kuwekwa uzio.
Baada ya kusikia malalamiko hayo, Mkuu wa Wilaya, Saad Mtambule aliamuru kusitishwa kwa ujenzi huo kwa muda, ili kutoa nafasi ya kufanya tathmini ya kina. Alibainisha kuwa atakutana na watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), linalodaiwa kumkodisha eneo hilo kwa Mwamposa, pamoja na wawakilishi wa wananchi, kabla ya kufanya mkutano wa pamoja na Wananchi jioni ya leo saa 10 (Julai 1, 2025).
Mtambule amesema lengo ni kuhakikisha haki zinalindwa huku pia wakiheshimu taratibu za umiliki na matumizi ya ardhi.
Pia soma ~ DC Kinondoni: Ramani haioneshi barabara zinazodaiwa kuzibwa kupisha Kanisa la Mwamposa