LGE2024 Wananchi Kibosho wakarabati barabara zote za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

luambo makiadi

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2017
Posts
10,602
Reaction score
8,798
Wakuu salaam,

Wananchi wa kata ya Kibosho halmashauri ya wilaya ya Moshi wamekarabati barabara zote za eneo hilo kwa michango yao binafsi.

Wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa muda mrefu wana utamaduni wa kuchangia shughuli za kimaendeleo bila kutegemea serikali.

Siku chache zilizopita wananchi wa kata za marangu mashariki,mwika kaskazini walifanya jambo hilo hilo

Na mwaka 2017 wananchi wa Vunjo walivunja rekodi ya michango Kitaifa kwa kuchangia shilingi bilion 7 kukarabati barabara zote za Jimbo hilo.

Hongereni Wana Kilimanjaro


Chanzo: Azam news
 

Wale wa Manispaa ya Kahama kuna jambo la kujifunza hapa.
 
Huko huwa wana kawaida kuchagua upinzani na wote wanaochagua upinzani serikali ya ccm ilishasema wazi haitopeleka maendeleo kwa hiyo lazima wajiongeze
 

Tunamsifu Rais wetu kwa kuwawezesha kuwa na demokrasi ambayo imewapa fursa wananchi wa Kibosho kutupigia story za ujenzi wa barabara
 
Hii imetokea pia barabara ya kuelekea Hospitali ya Seliani Ngaramtoni ARUSHA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…