LGE2024 Wananchi Kibosho wakarabati barabara zote za mitaa

LGE2024 Wananchi Kibosho wakarabati barabara zote za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Wakuu salaam,

Wananchi wa kata ya Kibosho halmashauri ya wilaya ya Moshi wamekarabati barabara zote za eneo hilo kwa michango yao binafsi.

Wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa muda mrefu wana utamaduni wa kuchangia shughuli za kimaendeleo bila kutegemea serikali.

Siku chache zilizopita wananchi wa kata za marangu mashariki,mwika kaskazini walifanya jambo hilo hilo

Na mwaka 2017 wananchi wa Vunjo walivunja rekodi ya michango Kitaifa kwa kuchangia shilingi bilion 7 kukarabati barabara zote za Jimbo hilo.

Hongereni Wana Kilimanjaro

Chanzo: Azam news
Wamekataza kupigwa picha mkuu?
 
Huko huwa wana kawaida kuchagua upinzani na wote wanaochagua upinzani serikali ya ccm ilishasema wazi haitopeleka maendeleo kwa hiyo lazima wajiongeze
Jimbo la Vunjo waliwahi kuchanga bilioni 9 kujenga barabara zao Magufuli akazuia ile account sasa wawe waangalifu huko Kibosho mama asije akawazuia kukarabati barabara zao.
 
Jimbo la Vunjo waliwahi kuchanga bilioni 9 kujenga barabara zao Magufuli akazuia ile account sasa wawe waangalifu huko Kibosho mama asije akawazuia kukarabati barabara zao.
Jiwe alkuwa mshamba alichanganyikiwa Jimbo Moja kuchangia ma bii
 
Jimbo la Vunjo waliwahi kuchanga bilioni 9 kujenga barabara zao Magufuli akazuia ile account sasa wawe waangalifu huko Kibosho mama asije akawazuia kukarabati barabara zao.
Yaan huyo baba jaman ,amekataa kujenga barabara wananchi wamejichangisha ela Yao yy anaizuia ,sjui alitaka wachangishe zienda Chato
 
Back
Top Bottom