Wananchi kuweka Mageti ya ukaguzi mitaani ni ishara ya kushindwa kwa Jeshi la Polisi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Sasa hivi maeneo mengi ya Mkoa wa DSM wananchi kwa umoja wao wameamua kuajiri walinzi binafsi na kuweka Vizuizi vya ukaguzi kwenye mitaa, ukifika kigamboni au Mbezi Beach ni lazima wenyeji wako wathibishe ujio wako mbele ya walinzi , vinginevyo utaishia njiani .

Pamoja na pongezi hizi kwa Wananchi kwa kuamua kujilinda Wenyewe na wahalifu, lakini kuna tafsiri kwamba jambo hili ni ishara ya Polisi kushindwa kutekeleza majukumu yao ya Halali baada ya kuelemewa na majukumu yasiyowahusu ya kisiasa.
 
Pathetic fool!! Ulinzi shirikishi wakati polisi wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi ili kuwalinda???

Kweli kabisa mkuu, wananchi wanalipa kodi kibao zinazotumika mpaka kugharamia vyombo vya ulinzi na usalama, lakini wanatugeuza kuwa vigilantes, watuambie fedha zinazokwenda wizara ya mambo ya ndani zinatumika vipi na kama hazitoshi basi serikali ipunguze gharama ya kuendesha serikali kuu kwa kuacha kununua magari ya serikali ya kifahari, samani/fanicha za kutisha tunazoziona ktk ofisi za serikali, serikali iache kugharamia bando za kununua vocha kwa wakubwa watumie WhatsApp n.k Ili waache kuwatumia wananchi kuwa mgambo/ vigilantes.

vigilantes
a member of a self-appointed group of citizens who undertake law enforcement in their community without legal authority, typically because the legal agencies are thought to be inadequate.
 
Nyie watu wa mujini mnadeka sana. Hivi mnadhani huku vijijini kusiko na vituo vya polisi tunalindwa na nani? Au mnadhani huku vijijini hatulipi kodi inatustahirisha kulindwa na polisi?
Kazi yenu kulialia tu kila siku na kutaka mlindwe wakati mmelala; wapuuzi sana nyie.
Jilindeni wenyewe, kama ni kodi sote tunalipa, basi polisi wasambazwe nchi nzima.
 
Pathetic fool!! Ulinzi shirikishi wakati polisi wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi ili kuwalinda???
Nadhani huelewi siku jambazi akivamia nyumbani kwako ukapiga kelele halafu hata jirani mmoja asikusaidie hata kupiga yowe ndipo utajua maana ya ulinzi shirikishi

Au uwe stendi ukabwe na kibaka hadharani halafu usione mwananchi yeyote wa kutusaidia ndipo utaelewa ulinzi shirikishi Ni Nini
 
Sasa hivi maeneo mengi ya Mkoa wa DSM wananchi kwa umoja wao wameamua kuajiri walinzi binafsi na kuweka Vizuizi vya ukaguzi kwenye mitaa , ukifika kigamboni au Mbezi Beach ni lazima wenyeji wako wathibishe ujio wako mbele ya walinzi , vinginevyo utaishia njiani .

Pamoja na pongezi hizi kwa Wananchi kwa kuamua kujilinda Wenyewe na wahalifu , lakini kuna tafsiri kwamba jambo hili ni ishara ya Polisi kushindwa kutekeleza majukumu yao ya Halali baada ya kuelemewa na MAJUKUMU YASIYOWAHUSU YA KISIASA .
Ukisoma sheria ya ugaidi na tafsiri yake utajua kabisa serikali ya ccm haina tofauti na ile ya Talibani
 
Ina maana hiyo mitaa makapuku kama Mimi ambao ha tuna mwenyeji wala ndugu haturuhusiwi kwenda kutembea????
 
Kweli kabisa mkuu, wananchi wanalipa kodi kibao zinazotumika mpaka kugharamia vyombo vya ulinzi na usalama, lakini wanatugeuza kuwa vigilantes, watuambie fedha zinazokwenda wizara ya mambo ya ndani zinatumika vipi na kama hazitoshi basi serikali ipunguze gharama ya kuendesha serikali kuu kwa kuacha kununua magari ya serikali ya kifahari, samani/fanicha za kutisha tunazoziona ktk ofisi za serikali, serikali iache kugharamia bando za kununua vocha kwa wakubwa watumie WhatsApp n.k Ili waache kuwatumia wananchi kuwa mgambo/ vigilantes.

vigilantes
a member of a self-appointed group of citizens who undertake law enforcement in their community without legal authority, typically because the legal agencies are thought to be inadequate.
hehehe
 
Sasa hivi maeneo mengi ya Mkoa wa DSM wananchi kwa umoja wao wameamua kuajiri walinzi binafsi na kuweka Vizuizi vya ukaguzi kwenye mitaa , ukifika kigamboni au Mbezi Beach ni lazima wenyeji wako wathibishe ujio wako mbele ya walinzi , vinginevyo utaishia njiani .

Pamoja na pongezi hizi kwa Wananchi kwa kuamua kujilinda Wenyewe na wahalifu , lakini kuna tafsiri kwamba jambo hili ni ishara ya Polisi kushindwa kutekeleza majukumu yao ya Halali baada ya kuelemewa na MAJUKUMU YASIYOWAHUSU YA KISIASA .
umetaja maeneo mawili tu. mbezi beach na kigamboni? ni sehem ndogo sana ya hii nchi.
labda kama wananchi nchi nzima wameweka vizuizi.
umeweka as if ni tanzania nzima wananchi wote wamefanyahikokitu kumbe wapi. asilimia kubwa nchini hawajachukua hatua hizo.
suala la ulinzi binafsi limekuwepo miaka mingi sana. si kitu cha juzi wala jana.
lakin asilimia kubwa hawawezi ku afford hizo services.
 
Sasa hivi maeneo mengi ya Mkoa wa DSM wananchi kwa umoja wao wameamua kuajiri walinzi binafsi na kuweka Vizuizi vya ukaguzi kwenye mitaa , ukifika kigamboni au Mbezi Beach ni lazima wenyeji wako wathibishe ujio wako mbele ya walinzi , vinginevyo utaishia njiani .

Pamoja na pongezi hizi kwa Wananchi kwa kuamua kujilinda Wenyewe na wahalifu , lakini kuna tafsiri kwamba jambo hili ni ishara ya Polisi kushindwa kutekeleza majukumu yao ya Halali baada ya kuelemewa na MAJUKUMU YASIYOWAHUSU YA KISIASA .
Plc wapo buzy na chadema
 
Kweli kabisa mkuu, wananchi wanalipa kodi kibao zinazotumika mpaka kugharamia vyombo vya ulinzi na usalama, lakini wanatugeuza kuwa vigilantes, watuambie fedha zinazokwenda wizara ya mambo ya ndani zinatumika vipi na kama hazitoshi basi serikali ipunguze gharama ya kuendesha serikali kuu kwa kuacha kununua magari ya serikali ya kifahari, samani/fanicha za kutisha tunazoziona ktk ofisi za serikali, serikali iache kugharamia bando za kununua vocha kwa wakubwa watumie WhatsApp n.k Ili waache kuwatumia wananchi kuwa mgambo/ vigilantes.

vigilantes
a member of a self-appointed group of citizens who undertake law enforcement in their community without legal authority, typically because the legal agencies are thought to be inadequate.
ukitaka kujua fedha za wizara ya ulinzi nenda tu wizarani omba report. tena fanya appointment na waziri husika.
ukisubiri wakuwekee hiyo report public utangoja sana.

for the record tu vigilantes hawajaanza leo wala jana.. kuna ambao walishatangulia before.
ila kama kawaida yenu wabongo waoga wanafki mpaka kudai haki zao ni ngumu. wanaishia tu kulalamika online
 
Pathetic fool!! Ulinzi shirikishi wakati polisi wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi ili kuwalinda???
Kwasababu unalipa kodi subiri siku aje jambazi kukutembelea nyumbani kwako, halafu ukishapapaswa kwa upumbavu wako ukawalumu polisi kwanini umepapaswa wakati unalipa kodi.

Hivi kama unalipa kodi kwanini unalala kwenye nyumba yenye mlango? au kwa haya mawazo yako unaweza kuwa unaishi pangoni.
 
Kweli kabisa mkuu, wananchi wanalipa kodi kibao zinazotumika mpaka kugharamia vyombo vya ulinzi na usalama, lakini wanatugeuza kuwa vigilantes, watuambie fedha zinazokwenda wizara ya mambo ya ndani zinatumika vipi na kama hazitoshi basi serikali ipunguze gharama ya kuendesha serikali kuu kwa kuacha kununua magari ya serikali ya kifahari, samani/fanicha za kutisha tunazoziona ktk ofisi za serikali, serikali iache kugharamia bando za kununua vocha kwa wakubwa watumie WhatsApp n.k Ili waache kuwatumia wananchi kuwa mgambo/ vigilantes.

vigilantes
a member of a self-appointed group of citizens who undertake law enforcement in their community without legal authority, typically because the legal agencies are thought to be inadequate.
Hii mentality ndio inawafanya muonekane wakulia lia, polisi hata kama wapo hawawezi kulinda kila nyumba, kila mtaa, Tanzania nzima.
 
Back
Top Bottom