Wananchi kuweka Mageti ya ukaguzi mitaani ni ishara ya kushindwa kwa Jeshi la Polisi

Wananchi kuweka Mageti ya ukaguzi mitaani ni ishara ya kushindwa kwa Jeshi la Polisi

Kama vile hujamuelewa mtoa mada. Sio kwamba napingana na wewe au yeye anapingana na wewe ila rudia tena kusoma ile uweze kuelewa mantiki ya hoja yake.
Mkuu nimeelewa sana mada ndo maana wengine tumejiongeza lakini askari wetu pia wamekua wakitoa ushirikiano wa hali ya juu sana km wakiona no ya kamanda wetu akiita difenda fasta tu wanafika kwa kweli hili swala tusilete siasa humo maana tunajua tz ni kubwa mno na askari hawawezi kulinda kila mtaa.Tutatokomeza huu ukabaji na ujambazi wa hovyo pia na kuripoti watu mnao hisi si wazuri wanapo ingia mitaani kwenu sio mpaka msubiri polisi kisa eti wanalipwa na kodi zetu.
 
Nyie watu wa mujini mnadeka sana. Hivi mnadhani huku vijijini kusiko na vituo vya polisi tunalindwa na nani? Au mnadhani huku vijijini hatulipi kodi inatustahirisha kulindwa na polisi?
Kazi yenu kulialia tu kila siku na kutaka mlindwe wakati mmelala; wapuuzi sana nyie.
Jilindeni wenyewe, kama ni kodi sote tunalipa, basi polisi wasambazwe nchi nzima.
Sasa huko kijijini kwenu vibaka wanakuja kuiba nini? Au vigunia vya kuogea?

Jaribu kuwa mtulivu wakati watu wa mjini tunajadili masuala ya kitaifa!

Haya tafuna mihogo yako kimya kimya!
 
Nikiyasikia hayo na kuangalia wingi wa askari wanaolinda taa nyekundu ya barabarani kwa dereva aliyekosea naona kama kuna matumizi mabaya sana ya kada hii ya askari!! Polisi wengi wamejipanga barabarani na kusahau ile dhana ya kulinda RAIA na Mali zao!! Wao wanachojua ni kujiweka barabarani kwa vile kuna masilai yao!
 
Na hata huko ni baadhi ya mitaa tu. Ni upuuzi kuweka kizuizi kwenye barabara ya umma mtu asipite mpaka aseme anaenda kwa nani. Kwahio siwezi kukatiza mtaa huo nikatokea mtaa mwingine kuendelea na safari yangu? au mitaa yao haitoki upande mmoja?

Ndiyo u vigilante, basi itafikia miji yetu baada ya vizuizi watajenga ngome kuzunguka miji , vitongoji na vijiji.

Nchi inazidi kumeguka toka taifa kuwa vitaifa vidogo vidogo siku zijazo wataomba kuwa na silaha kali zaidi ya mishale na mapanga maana watazidi kuona jinsi dola / serikali inavyowatupa huku wananchi wakizidi kupambana na majambazi, maharamia na wezi wa mifugo wenye silaha kali.

Dola kukusanya kodi kisha wakaitumia kwa vitu vya kifahari kama magari ya gharama kubwa na kushindwa kutoa huduma za usalama kwa raia ni ishara tosha ya dola kushindwa majukumu yake.

Living By The Gun in Turkana Kenya , sign of a failed state?


The use of guns has mainly been a preserve of men among the pastoralist communities as they battled raiders and other potential attackers. But a group of women and young girls in Turkana North, some as young as 14 years are going against the grain by using arms to protect their lives and property after quite a number of their men were killed by raiders. Franklin Macharia brings us the story of courage and determination by the women and girls of Turkana in our new series, living by the gun
 
Nikiyasikia hayo na kuangalia wingi wa askari wanaolinda taa nyekundu ya barabarani kwa dereva aliyekosea naona kama kuna matumizi mabaya sana ya kada hii ya askari!! Polisi wengi wamejipanga barabarani na kusahau ile dhana ya kulinda RAIA na Mali zao!! Wao wanachojua ni kujiweka barabarani kwa vile kuna masilai yao!
2082683_FB_IMG_1559946076802.jpg
 
Sasa huko kijijini kwenu vibaka wanakuja kuiba nini? Au vigunia vya kuogea?

Jaribu kuwa mtulivu wakati watu wa mjini tunajadili masuala ya kitaifa!

Haya tafuna mihogo yako kimya kimya!
Muone, mwanaume wa Dar wewe. Kazi kulialia tu mdekezwe kama wanawake. Jamii zote za kiafrika toka enzi na enzi wanawake na watoto ndiyo huwa wanalindwa, wanaume hujilinda. Sasa tumepata kundi la tatu, wanaume wa mjini.
Wanastahili kulindwa: wanawake, watoto, na wanaume wa mujini 😂😂
Jide yuko sahihi, 'wanaume kama mabinti'.
 
Back
Top Bottom