Kwa mawazo yangu uhaba wa vituo vya polisi sio tatizo. Tatizo ni kutokuwa na polisi wanaozunguka mtaani kutuhakikishia usalama wetu. Hawa kwa kuzunguka mtaani ndio wangewajua watu wanaoishi humo na wangeweza kuitikia mapema pale tukio la uhalifu linapotokea. Vituo vya polisi vinawageuza watu wa mezani ambao wanangojea kuitwa tukio likitokea. Hali hii ndio inapelekea kuwa ukiripoti tukio unaambiwa kamkamate unayemshuku uwaletee! Kwa maneno mengine kazi yao wame outsource kwa raia. Kwa wenzetu, kituo cha polisi ni mtaani ambako wana patrol kwa kutumia miguu, baiskeli au magari. Tuache kuwajengea vituo, tuwanunulie baiskeli.
Amandla....