ngosha wa mwanza
JF-Expert Member
- Feb 23, 2015
- 3,832
- 11,964
Mkuu nimeelewa sana mada ndo maana wengine tumejiongeza lakini askari wetu pia wamekua wakitoa ushirikiano wa hali ya juu sana km wakiona no ya kamanda wetu akiita difenda fasta tu wanafika kwa kweli hili swala tusilete siasa humo maana tunajua tz ni kubwa mno na askari hawawezi kulinda kila mtaa.Tutatokomeza huu ukabaji na ujambazi wa hovyo pia na kuripoti watu mnao hisi si wazuri wanapo ingia mitaani kwenu sio mpaka msubiri polisi kisa eti wanalipwa na kodi zetu.Kama vile hujamuelewa mtoa mada. Sio kwamba napingana na wewe au yeye anapingana na wewe ila rudia tena kusoma ile uweze kuelewa mantiki ya hoja yake.
Sasa huko kijijini kwenu vibaka wanakuja kuiba nini? Au vigunia vya kuogea?Nyie watu wa mujini mnadeka sana. Hivi mnadhani huku vijijini kusiko na vituo vya polisi tunalindwa na nani? Au mnadhani huku vijijini hatulipi kodi inatustahirisha kulindwa na polisi?
Kazi yenu kulialia tu kila siku na kutaka mlindwe wakati mmelala; wapuuzi sana nyie.
Jilindeni wenyewe, kama ni kodi sote tunalipa, basi polisi wasambazwe nchi nzima.
Na hata huko ni baadhi ya mitaa tu. Ni upuuzi kuweka kizuizi kwenye barabara ya umma mtu asipite mpaka aseme anaenda kwa nani. Kwahio siwezi kukatiza mtaa huo nikatokea mtaa mwingine kuendelea na safari yangu? au mitaa yao haitoki upande mmoja?
Nikiyasikia hayo na kuangalia wingi wa askari wanaolinda taa nyekundu ya barabarani kwa dereva aliyekosea naona kama kuna matumizi mabaya sana ya kada hii ya askari!! Polisi wengi wamejipanga barabarani na kusahau ile dhana ya kulinda RAIA na Mali zao!! Wao wanachojua ni kujiweka barabarani kwa vile kuna masilai yao!
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Aiseee!Ukisoma sheria ya ugaidi na tafsiri yake utajua kabisa serikali ya ccm haina tofauti na ile ya Talibani
Muone, mwanaume wa Dar wewe. Kazi kulialia tu mdekezwe kama wanawake. Jamii zote za kiafrika toka enzi na enzi wanawake na watoto ndiyo huwa wanalindwa, wanaume hujilinda. Sasa tumepata kundi la tatu, wanaume wa mjini.Sasa huko kijijini kwenu vibaka wanakuja kuiba nini? Au vigunia vya kuogea?
Jaribu kuwa mtulivu wakati watu wa mjini tunajadili masuala ya kitaifa!
Haya tafuna mihogo yako kimya kimya!