Wananchi Mabogini Moshi wapaza sauti tatizo la Maji safi na salama

Wananchi Mabogini Moshi wapaza sauti tatizo la Maji safi na salama

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Wananchi wa Kata ya Mabogini wilaya ya Moshi Vijijini wamepaza sauti na kuitaka Mamlaka ya maji safi na uondoshaji majitaka Moshi mjini (MUWSA),kulitafutia ufumbuzi wa haraka tatizo hilo.

Wananchi hawa wanapaza sauti kupitia group la WthsApp la Maendeleo Mabogini .
Hapa chini ni moja ya mwananchi mmoja alietoa kilio chake.
Naomba tumsome

Daaah wananchi wanajifungiaje control valve? Ukweli sijui hata nisemeje? Maji yamekuwa changamoto kubwa labda control valve ya KKKT NEWLAND imevungwa au imejifunga kwa kweli. Ninazungumza kwa uchungu kwa sababu eneo la kanisani au shuleni au hospitali kunakuwa na mikusanyiko ya watu na uhitaji wa maji ni wa lazima kuepusha magonjwa ya mlipuko. Hapa KKKT tuna shule ya watoto wa awali maji hayatoki. Tumechimba kisima kwa ajili ya kukusanya hata hayo maji kidogo yanayoweza kutoka usiku lakini wapi.

Kwa nini Muwasa mnatufanyia hivi?

Maswali mawili tu ninajuliza miongoni mwa mengi....
1. Hivi hawa watoto wadogo wanaosoma hapa watakapopata magonjwa ya mlipuko tutakuwa na cha kujitetea? Je watakuwa na kosa gani hawa watoto mpaka tuwasababishie magonjwa kwa makusudi?
2. Pili afya za watu wanaokusanyika hapa mara kwa mara zinakuwa hatarini kiasi gani?
Je, mnatuambia tuishi maisha gani pasipo maji? Tunaweza kushukuru kwa kidogo lakini hata hicho kidogo hatukipati.

Mheshimiwa Diwani na viongozi wote pamoja na wasimamizi wa maji tunaombeni msaada wenu hali ni mbaya hapa kanisani hasa kwa hawa watoto wadogo.

Nimekuwa nikishuhudia watoto wa shule za Sumaye na Mvuleni wakikimbilia kanisani kuomba maji ya kunywa wakiwa na kiu kali. Wanapokosa maji huondoka wamenyong'onyea lakini wakiwa wameumia sana.

Jamani jaman narudia tena tusaidieni wasaidieni hawa watoto wanateseka kwa kweli.
 
Sijui tunachoweza ninini? Labda rushwa na majungu
 
Back
Top Bottom