Wananchi Mara waandamana kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli

Wananchi Mara waandamana kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli

Siku hizi haipiti siku mbili bila kusikia kile kinachotangazwa kuwa
'wananchi wanataka Magufuli aongezewe muda'

Na ukifuatilia zaidi unagundua sio wananchi bali ni 'mipango mipango' tu
ya watu wachache.....
cha kushangaza Magufuli hata nusu ya miaka mitano tu ya kwanza hajamaliza...
na wala sio kwamba anakaribia kufikisha miaka kumi ya urais wake

Lakini 'harakati za waziwazi sasa zinaonekana' za kuweka mazingira
ya kumuwezesha akae zaidi ya kikomo cha miaka 10 kama wenzie...
Swali la kujiuliza.....anataka kuwa Rais wa maisha?
ni kweli miaka 10 haimtoshi?

Kwa kuwa iyo nchi ni ya wajinga hata akiamua mle nya mtakula
 
Dalili ishaonekana kitambo moja ni namna anavyobana upinzani, mgogoro ndani ya CUF, na kukamata baadhi ya viongozi wa upinzani ni dalili kuwa jpm ataongeza mda tuko hapa narudia tena lazma atabadili katiba ili akae madarakani na haya maandamano wanaratibu wao
 
Muswaada kama huo uende bunge harafu wapiga kura ni kessy, kangi lugola, msukuma, maji marefu, lusinde, unategemea kura yao itakaaje
 
Sisi watanzania ndio tunataka Magufuli aendelee kutuongoza... walau miaka mingine 40 ili ayafutirie mbali mafisadi...
 
Atafanya nini cha maana akipewa hata aka mia,mwafrika ni mwafrika tu hakuna lolote atakalofanya zaidi ya kijilimbikizia mali yeye na bashite kiongozi mzuri hana tamaa ya madaraka ya mda mrefu ila viongozi wa bovu ndo tabia zao hizo ndo maana mambo hayo yanatokea Africa tu
 
Nenda hospital waangalie kama ndani ya fuvu lako kuna ubongo au ugali
Hahahah hata wakikuta mlenda na matembele potelea mbali kule. hiyo ni tafsiri ya jamaa sio yangu kamanda. Tartiiibu sindano itazama tu
 
Wewe umeendelea kwa kipi toka ameingia?
Mambo mengi sanaa. La mwisho kabisa gari yangu iliyokuwa inadaiwa road licence ya milioni tatu na nusu sasa iko barabarani inapiga kazi. Sema lingine
 
Kabla hata hawajajua kuwa huyu Ndugu ataishi Kuiona 2020, Kabla hata ya Huyu Ndugu Magufuli hajafikia Nusu ya Miaka Mitano, Tayari Kuna Majuha, Misukule wanaotaka ati Katiba ibadilishwe ili Magufuli atawale Milele. Kwa Hila na Unafiki nilio uona kwa Magufuli, eg Uzuia Mikutano ya Wapinzani na Kiacha yake na CCM, Sishangai kuwa yeye Ndiye anayewatuma hawa. Ili kunituliza imani hii Mbaya basi nisikie akikemea Haya!

Mnamtuma Mh. Mkapa Burundi Kusafisha mess iliyosababishwa na ujinga wa aina hii halafu na sisi bila ya aibu tunathubutu hata kuwaza huu wazimu?

Halafu Mimi najiuliza? Kulikuwa na Faida Gani kwa Mwalimu Nyerere Kufariki na Kutuachia Mwinyi na Mkapa? Najua sio Vizuri Wastaafu Kuingilia Rais aliyeko Madarakani lakini, Inafikia Wazi Rais aliyeko Madarakani anatakiwa Kukemewa na Hawa Wazee wazi wazi hata Kama ni Kisayansi. Mwinyi alifanya hivyo alivyosema Nchi inaendeshwa Kama Gari lisilo na Msukani, Punde akaitwa ikulu aongee kupooza Mambo! Lakini Shikamoo Mzee Mwinyi Ulisema Ukweli!

Hivi Leo Mwalimu Angefufuka akaona haya Maandamano ya Kijinga ya kutaka Kuvuruga Mfumo mzuri aliyouweka Tangu 1985 Atasemaje! Ati atawale miaka 100 kwa lipi? Kutimiza Budget less than 40% au Kununua vijindege vya Mapangaboi, na Kuminya Budget za Kila Wizara kwa zaidi ya 70%? What the Hell?

 
Wewe umeendelea kwa kipi toka ameingia?
Wewe hujaendelea kwa sababu ulikuwa ukiishi kwa kupiga dili tu za makinikia na makontena hewa nadhani. Hatuwezi lingana wala kufanana. Utaisoma namba.na bado subiri
 
Haya mambo yanaandaliwa taratibu mwisho wa siku watu watang'ang'ania madarakani,
Na wanaojifanya wanaandamana ni uvccm
 
Mimi nafikiri tupunguze Mihemko ya kisiasa hakuna ambaye hamuungi mkono Raisi wetu kwa kile anachokifanya ni Raisi aliyethubutu naweza kusema kuliko wote ukimtoa baba wa Taifa katika kufanya Maamuzi magumu kwa manufaa ya Taifa! Ila nafikiri apewe nafasi afanye kazi zake bila pressure kutoka pembeni,Raisi ndio kwanza ana miaka 2 kazini na 8 ya kwenda tayari watu wameshaanza kufikiria kubadili katiba ili Aongoze sijui eti milele?Hata yeye akiwasikia atawashangaaa at least Basi angekuwa amebakiza miaka 2 na Matokeo ya kazi yake yapo wazi hapo Sawa ,kwa sasa ndio kwanza yupo kwenye kipindi cha kuinyoosha nchi na mifumo yake,Hii mihemuko ya kisiasa tunayoianzisha inaweza kuingilia maamuzi na utendaji Raisi kibinadamu!Jamani kuongoza nchi si kazi rahisi kama wengine tunavyofikiri wewe kuwa ndio msemaji na Muamuzi wa mwisho kabisa wa Mustakabali wa maisha wa watanzania Milioni zaidi ya 40 inachosha ,kwa wale waliowahi kuongoza hata taasisi Fulani watanielewa ,maana pale Ikulu Mheshimiwa ana ratiba tight nafikiri hata usingizi ni kwa masaa kama binadamu anahitaji na yeye ikifika muda Fulani apumzike acheze na wajukuu na aangalie yale alioyofanya katika kipindi chake na aingie kwenye historia ya Taifa kwa heshima.
 
Huo ni uchochezi mkubwa sana. Ila wakiandamana wanaotaka akae madarakani muhula mmoja utasikia balaa lake.
 
Mambo mengi sanaa. La mwisho kabisa gari yangu iliyokuwa inadaiwa road licence ya milioni tatu na nusu sasa iko barabarani inapiga kazi. Sema lingine
Kwa gari lako bovu huoni unaongeza gharama ya kila unachonunua huoni unaongeza gharama ya maisha ambayo in mean time itazidi hiyo ya kurudisha mkokoteni barabarani
 
Wewe hujaendelea kwa sababu ulikuwa ukiishi kwa kupiga dili tu za makinikia na makontena hewa nadhani. Hatuwezi lingana wala kufanana. Utaisoma namba.na bado subiri
Mi sijaisoma namba hata moja na sitegemei tatizo ni hali ya wanaoandamana ni mbovu na siku zinavyoendelea inazidi kuwa mbovu wakija kupata akili tayari wako utumwani
 
Back
Top Bottom