Mimi nafikiri tupunguze Mihemko ya kisiasa hakuna ambaye hamuungi mkono Raisi wetu kwa kile anachokifanya ni Raisi aliyethubutu naweza kusema kuliko wote ukimtoa baba wa Taifa katika kufanya Maamuzi magumu kwa manufaa ya Taifa! Ila nafikiri apewe nafasi afanye kazi zake bila pressure kutoka pembeni,Raisi ndio kwanza ana miaka 2 kazini na 8 ya kwenda tayari watu wameshaanza kufikiria kubadili katiba ili Aongoze sijui eti milele?Hata yeye akiwasikia atawashangaaa at least Basi angekuwa amebakiza miaka 2 na Matokeo ya kazi yake yapo wazi hapo Sawa ,kwa sasa ndio kwanza yupo kwenye kipindi cha kuinyoosha nchi na mifumo yake,Hii mihemuko ya kisiasa tunayoianzisha inaweza kuingilia maamuzi na utendaji Raisi kibinadamu!Jamani kuongoza nchi si kazi rahisi kama wengine tunavyofikiri wewe kuwa ndio msemaji na Muamuzi wa mwisho kabisa wa Mustakabali wa maisha wa watanzania Milioni zaidi ya 40 inachosha ,kwa wale waliowahi kuongoza hata taasisi Fulani watanielewa ,maana pale Ikulu Mheshimiwa ana ratiba tight nafikiri hata usingizi ni kwa masaa kama binadamu anahitaji na yeye ikifika muda Fulani apumzike acheze na wajukuu na aangalie yale alioyofanya katika kipindi chake na aingie kwenye historia ya Taifa kwa heshima.