Wananchi Mara waandamana kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli

Wananchi Mara waandamana kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli

anataka kuwa Rais wa maisha?
ni kweli miaka 10 haimtoshi?
Umenikumbusha kanghwimbo ka mchakamchaka enzi niliwa puraimari skul...Banda wa Malawi, katuvalia ngozi ya Simba, kututishia Watanzania, hatujali. Hatujali. Banda alijiita Ngwanzi. Raisi wa maisha....
 
Rafiki yake wa karibu (Paul Kagame) alianza hivi hivi. Sasa ameibomoa katiba ya Rwanda na kukiondoa kifungu kilichohusu ukomo wa madaraka ya urais na sasa anafanana na mzee Mugabe. Huyu dereva wa lori ndiko anakoelekea. Kama tutaamua kumwachia Lissu pekee awe mkosoaji wake, tutajikuta tumeshafika Kigali mapemaaaa.
 
Hayo ni yako tu lkn wananchi tulio wengi tunamsapoti Raisi wetu Magufuli na tunahitaji atawale milele Wanaompinga Magufuli ni watu wavivu wezi wahujumu uchumi
Acheni kukufuru. Anayetawala milele , ni yule asiyekuwa na mwanzo, wala mwisho.(aliyeumba mbinguni na nchi.)
 
Hilo haliwezekana labda atumie mbinu za Jean-Bedel-Bokassa.



Kuna jirani yangu aliwahi kunaambia "wazee wengi mawazo yao yalishavunda hivyo itabidi wafe kwanza Nadhani Tanzania Mpya itapatikana"


Wazee asilimia kubwa wapo upande wa kijani kibichi,ukiwauliza kuhusu mheshimiwa wanakwambia huyu ni Nyerere wa pili Jamani haya sinimaajabu..?

Na hili la kuendelea kwa uongozi wa bwana huyu wanaliunga mkono.
 
Hata FDR ali-serve 3 terms USA tofauti na utamaduni wa mihula miwili miwili uliokuwa umewekwa na watangulizi wake(though sheria ya ukomo haikuwepo kipindi hicho ilikuwa utamaduni tu) na moja ya sababu ya kufanya hivyo inasemwa ni yeye kuamini ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kuitoa US kwenye Great Depresion.

Kama Magu akiona inafaa ataitisha kura ya maoni tu kama Kagame na watu wataamua wenyewe.

Katiba wala siyo msahafu.
 
Kagameism inatunyemelea. Huu uchafu unaoendelea kwa kupangwa pangwa haufai na ni wa kupingwa kwa nguvu zote.
 
Wewe peke yako ndo unamhitaji atawale milele..
hata akibadili katiba kuna kifo hataweza kukikwepa milele
rais wetu ana afya madhubutu bado yupoyupo sana,
anaweza kutawala hata miaka 40 bila tabu yeyote ile..

hapa ni kazi tuu..
 
Wewe peke yako ndo unamhitaji atawale milele..
hata akibadili katiba kuna kifo hataweza kukikwepa milele
rais wetu ana afya madhubutu bado yupoyupo sana,
anaweza kutawala hata miaka 40 bila tabu yeyote ile..

hapa ni kazi tuu..
 
Semina ya Kagame ilimuingia vizuri...
Na tutaambiwa tu tulirekebishe likatiba letu...
 
Hii ni mipango michafu inayopangwa na huyu baba mwenye jeuri ya maneno na matendo.Anajitengenezea umaarufu kama walivyofanya role models wake akina Nkurunzinza na Kagame. Jambo hili lipingwe kwa nguvu zote na kila mpenda demokrasia
 
Habar wakuu,amani iwe juu yenu
Wananchi mkoa wa Mara kijiji cha Nyamuswa wakiongozwa na wazir mkuu mstaafu jaji Sinde Warioba wameeandamana na kuweka mkutano kwa lengo la kumpongeza rais Magufuli kwa kusimamia rasilimali za taifa ipasavyo..wananchi hao walienda mbali zaid kwa kubeba mabango yanayomtaka rais Maguful aongoze miaka 100!

My take:Hata Rwanda walianza hivi hivi chondechonde watz wenzangu tuwe makini kuna harufu ya ukagame inanukia,
[emoji19] [emoji19] [emoji37]
 
Mimi pia na kundi language zaidi ya watu ni tunataka kuandamana kupinga magufuli ajiudhulu kwani he tutakubaliwa?
 
Kuna watu wanaweza kubeza hali inayoendelea na kuichukulia poa! Maigizo mnayoyaona ya wanancho katika mikoa mbalimbali eti wanaandamana kudai Rais aongoze miaka mia .............. siyo kwa bahati mbaya!

natabiri kitakachofuata ni Muswada Wa mabadiliko kupelekwa bungeni ili kubadilisha vifungu vya katiba vitakavyompa Fursa Rais Wa sasa kuongezewa muda

time will tell
 
Hana lolote,mbona hapatakalika.Yaani katiba ya nchi ivunjwe hivihivi pakubwa hivyo tumtazame tu!?.Acha avunje vile vidogovidogo Ila kwenye miaka ya kuongoza asahau.

Na hao waropokaji tulishawazoea.Walisema kwa Mkapa,wakaja kwa JK na wimbo wao huoho wa kuongezewa miaka.Na leo tena wamerejea,tutawakomesha!!
 
kwenye vyombo vya habari siku hizi bila kumtaja magu habari haijaisha...hata kama habari yenyewe kiuhalisia haimuhusu kabisa...mfano
" wananchi wilayani kilwa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji. wakizungumza na kituo hiki wananchi hao walisema wanashindwa kwenda sambamba na kauli ya muheshimiwa jpm ya hapa kazi tu""
ilimradi wamtaje tu bwana mkubwa
 
Back
Top Bottom