Umenena vema. Hata ue utaratibu wa kuchoma vibaka ulianza hivi hivi. Kabla yake hakuna kibaka aliyewahi kuchomwa. Raia kila walipomkamata kibaka walimpeleka polisi, lakini ipolisi badala ya kumchukulia hatua za kisheria kibaka, walimdai peßa kibaka, akishawapa, walimwachia. Kesho yake wananchi wanamwona kibaka mtaani anatamba. Ikatojea tukio moja tu Dar, Wananchi wakamchoma moto kibaka. Polisi wakatangaza kuwa wananchi wenye hasira kali wamemchoma moto kibaka. Habari zikasikika nchi nzima, na huo ukageuka kuwa ndio utaratibu wa kushughulikia vibaka.
Na hata hii hali ya sasa, taratibu, polisi wasiofuata utaratibu wa kuwakamata watuhumiwa, wanaweza kuishia kuchomwa moto na wananchi, wakichukiliwa kuwa wanamteka mtuhumiwa.
Polisi lazima wabadilike, wafuate utaratibu. Wasipobadilika kwa hiari, watabadilishwa kwa nguvu, na kufikua huko kuna gharama watailipa.