Wananchi Mwanza walalamika vigogo kupendelewa viwanja

😄😄 Luchelele Kule karibu na jembe ni jembe mtu ukipata kiwanja karibu na ziwani pako poa kishenzi,tatizo Ni barabara tu sijui Kama zineshatengenezwa.
Nilimsikia meya akizungumzia barabara ya luchelele, buhongwa-kishiri pamoja na mahina adi nile perch nyakato zitapigwa lami kuanzia mwaka huu wa fedha na alisema hayo alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya mawe kutoka ndama igoma adi mhandu shule ya primary ya samia suluhu.
 
Karibu sana mkuu, japo kuna wananchi wanataka viwanja hapo isamilo kuweka nyumba video nasi tuna mshukuru mkurugenzi wa jiji kuwapuuzia wananchi wanaotaka kuharibu mandhari ya jiji la Mwanza kwa kuuza viwanja kwa walamba asali tu🙏🙏🙏🙏
Hahah kwa kweli mkuu mimi Sina nilichoshangaa kwa kuona majina hayo ya wakuu,maeneo ya wanyonge hua yanajulikana tu waende huko wasije kuchafua mji kwa makazi duni.Hivi mkuu Kule mji mwema panahesabika Kama Isamilo au kwenyewe kunajitegemea?
 
Nilimsikia meya akizungumzia barabara ya luchelele, buhongwa-kishiri pamoja na mahina adi nile perch nyakato zitapigwa lami kuanzia mwaka huu wa fedha na alisema hayo alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya mawe kutoka ndama igoma adi mhandu shule ya primary ya samia suluhu.
Duh wakifanya hivyo ntatafuta kiwanja karibu na ziwani,Mwz napakubali kishenzi.🙏🙏 Mkuu.
 
Hahah kwa kweli mkuu mimi Sina nilichoshangaa kwa kuona majina hayo ya wakuu,maeneo ya wanyonge hua yanajulikana tu waende huko wasije kuchafua mji kwa makazi duni.Hivi mkuu Kule mji mwema panahesabika Kama Isamilo au kwenyewe kunajitegemea?
Naona ipo kata ya kitangiri ni sehemu ya kilimahewa.
 
Masuala ya kila jambo , wananchi wanalalamika huu ni ushamba sasa. ....japo pia nakubali kuna sabotage inafanyika lakin ifike wakati kila mwananchi apambane na uwezo wake .... maeneo kama isamilo,hata unguja , mirongo na pamba ni sura ya mji ,kuweka makazi ordinary ni kuharibu mji... nadhani ordinary people tusogeee luchelele , Kishiri au Mahina huko kikubwa watuwekee miundombinu mizuri
 
Duh wakifanya hivyo ntatafuta kiwanja karibu na ziwani,Mwz napakubali kishenzi.[emoji120][emoji120] Mkuu.
Kuna viwanja bei Chee beach front Kayenze , vinauzwa na manispaa changamkia fursa... huko nako vigogo wanakimbilia , maana nilimskia mkuu wa mkoa anapapigia debe
 
Baadhi ya wananchi walioomba kuuziwa viwanja eneo la Luchelele na Isamilo, jijini Mwanza, wamelalamika kukosa viwanja hivyo na kudai viongozi wa serikali na wabunge kuviwahi.

Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilitangaza kuuza viwanja hivyo na kuwataka wanaovitaka kuchukua fomu kuanzia Juni 2 hadi 6, 2021.

Wakizungumza na gazeti hili, walidai waliomba viwanja hivyo baada ya kujaza fomu na kukamilisha malipo ya maombi ya Sh. 20,000, lakini orodha iliyotoka ina majina ya vigogo.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kuwekwa kwenye tovuti yao ina orodha ya watu 427 waliopata eneo la Luchelele na 39 Isamilo.

Majina ya vigogo yalijitokeza kwenye viwanja vya Isamilo ni ya Spika wa Bunge Tulia Akson, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Alphayo Kidata, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mery Masanja.

Wengine ni Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Seleman Yahaya na Meya wa Jiji hilo, Sima Costantine Sima na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike.

Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, Michael Magufuli na Mkuu wa Mkoa mstaafu, Said Meck Sadik, ambao wengi wamepewa viwanja eneo la Isamilo ambalo lipo katikati ya Jiji la Mwanza.

Fedha za kuchukua fomu zilikusanywa na Jiji la Mwanza huku wananchi wa kawaida wakijitokeza kulipia ili waweze kupata viwanja vya makazi na biashara.

Kwa mujibu wa tangazo hilo la kuwapatia viwanja vigogo hao, walitakiwa kufika ofisi za jiji kuchukua ankara ya malipo ili wakavilipie.

Mmoja wa wananchi walioomba kununua viwanja hivyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alidai alilipia benki Sh. 20,000 kwa ajili ya kuomba kiwanja eneo la Luchelele.

Vilevile, tangazo lililotolewa kwa wananchi wakati wa kutangaza kuuza viwanga hivyo, Luchelele mita moja ya mraba ilikuwa ikiuzwa Sh. 5,000 kwa viwanja vya makazi. Eneo la Isamilo mita moja ya mraba ilikuwa ikiuzwa Sh. 25,000.

Katika maeneo hayo mawili pia alisema kulikuwa na viwanja kwa ajili ya makazi na biashara.

Tangazo la Jiji la Mwanza lilisema watu waliopatiwa viwanja hivyo walitakiwa kwenda kuchukua ankara za malipo kuanzia Juni 23 hadi Juni 30, 2021.

Aidha, tangazo hilo ambalo lipo kwenye tovuti hiyo, lilisisitiza kuwa mtu yeyote atakayeshindwa kuzingatia muda huo atanyang'anywa kiwanja na kumpatia mtu mwingine.

Alipoulizwa kuhusu vigogo hao kupatiwa viwanja, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Seleman Yahaya alisema amtumie ujumbe mfupi wa simu na kisha kukata simu.

Hata hivyo, ujumbe huo haukujibiwa.

Chanzo: NIPASHE
Bora hata wanapata fursa ya kulalamika,hapo awali ulikuwa huwezi kulalamika popote..

Wahusika chukueni hatua za kinidhamu kwa waliohusika.
 
Hawana hata aibu,Rais Samia mambo haya ndio yanakuchafua..

Fukuza huyo DED na batilisha huo mchakato.
 
Kuna viwanja bei Chee beach front Kayenze , vinauzwa na manispaa changamkia fursa... huko nako vigogo wanakimbilia , maana nilimskia mkuu wa mkoa anapapigia debe
Aisee nashukuru sana kwa hii taarifa mkuu,nitaishughulikia as soon as possible.🙏🙏
 
Bora hata wanapata fursa ya kulalamika,hapo awali ulikuwa huwezi kulalamika popote..

Wahusika chukueni hatua za kinidhamu kwa waliohusika.
Tulia Ackson anatafuta nini lake zone? [emoji13][emoji13][emoji13]
1657871620557.png
 
Back
Top Bottom