Wananchi Mwanza walalamika vigogo kupendelewa viwanja

Wananchi Mwanza walalamika vigogo kupendelewa viwanja

Unasubiria hela ya kukopeshwa wakati walamba asali wanaipata ndani ya siku moja tena ikiwa ni kama kifuta jashoo🤣🤣🤣🤣
Mlamba asali yeye ananyanyua tu simu na kumpigia gabachori mkwepa kodi, haloo hebu niingizie bilioni kuna kaplot nakataka.
 
Baadhi ya wananchi walioomba kuuziwa viwanja eneo la Luchelele na Isamilo, jijini Mwanza, wamelalamika kukosa viwanja hivyo na kudai viongozi wa serikali na wabunge kuviwahi.

Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilitangaza kuuza viwanja hivyo na kuwataka wanaovitaka kuchukua fomu kuanzia Juni 2 hadi 6, 2021.

Wakizungumza na gazeti hili, walidai waliomba viwanja hivyo baada ya kujaza fomu na kukamilisha malipo ya maombi ya Sh. 20,000, lakini orodha iliyotoka ina majina ya vigogo.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kuwekwa kwenye tovuti yao ina orodha ya watu 427 waliopata eneo la Luchelele na 39 Isamilo.

Majina ya vigogo yalijitokeza kwenye viwanja vya Isamilo ni ya Spika wa Bunge Tulia Akson, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Alphayo Kidata, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mery Masanja.

Wengine ni Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Seleman Yahaya na Meya wa Jiji hilo, Sima Costantine Sima na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike.

Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, Michael Magufuli na Mkuu wa Mkoa mstaafu, Said Meck Sadik, ambao wengi wamepewa viwanja eneo la Isamilo ambalo lipo katikati ya Jiji la Mwanza.

Fedha za kuchukua fomu zilikusanywa na Jiji la Mwanza huku wananchi wa kawaida wakijitokeza kulipia ili waweze kupata viwanja vya makazi na biashara.

Kwa mujibu wa tangazo hilo la kuwapatia viwanja vigogo hao, walitakiwa kufika ofisi za jiji kuchukua ankara ya malipo ili wakavilipie.

Mmoja wa wananchi walioomba kununua viwanja hivyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alidai alilipia benki Sh. 20,000 kwa ajili ya kuomba kiwanja eneo la Luchelele.

Vilevile, tangazo lililotolewa kwa wananchi wakati wa kutangaza kuuza viwanga hivyo, Luchelele mita moja ya mraba ilikuwa ikiuzwa Sh. 5,000 kwa viwanja vya makazi. Eneo la Isamilo mita moja ya mraba ilikuwa ikiuzwa Sh. 25,000.

Katika maeneo hayo mawili pia alisema kulikuwa na viwanja kwa ajili ya makazi na biashara.

Tangazo la Jiji la Mwanza lilisema watu waliopatiwa viwanja hivyo walitakiwa kwenda kuchukua ankara za malipo kuanzia Juni 23 hadi Juni 30, 2021.

Aidha, tangazo hilo ambalo lipo kwenye tovuti hiyo, lilisisitiza kuwa mtu yeyote atakayeshindwa kuzingatia muda huo atanyang'anywa kiwanja na kumpatia mtu mwingine.

Alipoulizwa kuhusu vigogo hao kupatiwa viwanja, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Seleman Yahaya alisema amtumie ujumbe mfupi wa simu na kisha kukata simu.

Hata hivyo, ujumbe huo haukujibiwa.

Chanzo: NIPASHE
Hawa wanaolalamika wantaka kutuletea dhahama kama ya yule mzee Magagnga wa Arusha aliyevunja mapagale yake eti yenye thamani ya milioni 200, pale chenye thamani ni ardhi kuwa mjini na sio yale mapagale,sasa hawa wanaotaka Isamilo wanataka wawekeze kwenye mapagale ya milioni 10 halafu baadae watakuja kudai nyumba zao zina thamani za mamilioni,kumbe chenye thamani ni ardhi na si mapagale, ila nae spuka kukimbilia Mwanza na kutaka kutuacha solemba sisi watu wa Mwanjelwa ndio nini?
 
Mbona tulia hajanunua njombe au njombe sio mji[emoji16][emoji16]
Wewe ni kiazi cha Hungumalwa..Hakuna kiongozi hana ardhi ya miti na Parachuchi Njombe..

Kumbuka nyie maskini mnatakiwa kuhama kule milimani Ili kupisha wawekezaji ambao ndio hao kina Tulia.
 
Back
Top Bottom