TheDreamer Thebeliever
JF-Expert Member
- Feb 26, 2018
- 2,490
- 3,584
Habari wadau!
Hali sasa imekuwa mbaya sana, wananchi wamekuwa wakitapeliwa maeneo yao kupitia hawa wawekezaji ambao kipindi cha JK walisumbua sana lakini alipoingia madarakani Magufuli walijificha kama hawapo na wakatelekeza maeneo yao kama hawayajui.
Ndio Rais Samia Hassan ameruhusu wawekezaji lakini wawekezaji wanapaswa kufuata sheria katika utwaaji ardhi, sio kuwarubuni wananchi kwa kutumia mamlaka au kutumia udhaifu wa sheria kupora ardhi ya wananchi.
Natambua makampuni mengi tunayoyaona ya warabu, lakini uhalisia ni makampuni ya viongozi na wengine ni wastaafu hata wa ngazi kubwa serikalini.
Muwekezaji anakuja anawadanganya wananchi wampatie ardhi la sivyo makazi yao yatabomolewa kwa vile yeye ni mjukuu au ndugu wa kiongozi anaendesha biashara ya familia,wakati anajua kabisa kuna sheria ya utwaaji ardhi ambayo anapaswa kuifuata katika kulipa fidia pia kutoa notisi inayostahiki lakini anatengeneza mazingira ya utapeli na rushwa katika jamii hii haikubaliki kabisa.
Akifanikiwa kupata kipande cha ardhi kwa wananchi wajinga wachache anamwamwaga kifusi ili kuharibu mazingira yasikarike kwa wale ambao hawaja kubali kumpatia ardhi kwa matwakwa yake.
Mwekezaji anatumia tools zote ikiwamo serikali za mitaa na madiwani mpaka mda mwngine halmashauri kuhalalisha ,uhaini wake hii ni hatari sana ndio maana migogoro ya ardhi Tanzania haitokwisha.
Tunazijua vizuri kampuni hizi na wamiliki wake pia tunawajua ,wengine ni waZanzibar japo wamepata nafasi katika Serikali ya Tanzania lakini si vizuri kuwatendea vibaya waTanganyika .
Hata kama wao wakubwa wa hizo kampuni hawajui nini kinachoendelea ila wanapaswa kujua kwamba wanachokifanya si sahihi hata kama wanafanya kwa watu ambao ni masikini na wengine hawajui haki zao.
Tukumbuke utajiri mwisho hapa hapa duniani, mbinguni hakuna vyeo, nyazifa wala mamlaka. Mbinguni hautotambulika kwamba ulikuwa rais, mbunge, diwani au mwenyekiti wa kijiji ardhi hii hii unayowatapeli wananchi ndio itakumeza na kukubana kwa mateso pindi utakapoingia kaburini siku yako ikifika.