Wananchi tumeanza kumkumbuka Magufuli. Wananchi wanatapeliwa viwanja na maeneo yao kwa watu wanaojiita Wawekezaji

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau!

Hali sasa imekuwa mbaya sana, wananchi wamekuwa wakitapeliwa maeneo yao kupitia hawa wawekezaji ambao kipindi cha JK walisumbua sana lakini alipoingia madarakani Magufuli walijificha kama hawapo na wakatelekeza maeneo yao kama hawayajui.

Ndio Rais Samia Hassan ameruhusu wawekezaji lakini wawekezaji wanapaswa kufuata sheria katika utwaaji ardhi, sio kuwarubuni wananchi kwa kutumia mamlaka au kutumia udhaifu wa sheria kupora ardhi ya wananchi.

Natambua makampuni mengi tunayoyaona ya warabu, lakini uhalisia ni makampuni ya viongozi na wengine ni wastaafu hata wa ngazi kubwa serikalini.

Muwekezaji anakuja anawadanganya wananchi wampatie ardhi la sivyo makazi yao yatabomolewa kwa vile yeye ni mjukuu au ndugu wa kiongozi anaendesha biashara ya familia,wakati anajua kabisa kuna sheria ya utwaaji ardhi ambayo anapaswa kuifuata katika kulipa fidia pia kutoa notisi inayostahiki lakini anatengeneza mazingira ya utapeli na rushwa katika jamii hii haikubaliki kabisa.

Akifanikiwa kupata kipande cha ardhi kwa wananchi wajinga wachache anamwamwaga kifusi ili kuharibu mazingira yasikarike kwa wale ambao hawaja kubali kumpatia ardhi kwa matwakwa yake.

Mwekezaji anatumia tools zote ikiwamo serikali za mitaa na madiwani mpaka mda mwngine halmashauri kuhalalisha ,uhaini wake hii ni hatari sana ndio maana migogoro ya ardhi Tanzania haitokwisha.

Tunazijua vizuri kampuni hizi na wamiliki wake pia tunawajua ,wengine ni waZanzibar japo wamepata nafasi katika Serikali ya Tanzania lakini si vizuri kuwatendea vibaya waTanganyika .

Hata kama wao wakubwa wa hizo kampuni hawajui nini kinachoendelea ila wanapaswa kujua kwamba wanachokifanya si sahihi hata kama wanafanya kwa watu ambao ni masikini na wengine hawajui haki zao.

Tukumbuke utajiri mwisho hapa hapa duniani, mbinguni hakuna vyeo, nyazifa wala mamlaka. Mbinguni hautotambulika kwamba ulikuwa rais, mbunge, diwani au mwenyekiti wa kijiji ardhi hii hii unayowatapeli wananchi ndio itakumeza na kukubana kwa mateso pindi utakapoingia kaburini siku yako ikifika.
 
Haya mambo ya utapeli wa ardhi hata wakati wa Magufuli yaliendelea kuwepo, binafsi nimeingia kwenye mgogoro wa ardhi na mtu mimi nikiwa na hati miliki na wakati tukiendelea na shauri mahakamani kumetokea mambo mengi ya ovyo huko wizarani (sitaki niingie ndani zaidi maana kesi bado inaendelea) yaani kwa kweli ishu ya utapeli wa ardhi bado ni ngumu sana.
 
Mkuu mbona umeeleza jumla jumla,
Eleza kwa kina namna ulivyo/mlivyoporwa ardhi ili jamii ikusaidie angalau kwa ushauri.
 
Sema mmeanza mkumbuka wendazake , maana mlisha muona ni Mungu wenu ,Sio wate msitulazimishe, mwenda zake hakuna alichofanya kwangu tofauti na kunipunguzia mzunguko wa pesa yangu , ningekua mbali Sana japo sijafilisika
 
Kila mwanadamu ana mapungufu yake lakini kwenye swala la kusimamia wananchi wasipokonye ardhi alikuwa shujaa hasiyepingika,wewe ulipunguziwa mzunguko lakini kipindi hicho hicho nilijenga nyumba yangu.
 
Habari wadau..!
Hali sasa imekuwa mbaya sana ,wananchi wamekuwa wakitapeliwa maeneo yao kupitia hawa wawekezaji ambao kipindi cha JK walisumbua sana lakini alipoingia madarakani Magufuli walijificha kama hawapo na wakatelekeza maeneo yao kama hawayajui...
Sema mmeanza mkumbuka wendazake , maana mlisha muona ni Mungu wenu , bina
Kila mwanadamu ana mapungufu yake lakini kwenye swala la kusimamia wananchi wasipokonye ardhi alikuwa shujaa hasiyepingika,wewe ulipunguziwa mzunguko lakini kipindi hicho hicho nilijenga nyumba yangu.
Ndio ulijenga nyumba, ila jua pia uliwabana mbavu mafundi wako mpaka wakakoma , maana KAZI zilisha kua Chache, so fundi anakwambia ukweli kwamba gharama ya kupiga bati tafadhali nipe ml 4 tokana na gharama ya bati na ukubwa, na mchoro wa nyumba yako , wewe unasema una mil MOJA, hataki Basi maana unajua atakubali kisa vyuma vimekaza,

Maisha gani ya ajabu, Sasa angalia Iyo nyumba YAKO vizuri usije kuta hata quality ipo chini, maana ukimlipa fundi vizuri ,utapata ushauri mzuri ,na quality Safi, kujenga sio tatizo Mkuu ila je imejenga kistandard ajalishi ni vyumba viwili ,
 
Habari wadau!

Hali sasa imekuwa mbaya sana, wananchi wamekuwa wakitapeliwa maeneo yao kupitia hawa wawekezaji ambao kipindi cha JK walisumbua sana lakini alipoingia madarakani Magufuli walijificha kama hawapo na wakatelekeza maeneo yao kama hawayajui.

Ndio Rais Samia Hassan ameruhusu wawekezaji lakini wawekezaji wanapaswa kufuata sheria katika utwaaji ardhi, sio kuwarubuni wananchi kwa kutumia mamlaka au kutumia udhaifu wa sheria kupora ardhi ya wananchi.

Natambua makampuni mengi tunayoyaona ya warabu, lakini uhalisia ni makampuni ya viongozi na wengine ni wastaafu hata wa ngazi kubwa serikalini.

Muwekezaji anakuja anawadanganya wananchi wampatie ardhi la sivyo makazi yao yatabomolewa kwa vile yeye ni mjukuu au ndugu wa kiongozi anaendesha biashara ya familia,wakati anajua kabisa kuna sheria ya utwaaji ardhi ambayo anapaswa kuifuata katika kulipa fidia pia kutoa notisi inayostahiki lakini anatengeneza mazingira ya utapeli na rushwa katika jamii hii haikubaliki kabisa.

Akifanikiwa kupata kipande cha ardhi kwa wananchi wajinga wachache anamwamwaga kifusi ili kuharibu mazingira yasikarike kwa wale ambao hawaja kubali kumpatia ardhi kwa matwakwa yake.

Mwekezaji anatumia tools zote ikiwamo serikali za mitaa na madiwani mpaka mda mwngine halmashauri kuhalalisha ,uhaini wake hii ni hatari sana ndio maana migogoro ya ardhi Tanzania haitokwisha.

Tunazijua vizuri kampuni hizi na wamiliki wake pia tunawajua ,wengine ni waZanzibar japo wamepata nafasi katika Serikali ya Tanzania lakini si vizuri kuwatendea vibaya waTanganyika .

Hata kama wao wakubwa wa hizo kampuni hawajui nini kinachoendelea ila wanapaswa kujua kwamba wanachokifanya si sahihi hata kama wanafanya kwa watu ambao ni masikini na wengine hawajui haki zao.

Tukumbuke utajiri mwisho hapa hapa duniani, mbinguni hakuna vyeo, nyazifa wala mamlaka. Mbinguni hautotambulika kwamba ulikuwa rais, mbunge, diwani au mwenyekiti wa kijiji ardhi hii hii unayowatapeli wananchi ndio itakumeza na kukubana kwa mateso pindi utakapoingia kaburini siku yako ikifika.

Unamkumbuka Magufuli wakati yeye ndio alinajisi uchaguzi na kuweka viongozi ambao hawakuchaguliwa na wananchi. Unataka kuleta sifa za kijinga wakati Magufuli ndio aliweka hao viongozi kwa maslahi yake binafsi.
 
Kila mwanadamu ana mapungufu yake lakini kwenye swala la kusimamia wananchi wasipokonye ardhi alikuwa shujaa hasiyepingika,wewe ulipunguziwa mzunguko lakini kipindi hicho hicho nilijenga nyumba yangu.

Ww si ulikuwa kwenye kundi lake la watu wasiojulikana, ulitegemea ungeacha kujenga, na sasa kumkumbuka?
 
Wahindi na waarabu wanaichezea sana Tanganyika
Tanganyika imekosa mtetezi mbaya zaidi vigogo wameungana na hawa watu kuwadhulumu watanzania
 
Back
Top Bottom