Wananchi Tumekuwa Spectators Katika Nchi Yetu – Hii Ni Dhihaka Kubwa Kwa Demokrasia Yetu!

Wananchi Tumekuwa Spectators Katika Nchi Yetu – Hii Ni Dhihaka Kubwa Kwa Demokrasia Yetu!

Joined
Dec 18, 2023
Posts
15
Reaction score
31
Kweli tumefika pabaya! Tumepunguzwa hadhi mpaka kura yetu imegeuzwa kuwa kama ritual tu ya kufurahisha watawala, bila thamani ya kweli. Wananchi tumeonekana wajinga, tumetupwa pembeni kana kwamba hatuna akili za kupambanua nani anafaa kutuongoza. Hivi kwanini kura yangu – kura yako – iwe treated kama worthless piece of paper wakati ni msingi wa sovereignty yetu? Ni kama vile social contract iliyowekwa na wanafalsafa kama Rousseau imechukuliwa na kutupwa jalalani.

Tumeachwa kama spectators ndani ya nchi yetu, tunaangalia wachache wakichezea mustakabali wetu huku wakijifanya ndio wenye monopoly of wisdom. Hii siyo demokrasia, ni dhihaka! Hii ni psychological torture, inaua matumaini ya wananchi na kuondoa kabisa imani kwenye system. Na bado wanataka tuendelee kucheka, tuendelee kuvumilia kana kwamba hatujui tunachoona? Enough is enough!

Je, sisi wananchi tutabaki kukandamizwa huku tukijifanya hatuoni? Au tutasimama na kudai kile ambacho ni chetu kwa haki? Kama kweli hii nchi ni ya wananchi, basi power must go back to the people – siyo kutekwa na wachache wenye dharau na dhihaka dhidi ya wananchi!
 
Jaji mkuu na Spika wanapata mafao ya uhakika. Hawa ni watu ambao wananguvu ya kupindua meza kama mambo hayaendi lakini sasa hivi wamekua walinda maslahi.

Wakuu wote wa vyombo vya usalama nao ni hivyo hivyo. Wananchi wamegawanyika mno.
 
Back
Top Bottom