Wananchi tuna haki kufahamu alipo Makamu wa Rais Philip Mpango

Salaam, Shalom!!

Tuliuliza Yu wapi Rais wetu?, tukajibiwa, hajambo, anachapa KAZI!!!

Hazikupita siku chache, tunaambiwa, hatunaye.😭😭

Tungejua Yu, mgonjwa ,tungemwombea, baada ya siku kadhaa, tukapokea msiba, tukazika,

Hata miaka mitatu, haijeisha, Mh Mpango naye haonekani!!

MSITUTONESHE, BADO TUNA MAUMIVU!!

TUAMBIWE MH MPANGO YU WAPI, IKIWA NI MGONJWA, TUAMBIWE TUMWOMBEE!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Amen.
 
Tuacheni uchuro, kila mtu atakufa na kifo hakifichwi...

Mbona kipindi kile alipotea alipobanwa na 'mdudu' lakini baadaye akarejea ingawa alikuwa anakohoa kohoa lakini alirejea na maisha yakaendelea...
 
Si tushaambiwa yupo ziara za nje ya nchi?
 
Hii ya kutoonekana kwenye tukio tuliloambiwa yeye ndiye mgeni rasmi, linafikirisha sana.

Kusema kuwa hatunaye, ni neno gumu kulitamka kama hakuna uhakika.

Niamini tu kuwa Mpango ni mgo jwa ila majitu yasiyo na upendo yanatudanganya kuwa ni mzima.

Kama ni mgonjwa, Yesu wa uponyaji uliyewaponya wanadamu kwa neno lako tu moja, basi kwa mapenzi yako, kwaajili ya sisi tukuombao, neno hilo likamwangukie ndugu yetu Filipo Mpango, hata aweze kurejea nyumbani akiwa hai na mwenye afya njema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…