Wananchi tuna haki kufahamu alipo Makamu wa Rais Philip Mpango

Amen
Hii ya kutoonekana kwenye tukio tuliloambiwa yeye ndiye mgeni rasmi, linafikirisha sana.

Kusema kuwa hatunaye, ni neno gumu kulitamka kama hakuna uhakika.

Niamini tu kuwa Mpango ni mgo jwa ila majitu yasiyo na upendo yanatudanganya kuwa ni mzima.

Kama ni mgonjwa, Yesu wa uponyaji uliyewaponya wanadamu kwa neno lako tu moja, basi kwa mapenzi yako, kwaajili ya sisi tukuombao, neno hilo likamwangukie ndugu yetu Filipo Mpango, hata aweze kurejea nyumbani akiwa hai na mwenye afya njema.
 
"Nimesikia habari nzito kuhusu mwamba huyu lakini siwezi kuisema hapa kama ilivyokuwa vigumu kusema ya Magufuli" - Nukuu
Sidhani hata kama wanajali hizi dukuduku za wananchi. Nimesikia habari nzito kuhusu mwamba huyu lakini siwezi kuisema hapa kama ilivyokuwa vigumu kusema ya Magufuli aliyesemekana kufariki lakini serikali ikaja kutoa taarifa baada ya wiki moja hivyo kusogeza mbele tarehe ya kifo chake.

Ngoja pia waendelee kuficha ugonjwa wa Mpango lakini kifo kitawaumbua kama kilipowaumbua kwa Magufuli. Wakati ukuta.
Mkuu TPaul, yawezekana unajua kitu fulani kinachofichwa kuhusiana na huyu mwamba. Japo kwa "codes" ebu jaribu kufunguka zaidi.

Ukisoma "between the lines" katika andiko lako, mbona linatisha!?
 
"Nimesikia habari nzito kuhusu mwamba huyu lakini siwezi kuisema hapa kama ilivyokuwa vigumu kusema ya Magufuli" - NukuuMkuu TPaul, yawezekana unajua kitu fulani kinachofichwa kuhusiana na huyu mwamba. Japo kwa "codes" ebu jaribu kufunguka zaidi.

Ukisoma "between the lines" katika andiko lako, mbona linatisha!?
Wakati ukuta. Tusubiri tutangaziwa muda mfupi ujao. Hawawezi kuficha milele.
 
Tulimpoteza Magufuli kwa sababu kuumwa hadi kuzidiwa kulifanywa National Bigly Secret ambapo wananchi hatukujulishwa iwapo anaumwa ama amezidiwa zaidi ya kustuliwa na taarifa ya kifo chake mnamo 17 March 2021...
Wasijibebeshe mzigo bila sababu. Waseme tu hali ilivyo. Kwani kuugua itakuwa yeye ni mtu wa kwanza? Wanavyofanya mambo kwa kificho wanatufanya tusiwaelewe vizuri, au tuanze kuwatilia shaka na kuto waamini.
 
Tulimpoteza Magufuli kwa sababu kuumwa hadi kuzidiwa kulifanywa National Bigly Secret ambapo wananchi hatukujulishwa iwapo anaumwa ama amezidiwa zaidi ya kustuliwa na taarifa ya kifo chake mnamo 17 March 2021.

Rais ni wa Jamhuri na anamilikiwa na wwnanchi wote bila kujali iyikadi, imani wala kabila. Nasema anamilikiwa ni kwa sababu shughuli zake zote zinamhusu kila raia awe mdogo au mkubwa kwa jinsia zote.

Rais anamilikiwa na wananchi ndo maana analindwa na wananchi na kutunzwa na kodi za wananchi. Ingawa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wanadhani wao pekee ndo wenye dhamana ya kumtunza na kumlinda Rais. Wananchi watasali kwa miungu yao, watatambika kwa mahoka wao na kadhalika ilimradi Rais aweze kufikia matarajio na matamanio yao. Wenye Mungu nap watamuombea ili awe salama na aweze kutekeleza majukumu yake vyema.

Inaelekea tukio la marehemu JPM halijatupa funzo lolote. Zimeanza tetesi kupitia wale wale walioeneza uvumi kuhusu hatma ya JPM na sasa wanamtaja Makamu wa Rais. Tetesi hizi zimeendelea kupata mwangwi mkubwa kupitia mitandao ya jamii kuhusu afya na uhai wa Makamu wa Rais.

Serikali, imeelekwa kupuuza uvumi huo kama ilivyopuuza enzi Mwendazake anapigania uhai wake vyumba vya afya. Tuliona viongozi wakubwa akiwemo Waziri Mkuu wakitoa matamko ya kubeza tetesi hizo kwa kuuaminisha Umma kwamba Rais wao anachapakazi yupo gado kabisa.

Jana, serikali ilisambaza bango mitandaoni kumuonesha Makamu wa Rais atakuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa TAWIRI unaoanza tarehe 06 Desemba 2023..... sisi tunaochoshwa na tetesi za vifo vya wakubwa tukanyenua mikono juu kumshukuru Mungu kuwa tetesi kuhusu hali ya Mhe. Mpango ni uzushi na upotofu. Lakini aliyefika mkutanoni ni mwakilishi (Mhe. Kairuki) na siyo mgeni mlengwa.

Tumepatwa na msiba wa kitaifa kule Hanang kwa kuondokewa na ndugu zetu kutokana na mafuriko makubwa. Tumeona mfariji wa Taifa ambaye ni Rais ameshajitokeza na kuaimama na wananchi wale na hata Waziri Mkuu na viongozi wengine wa Serikali wakifanya juu chini ili kuwanasua waliokwama chini ya tope zito la mlima Hanang. Lakini hatujamsikia popote Makamu wetu wa Rais akitoa pole kama ilivyo kawaida yake kwa matukio aina hii.

Kwa niaba ya Watanzania, naleta ombi kwa serikali ituondoe kizani kuhusu alipo makamu wa Rais. Hizi tetesi zinazoendelea hazina afya kwa Taifa.

Endapo kweli hatunaye na hatukutangaziwa kuumwa kwake ni wazi hatutazuiwa kuwaza kwamba serikalini kuna hila nyingi dhidi ya viongozi wa Kitaifa na hakika tutaamini kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na mamlaka zingine zina muunganiko usio na afya kwa Taifa letu.

Naomba tujulishwe
Sawa kabisa kama kuna tanzia la kitaifa tujulishwe!
 
Serikali ina utaratibu wake wa kufanya mambo yake, nadhani hata ukienda ikulu uatajibiwa hivyo.
Hili jibu linatosha.

Hata kwenye familia baba akiwa mgonjwa watoto hawawezi wakawa wa kwanza kuambiwa, na hata kama akianguka mbele ya watoto atabebwa na baadaye watoto wanaelezwa kwamba baba ni mzima kabisa na anawapa hi.
 
Tulimpoteza Magufuli kwa sababu kuumwa hadi kuzidiwa kulifanywa National Bigly Secret ambapo wananchi hatukujulishwa iwapo anaumwa ama amezidiwa zaidi ya kustuliwa na taarifa ya kifo chake mnamo 17 March 2021.

Rais ni wa Jamhuri na anamilikiwa na wwnanchi wote bila kujali iyikadi, imani wala kabila. Nasema anamilikiwa ni kwa sababu shughuli zake zote zinamhusu kila raia awe mdogo au mkubwa kwa jinsia zote.

Rais anamilikiwa na wananchi ndo maana analindwa na wananchi na kutunzwa na kodi za wananchi. Ingawa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wanadhani wao pekee ndo wenye dhamana ya kumtunza na kumlinda Rais. Wananchi watasali kwa miungu yao, watatambika kwa mahoka wao na kadhalika ilimradi Rais aweze kufikia matarajio na matamanio yao. Wenye Mungu nap watamuombea ili awe salama na aweze kutekeleza majukumu yake vyema.

Inaelekea tukio la marehemu JPM halijatupa funzo lolote. Zimeanza tetesi kupitia wale wale walioeneza uvumi kuhusu hatma ya JPM na sasa wanamtaja Makamu wa Rais. Tetesi hizi zimeendelea kupata mwangwi mkubwa kupitia mitandao ya jamii kuhusu afya na uhai wa Makamu wa Rais.

Serikali, imeelekwa kupuuza uvumi huo kama ilivyopuuza enzi Mwendazake anapigania uhai wake vyumba vya afya. Tuliona viongozi wakubwa akiwemo Waziri Mkuu wakitoa matamko ya kubeza tetesi hizo kwa kuuaminisha Umma kwamba Rais wao anachapakazi yupo gado kabisa.

Jana, serikali ilisambaza bango mitandaoni kumuonesha Makamu wa Rais atakuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa TAWIRI unaoanza tarehe 06 Desemba 2023..... sisi tunaochoshwa na tetesi za vifo vya wakubwa tukanyenua mikono juu kumshukuru Mungu kuwa tetesi kuhusu hali ya Mhe. Mpango ni uzushi na upotofu. Lakini aliyefika mkutanoni ni mwakilishi (Mhe. Kairuki) na siyo mgeni mlengwa.

Tumepatwa na msiba wa kitaifa kule Hanang kwa kuondokewa na ndugu zetu kutokana na mafuriko makubwa. Tumeona mfariji wa Taifa ambaye ni Rais ameshajitokeza na kuaimama na wananchi wale na hata Waziri Mkuu na viongozi wengine wa Serikali wakifanya juu chini ili kuwanasua waliokwama chini ya tope zito la mlima Hanang. Lakini hatujamsikia popote Makamu wetu wa Rais akitoa pole kama ilivyo kawaida yake kwa matukio aina hii.

Kwa niaba ya Watanzania, naleta ombi kwa serikali ituondoe kizani kuhusu alipo makamu wa Rais. Hizi tetesi zinazoendelea hazina afya kwa Taifa.

Endapo kweli hatunaye na hatukutangaziwa kuumwa kwake ni wazi hatutazuiwa kuwaza kwamba serikalini kuna hila nyingi dhidi ya viongozi wa Kitaifa na hakika tutaamini kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na mamlaka zingine zina muunganiko usio na afya kwa Taifa letu.

Naomba tujulishwe
Uliambiwa yupo kwenye majukum, ni swala la utulivu tu, wasije kuja na habari zingine full stop,

Sie tushikilie kauli tajwa hapo iliyotolewa , vinginevyo hataeleweka mtu, kwa sababu hata kama anaumwa ni lini Tumeona kiongozi wake amemtembelea na kumjulia hali,

Kama Rais wa nchi kubwa kama USA anaumwa na ulimwengu wote unajua kwa nini kwenye nchi za kwetu, binafsi naamini ni mzima anaendelea na shughuli zake kama tulivyotangaziwa
 
Back
Top Bottom