Wananchi tuna haki kufahamu alipo Makamu wa Rais Philip Mpango

Wananchi tuna haki kufahamu alipo Makamu wa Rais Philip Mpango

Mungu azid kumlinda makamu wetu
 

Attachments

  • 20231007_065831 (1).jpg
    20231007_065831 (1).jpg
    70.6 KB · Views: 1
......Kama Rais wa nchi kubwa kama USA anaumwa na ulimwengu wote unajua kwa nini kwenye nchi za kwetu, binafsi naamini ni mzima anaendelea na shughuli zake kama tulivyotangaziwa
Inaelekea afya za viongozi wa nchi kama zetu ni National Essential Asset. Yaani kuijua ni sawa na kutishia usalama wa nchi husika.

Tunakoelekea ama tulipo sasa siyo kuzuri na salama kama jamii yenye usawa
 
...na kwa kuongeza, anaetoa hizi taarifa ni yule yule alietoa za JPM! Sijui tutamwonaje yakitokea (ingawa hatuombi yatokee) yale ya JPM!? Hakika mimi sitmwelewa, nitahisi km tuna WM muongo haijawahi tokea. Ati yuko nje kwa majukumu...! Yasio na mwisho? Hakuna wapiga picha huko?! Hakna vyombo vy habari huko!?...nk
 
Tulimpoteza Magufuli kwa sababu kuumwa hadi kuzidiwa kulifanywa National Bigly Secret ambapo wananchi hatukujulishwa iwapo anaumwa ama amezidiwa zaidi ya kustuliwa na taarifa ya kifo chake mnamo 17 March 2021.

Rais ni wa Jamhuri ijulikane kuwa anamilikiwa na wananchi wote bila kujali itikadi, imani wala kabila. Nasema anamilikiwa ni kwa sababu shughuli zake zote zinamhusu kila raia awe mdogo au mkubwa kwa jinsia zote.

Rais anamilikiwa na wananchi ndo maana analindwa na wananchi na kutunzwa na kodi za wananchi. Ingawa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wanadhani wao pekee ndo wenye dhamana ya kumtunza na kumlinda Rais. Wananchi watasali kwa miungu yao, watatambika kwa mahoka wao na kadhalika ilimradi Rais aweze kufikia matarajio na matamanio yao. Wenye Mungu nao watamuombea ili awe salama na aweze kutekeleza majukumu yake vyema.

Inaelekea tukio la marehemu JPM halijatupa funzo lolote. Zimeanza tetesi kupitia wale wale walioeneza uvumi kuhusu hatma ya JPM na sasa wanamtaja Makamu wa Rais. Tetesi hizi zimeendelea kupata mwangwi mkubwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu afya na uhai wa Makamu wa Rais.

Serikali, imeendelea kupuuza uvumi huo kama ilivyopuuza uvumi (uliokuwa siyo uvumi) enzi Mwendazake wakati anapigania uhai wake vyumba vya afya. Tuliona viongozi wakubwa akiwemo Waziri Mkuu wakitoa matamko ya kubeza tetesi hizo kwa kuuaminisha Umma kwamba Rais wao anachapakazi yupo gado kabisa.

Jana, serikali ilisambaza bango mitandaoni kumuonesha Makamu wa Rais atakuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa TAWIRI unaoanza tarehe 06 Desemba 2023..... sisi tunaochoshwa na tetesi za vifo vya wakubwa tukanyenya mikono juu kumshukuru Mungu kuwa tetesi kuhusu hali ya Mhe. Mpango ni uzushi na upotofu. Lakini aliyefika mkutanoni ni mwakilishi (Mhe. Kairuki) na siyo mgeni mlengwa.

Tumepatwa na msiba wa kitaifa kule Hanang kwa kuondokewa na ndugu zetu kutokana na mafuriko makubwa. Tumeona mfariji wa Taifa ambaye ni Rais ameshajitokeza na kusimama na wananchi wote na hata Waziri Mkuu na viongozi wengine wa Serikali wanafanya kila linalowezekana ili kuwanasua waliokwama chini ya tope zito la mlima Hanang. Lakini hatujamsikia popote Makamu wetu wa Rais akitoa pole kama ilivyo kawaida yake kwa matukio aina hii.

Kwa niaba ya Watanzania, naleta ombi kwa serikali ituondoe kizani kuhusu alipo makamu wa Rais. Hizi tetesi zinazoendelea hazina afya kwa Taifa.

Endapo kweli hatunaye na hatukutangaziwa kuumwa kwake ni wazi hatutazuiwa kuwaza kwamba serikalini kuna hila nyingi dhidi ya viongozi wa Kitaifa na hakika tutaamini kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pamoja na mamlaka zingine zina muunganiko usio na afya kwa Taifa letu.

Naomba tujulishwe

Yupo mzima wala haumwi!
 
Sidhani hata kama wanajali hizi dukuduku za wananchi. Nimesikia habari nzito kuhusu mwamba huyu lakini siwezi kuisema hapa kama ilivyokuwa vigumu kusema ya Magufuli aliyesemekana kufariki lakini serikali ikaja kutoa taarifa baada ya wiki moja hivyo kusogeza mbele tarehe ya kifo chake.

Ngoja pia waendelee kuficha ugonjwa wa Mpango lakini kifo kitawaumbua kama kilipowaumbua kwa Magufuli. Wakati ukuta.

Acha kuleta porojo za kipumbavu na za mitaani kwa nia ya kuleta taharuki hapa! Umesikia kwa nani na ni kitu gani umesikia, kiandike hapa! Na Magufuli alifariki wiki moja kabla? Hiyo wiki moja aliyofariki asitangazwe ilikuwa inahusu nini na kwa nini Rais Samia alitangazia kifo hicho akiwa Tanga na siyo Ikulu ya Dodoma? Wacheni kutuletea habari za kuokota za redio mbao hapa!
 
Back
Top Bottom