Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sukari na nishati haijawahi mwacha mtu salamaBila ya kujali itikadi, sote wananchi tuungane ktk uzi huu kulaani kwa kauli moja uonevu wa spika dhidi ya Mpina...
Hahahah jamaa anamchukia vibaya sana 😂😂
Nasimama na utafutaji wangu wa hela!Bila ya kujali itikadi, sote wananchi tuungane ktk uzi huu kulaani kwa kauli moja uonevu wa spika dhidi ya Mpina...
Hakuna cha uonezi hapo. Alitaka tuendelee kununua sukari kwa shs 6000 plus? Anatumika tu kuwatetea wamiliki wa viwanda vya sukari waliogoma kuagiza sukari ya kuziba gap.Bila ya kujali itikadi, sote wananchi tuungane ktk uzi huu kulaani kwa kauli moja uonevu wa spika dhidi ya Mpina...
Kweli kabisa 😅Hahaha Yan ukitaka kuvurugana na Tindo toa sifa Kwa magufuli
Hofu yangu ni kuwa kama ile agenda ya DPW ilipita, sidhani kama ile kamati iliyoundwa na spika itakuja na jipya. Maana kwenye hotuba yake spika ni kama amemhukumu moja kwa moja Mpina kama mkosaji. Ila ameamua kuunda kamati kama geresha tu.Kwasababu tumeamua kukaa kimya kama wajinga, sasa wapuuzi wameamua kututawala hovyo bila aibu, inashangaza sana bunge linalojainasibu ni muwakilishi wa wananchi kumuadhibu mbunge aliyeanza kutoa taarifa kwa wananchi juu ya ufisadi wa kutisha wizara ya kilimo...
Mbona ushahidi umekamilika na vielelezo vyote. Au hujasoma hotuba ya Mpina Kwa waandishi wa Habari.Tuache ushabiki, je amepeleka ushahidi kama ambavyo ilihitajika? Kumbukeni hii sio awamu ya kuropoka ropoka bila data na supporting documents. Siasa za uzushi hazina nafasi
Mkuu huyo Mpina akienda front seat utamsahau .Bila ya kujali itikadi, sote wananchi tuungane katika uzi huu kulaani kwa kauli moja uonevu wa spika dhidi ya Mpina.
Shime watanzania kila mtu aandike katika uzi huu maneno yafuatayo:
"NASIMAMA NA MPINA",
Hii itasaidia kumtia moyo Mpina na kumshinikiza spika Tulia kuachana na njama zake za kumnyamazisha.
NB: Huu siyo uzi wa kupiga stori, andika hayo maneno matatu tu. Comment ya kwanza nimeonesha mfano.
PIA SOMA
- Spika Tulia amburuza Luhanga Mpina Kamati ya maadili
- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge
- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya
- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
Ametoa ushahidi dhidi ya waziri Bashe Kwa waandishi wa habari kabla hajaukabidhi kwenye Ofisi ya Spika wa bunge.Amefanyaje kwani mpina hadi huyo spika amjie juu
Hata saa mbovu kuna wakati inakuwa sahihi.Unasimama na shetani aliyechoma nyavu za wavuvi wa nchi hii na kuwatia umaskini? Mnaomsapoti Mpina hamna tofauti na vijana wapumbavu wa Liberia waliomchagua dikteta Charles Taylor aliyeua wazazi wao. Wakati wa kampeni walikuwa na msemo wao wa "He killed My Ma, He killed my Pa.... I'll Vote for him"
Mpina alikuwa ni miongoni mwa viongozi makatili wa awamu ya 5 waliofanya ushenzi mwingi sana kwa wananchi wasio na hatia. Hana political legitimacy ya kunyooshea mtu kidole.