Wananchi tunamsaidiaje Mpina?
Taarifa ya Mpina ni ya hakika na inapaswa kuungwa mkono, lakini Mimi huwa siungi mkono watu walioshiriki dhuluma kipindi cha dhalimu magu. Hivyo aungwe mkono na wananchi, lakini mimi na watu wa dhuluma hapana.
Ni ufinyu wa mawazo kuwa subjective kwenye Kila hoja.
 
Bila ya kujali itikadi, sote wananchi tuungane katika uzi huu kulaani kwa kauli moja uonevu wa spika dhidi ya Mpina.

Shime watanzania kila mtu aandike katika uzi huu maneno yafuatayo:
"NASIMAMA NA MPINA",

Hii itasaidia kumtia moyo Mpina na kumshinikiza spika Tulia kuachana na njama zake za kumnyamazisha.

NB: Huu siyo uzi wa kupiga stori, andika hayo maneno matatu tu. Comment ya kwanza nimeonesha mfano.

PIA SOMA
- Spika Tulia amburuza Luhanga Mpina Kamati ya maadili

- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge

- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya

- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
Aseme kwanza malizetu za uvuvi alizo kwapua kwakisingizio cha uvuvi haram zipowapi atarudisha lini? Ndio nitamuelewa shetani hawezi kuwa naimani kaziyake nikupotosha tu alafu mkumbuke magu alimwita kichaa ,anaemuamini kichaa nayeye ni ............
 
Tuache ushabiki, je amepeleka ushahidi kama ambavyo ilihitajika? Kumbukeni hii sio awamu ya kuropoka ropoka bila data na supporting documents. Siasa za uzushi hazina nafasi
Ungetulia ufuatilie mjadala tu wewe.

Maana unaonesha wazi kuwa umetoka usingizini na kukuta muziki unaoishilizia na kuishia kutikisa tako moja tu na ngoma kukatika.

Kwa taarifa yako ni kuwa kila unaosemekana "uongo wa Bashe" umethibitishwa kwa nyaraka tena toka mamlaka halali za kiserikali mf. BRELA, TRA, Benki nk

Wewe labda ungeshauri watu wasubiri Ili kujua nyaraka za ushahidi zilizowasilishwa ni halali/genuine au ni za kughushi Ili kum - incriminate Waziri Bashe na Mwigulu na viongozi wengine.

Ikiwa hivi, kwamba nyaraka si halisi, basi huo utakuwa mjadala mwingine.

LAKINI: Kwa jinsi mambo yalivyo hadi kiasi cha Spika Dr. Tulia Jackson kupanic na kukasirika hivyo, ni wazi kuwa Luhaga Mpina ameishika serikali pabaya.!
 
Bila ya kujali itikadi, sote wananchi tuungane katika uzi huu kulaani kwa kauli moja uonevu wa spika dhidi ya Mpina.

Shime watanzania kila mtu aandike katika uzi huu maneno yafuatayo:
"NASIMAMA NA MPINA",

Hii itasaidia kumtia moyo Mpina na kumshinikiza spika Tulia kuachana na njama zake za kumnyamazisha.

NB: Huu siyo uzi wa kupiga stori, andika hayo maneno matatu tu. Comment ya kwanza nimeonesha mfano.

PIA SOMA
- Spika Tulia amburuza Luhanga Mpina Kamati ya maadili

- Luhanga Mpina apewa siku 10 na Spika kuleta ushahidi wa Bashe kulidanganya Bunge

- Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya

- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
Tunataka sukari kwa namna yeyote inayowezekana ili iteremke kutoka Tsh 10,000 hadi Tsh 3,000 tuliyozoea. Huyu kichaa wa Magufuli ana ajenda zake za kuwa nje ya baraza la mawaziri.
 
Wananchi ndio tunaua hili Taifa!

Wanasiasa wanatawala kulingana na namna raia wake walivyo, Kama raia wake ni mambumbu, au maskini, au walioelimika, au matajiri au wadai haki, au malofa n.k

Hasara ya wanasiasa aina ya Mpina au Tundulisu na wengineo ni kupigania haki ya raia malofa

Faida ya wanasiasa wabadhirifu ni kutawala raia malofa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ni ufinyu wa mawazo kuwa subjective kwenye Kila hoja.
Ni hivi watu wa aina ya Mpina huwa wanabadilika kutokana na mlo, ninaweza kumuunga mkono Leo kwa hoja hii, nikampa millage ya kupata madaraka, kisha akarudia yale yale ya ulevi wa madaraka. Nakubali kuwa taarifa yake ya sasa ni ya msingi, lakini huwa siungi mkono watu ambao sio wasimamia haki. Ukitaka muunge mkono wewe, shida Iko wapi?
 
Hahahaha bwana Tindo na ugomvi wa magufuli haha sijui alikukosea nini Yule jamaa
Mimi na viongozi walevi wa madaraka hapana. Hata afanye vizuri vipi hawezi kupata sifa toka kwangu, sana sana atakachopatia nitaona ni wajibu wake maana analipwa mshahara.
 
lakin kwanin nae mpina mbunge mkomavu ule ushahidi hakuupeleka bungen? Kisha akaitisha vyombo vya habari?
Ndicho alichokifanya mkuu. Spika yeye alitaka ushahidi huo ujadiliwe kwanza na Kamati ndipo Mpina autoe kwa wananchi.
 
Mkuu ni kweli. Lkn watu hujifunza kutokana na makosa na kisha hubadilika.

Hata shetani alikuwa malaika mkuu. Je, tuendelee kuheshimu asili yake (alipokuwa malaika) ama tumhukumu kwa kazi zake za sasa?
Taarifa yake ya Sasa ni ya uhakika na nimeikubali, lakini usishangae akipata mlo akaanza kuongea lugha za ajabu. Nimeshajifunza sana kwa hayo matakataka ya ccm, hivyo siwafagilii kabisa. Hata wakipatia Sina muda wa kuwashobokea.
 
Unasimama na shetani aliyechoma nyavu za wavuvi wa nchi hii na kuwatia umaskini? Mnaomsapoti Mpina hamna tofauti na vijana wapumbavu wa Liberia waliomchagua dikteta Charles Taylor aliyeua wazazi wao. Wakati wa kampeni walikuwa na msemo wao wa "He killed My Ma, He killed my Pa.... I'll Vote for him"

Mpina alikuwa ni miongoni mwa viongozi makatili wa awamu ya 5 waliofanya ushenzi mwingi sana kwa wananchi wasio na hatia. Hana political legitimacy ya kunyooshea mtu kidole.
Manabii na wanafunzi wengi wa Yesu walikuwa wauaji kabla. Hata Shetani hapo awali alikuwa malaika mkuu.

Watu hujifunza na kubadilika mkuu na tuyazingatie mabadiliko badala ya kuishi kwa historia.
 
NASIMAMA NA MPINA.

Lakin nadhani kuna sehemu umekosea, hata kama nikweli spika anampinga mpina, lakin kwanin nae mpina mbunge mkomavu ule ushahidi hakuupeleka bungen? Kisha akaitisha vyombo vya habari?

Wote tunaijua nchi yetu, HOJA YAKE NI KUBWA KULIKO KOSA ALILOFANYA, ila linageuzwa lake kama ndio kubwa kuliko hoja ya SUKARI.

Narudia tena nasimama nae na ninapenda serikari impatie majibu hoja yake.
Kwa Hilo bunge lenye hadi wabunge wasio na vyama, ni nadra taarifa kama hiyo kufanyiwa kazi. Ni Bora huyo Mpina kaiweka hadharani tu. Kumbuka taarifa ya shambulio la Lisu ilivyowekwa kapuni
 
Serikali na Bunge vyote vimemgeukia Mh Mpina hapa kuna jambo

Mh Mpina kasema kweli ndio mana serikali na bunge linahangaika

TUPAZE SAUTI KUMTETEA MPINA
 
Back
Top Bottom