Wananchi wa Arusha mlichofanya kwa RC ni dharau kubwa kwa mamlaka za uteuzi; acheni mgomo fungueni mioyo

Wananchi wa Arusha mlichofanya kwa RC ni dharau kubwa kwa mamlaka za uteuzi; acheni mgomo fungueni mioyo

Wananchi wa Arusha wameingia mitini kumpokea RC mpya. Hii siyo Ishara nzuri kwa kiongozi anayependa kuabudiwa. Vyombo vya habari vilijiandaa kurusha live msafara wake lakini wamekwama kwa kukosekana umati.

Jambo la pili lililowaudhi wananchi wa Arusha ni kitendo cha kuwa na kiongozi anayewaza kugombana na watu kila wakati. Kila anapozungumza anaonyesha kutengeneza maadui kuliko marafiki. Huu siyo uongozi

Jambo jingine nikuchukua magari ya utalii na kuyapeleka KIA ambacho ni tafsiri ya rushwa. Haya magari kwanini wanapoteuliwa wakuu wengine wa mkoa hayalazimishwi kujitokeza kumlaki?

Mkuu wa mkoa wa Mwanza amekwenda kuripoti hakuna misafara, mkuu wa mkoa wa Mara hakuna msafara; Mongela hakuwa na misafara. Kwanini tunaamini kupanga watu kwenye msafara ndio utandaji?

Mkuu wa mkoa ni nafasi ya utumishi siyo siasa; kuchukua magari ya watu binafsi na kufanya nayo siasa ni rushwa. Kwanini tusikemee haya? Kama tunaamini ndio utaratibu basi wakuu wote wa mikoa wawe wanalazimisha misafara kila wanapokwenda tuone kama umaskini unaisha.

Viongozi wa juu jifunzeni kukemea la sivyo itanonekana kuna baraka kutoka juu

View: https://www.youtube.com/live/VXTPjuOMofk?si=8Cu7jXfTxNFEaJmd

Aisee Arusha Hawataki Shobo.

Somo amelipata Day 1
 
Nyie si wadudujiandaeni kuuliwa kwa kupuliziwa dawa maalumu.

Mkandaji wenu yupo hapo chuga
Makonda ni mshamba Wala hawezi hapa amefika.... Kama hatujampeleka mto nduruma akaogelee ohooo.. achana na wadudu asee jombii.
 
Sasa mbona hskupits Matejoo na kambi ya fisi, huyo Makonda haijui Arusha kabisa kabisaa 🤣
 
Jf itajaa nyuzi za uongo kuhusu makonda
 
Back
Top Bottom