Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wametumwa na Chatanda a.k.a Singo MazaSiku chache baada ya RC Makonda kuelekeza TAKUKURU wamweke ndani Mtendaji Kata ya Bwawani na asipewe dhamana kwa tuhuma za kuchukua rushwa milioni moja; wananchi wa kati hiyo zaidi ya mia mbili wamekodi magari na kwenda ofisi za TAKUKURU kushinikiza mtendaji huyo aachiwe huru kwani mafisadi wakiongozwa na madiwani na viongozi wa CCM waliofisadi kata hiyo wameanza kutumia ulaghai kuwakandamiza wananchi.
Wananchi wamesema mtendaji huyo alipangiwa kufanya kazi kata hiyo mwaka 2019. Alipoanza kazi mashamba ya kijiji yalikuwa yanatumika na viongozi kulima na kujimilikisha kama ya kwao. Mtendaji aliwanyang'anya mashamba hayo viongozi akiwemo diwani na kuwapa wananchi jambo ambalo viongozi hao wa CCM walichukizwa nalo.
Wakati anapangwa kufanya kazi katika kata hiyo hakuna fedha iliyokuwa inakusanywa kama ushuru kutoka kwenye mali za kata; kwa sasa mashamba yanachangia zaidi ya milioni 30.
Amefanikisha kujenga kituo cha afya na shughuli za maendeleo zinaendelea. Aidha, wakati anaingia wanafunzi walikuwa wanapeleka mahindi na maharage kwa ajili ya chakula ila sasa hivi mtendaji huyo ametenga ekari 20 kwa ajili ya shule na kwa mwaka huu shule imevuna zaidi ya gunia 80 zinazotumika kulisha wanafunzi.
Kuhusu rushwa ya milioni moja inayodaiwa na Mkuu wa Mkoa, wananchi wamesema fedha hizo zilitolewa adharani na hazikuwahi kukabidhiwa kwa mtendaji badala yake zilielekezwa kununua vifaa vya ujenzi na kwamba Makonda alipaswa kuwahoji wananchi kuliko kutoka na taarifa ofisini kwake na kwenda kuwakamata watu wasio na hatia kwa maelekezo ya mafisadi wanaotumia mali za umma kuwaumiza viongozi wenye maono kama mtendaji.
Wananchi hao wameitaka TAKUKURU kufanya kazi kwa utaalamu badala ya kufanya kazi kisiasa. Wamehoji kama kweli kulikuwepo rushwa kwanini TAKUKURU haikuwahi kuchunguza badala yake inapokea maelekezo? Wamehoji kwanini TAKUKURU wameshindwa kufika kijijini kufanya mahojiano na wananchi badala yake wamejazana kumweka mahabusu mtendaji ambaye dhamana ni haki yake?
Mwisho, wananchi wanadai mambo aliyoyafanya mtendaji wa Bwawani yanastahili pongezi na siyo kuadhibiwa kama mkuu wa Mkoa anavyofanya. Kama mkuu wa mkoa ana vyombo alipaswa kubaini mapema kwamba viongozi wa CCM wa kata wanatumia ofisi yake kupambana na watendaji wa serikali wanaowatumikia wananchi kwa haki.
Na yeye arejeshe Pesa alizozipora huko TASAF.Ni jukumu la Makonda kufuatilia kwa undani badala ya kutoa maelekezo na majibu haraka hadharani
Kufanya mambo bila kuyapa tafakari ya kutosha kadri inavyostahili.Hivi, nini maana ya neno " KUKURUPUKA"?
Hakika kabisa, mambo kadhaa yalinisaidia:Sasa fikira hapo huyo OCCID na polisi wenzake wangekurupuka tu kwa kuzingatia hao wanasiasa na kukutia rumande ina maana ungesota jela miezi yote waliyokuwa wanafanya huo uchunguzi wao kwa sababu hiyo tuhuma yenyewe kwa sheria za Tanzania haina dhamana. Ni mfumo mbaya sana polisi kupewa maelekezo na wanasiasa jinsi ya kufanya kazi zao ikiwemo amri za kukamata watuhumiwa kutoka kwa wanasiasa.
Na yeye arejeshe Pesa alizozipora huko TASAF.
View: https://youtu.be/MDj94T7_NOE?si=zm15RzDwRYRZ-qnb
Mkuu acheni kusifia Majambazi na Viongozi wa kundi la wasiojulikana.Aisee sijawahi kuiona hii
Asante kwa kumbukumbu hizi
Kweli hizo ni dhulma ila wanapoongea kama wema
Nani anasifia majambaziMkuu acheni kusifia Majambazi na Viongozi wa kundi la wasiojulikana.
Tatizo la Arusha wahuni walishaipiga copy serikali sasa Makonda anawapiga spana hadi watanyooka.Siku chache baada ya RC Makonda kuelekeza TAKUKURU wamweke ndani Mtendaji Kata ya Bwawani na asipewe dhamana kwa tuhuma za kuchukua rushwa milioni moja; wananchi wa kati hiyo zaidi ya mia mbili wamekodi magari na kwenda ofisi za TAKUKURU kushinikiza mtendaji huyo aachiwe huru kwani mafisadi wakiongozwa na madiwani na viongozi wa CCM waliofisadi kata hiyo wameanza kutumia ulaghai kuwakandamiza wananchi.
Wananchi wamesema mtendaji huyo alipangiwa kufanya kazi kata hiyo mwaka 2019. Alipoanza kazi mashamba ya kijiji yalikuwa yanatumika na viongozi kulima na kujimilikisha kama ya kwao. Mtendaji aliwanyang'anya mashamba hayo viongozi akiwemo diwani na kuwapa wananchi jambo ambalo viongozi hao wa CCM walichukizwa nalo.
Wakati anapangwa kufanya kazi katika kata hiyo hakuna fedha iliyokuwa inakusanywa kama ushuru kutoka kwenye mali za kata; kwa sasa mashamba yanachangia zaidi ya milioni 30.
Amefanikisha kujenga kituo cha afya na shughuli za maendeleo zinaendelea. Aidha, wakati anaingia wanafunzi walikuwa wanapeleka mahindi na maharage kwa ajili ya chakula ila sasa hivi mtendaji huyo ametenga ekari 20 kwa ajili ya shule na kwa mwaka huu shule imevuna zaidi ya gunia 80 zinazotumika kulisha wanafunzi.
Kuhusu rushwa ya milioni moja inayodaiwa na Mkuu wa Mkoa, wananchi wamesema fedha hizo zilitolewa adharani na hazikuwahi kukabidhiwa kwa mtendaji badala yake zilielekezwa kununua vifaa vya ujenzi na kwamba Makonda alipaswa kuwahoji wananchi kuliko kutoka na taarifa ofisini kwake na kwenda kuwakamata watu wasio na hatia kwa maelekezo ya mafisadi wanaotumia mali za umma kuwaumiza viongozi wenye maono kama mtendaji.
Wananchi hao wameitaka TAKUKURU kufanya kazi kwa utaalamu badala ya kufanya kazi kisiasa. Wamehoji kama kweli kulikuwepo rushwa kwanini TAKUKURU haikuwahi kuchunguza badala yake inapokea maelekezo? Wamehoji kwanini TAKUKURU wameshindwa kufika kijijini kufanya mahojiano na wananchi badala yake wamejazana kumweka mahabusu mtendaji ambaye dhamana ni haki yake?
Mwisho, wananchi wanadai mambo aliyoyafanya mtendaji wa Bwawani yanastahili pongezi na siyo kuadhibiwa kama mkuu wa Mkoa anavyofanya. Kama mkuu wa mkoa ana vyombo alipaswa kubaini mapema kwamba viongozi wa CCM wa kata wanatumia ofisi yake kupambana na watendaji wa serikali wanaowatumikia wananchi kwa haki.
Mkuu rudi njoo CHADEMA tupambanie HAKI.Nani anasifia majambazi
Ndio maana nilihama mazima huko
Siwezi kuyasifia hayo
Mbona wewe huwa huweki picha? Uchaguzi wote wa Chadema ulisema ulikuwepo ulituwekea mkuu?Kapicha ka Maandamano 😂