Wananchi wa kata ya Bwawani Arusha waandamana kulazimisha TAKUKURU wamwachie Mtendaji Kata aliyewekwa Ndani na Makonda; wadai RC hasikilizi wananchi

Siku chache baada ya RC Makonda kuelekeza TAKUKURU wamweke ndani Mtendaji Kata ya Bwawani na asipewe dhamana kwa tuhuma za kuchukua rushwa milioni moja; wananchi wa kati hiyo zaidi ya mia mbili wamekodi magari na kwenda ofisi za TAKUKURU kushinikiza mtendaji huyo aachiwe huru kwani mafisadi wakiongozwa na madiwani na viongozi wa CCM waliofisadi kata hiyo wameanza kutumia ulaghai kuwakandamiza wananchi.

Wananchi wamesema mtendaji huyo alipangiwa kufanya kazi kata hiyo mwaka 2019. Alipoanza kazi mashamba ya kijiji yalikuwa yanatumika na viongozi kulima na kujimilikisha kama ya kwao. Mtendaji aliwanyang'anya mashamba hayo viongozi akiwemo diwani na kuwapa wananchi jambo ambalo viongozi hao wa CCM walichukizwa nalo.

Wakati anapangwa kufanya kazi katika kata hiyo hakuna fedha iliyokuwa inakusanywa kama ushuru kutoka kwenye mali za kata; kwa sasa mashamba yanachangia zaidi ya milioni 30.

Amefanikisha kujenga kituo cha afya na shughuli za maendeleo zinaendelea. Aidha, wakati anaingia wanafunzi walikuwa wanapeleka mahindi na maharage kwa ajili ya chakula ila sasa hivi mtendaji huyo ametenga ekari 20 kwa ajili ya shule na kwa mwaka huu shule imevuna zaidi ya gunia 80 zinazotumika kulisha wanafunzi.

Kuhusu rushwa ya milioni moja inayodaiwa na Mkuu wa Mkoa, wananchi wamesema fedha hizo zilitolewa adharani na hazikuwahi kukabidhiwa kwa mtendaji badala yake zilielekezwa kununua vifaa vya ujenzi na kwamba Makonda alipaswa kuwahoji wananchi kuliko kutoka na taarifa ofisini kwake na kwenda kuwakamata watu wasio na hatia kwa maelekezo ya mafisadi wanaotumia mali za umma kuwaumiza viongozi wenye maono kama mtendaji.

Wananchi hao wameitaka TAKUKURU kufanya kazi kwa utaalamu badala ya kufanya kazi kisiasa. Wamehoji kama kweli kulikuwepo rushwa kwanini TAKUKURU haikuwahi kuchunguza badala yake inapokea maelekezo? Wamehoji kwanini TAKUKURU wameshindwa kufika kijijini kufanya mahojiano na wananchi badala yake wamejazana kumweka mahabusu mtendaji ambaye dhamana ni haki yake?

Mwisho, wananchi wanadai mambo aliyoyafanya mtendaji wa Bwawani yanastahili pongezi na siyo kuadhibiwa kama mkuu wa Mkoa anavyofanya. Kama mkuu wa mkoa ana vyombo alipaswa kubaini mapema kwamba viongozi wa CCM wa kata wanatumia ofisi yake kupambana na watendaji wa serikali wanaowatumikia wananchi kwa haki.
Wametumwa na Chatanda a.k.a Singo Maza
 
Sasa fikira hapo huyo OCCID na polisi wenzake wangekurupuka tu kwa kuzingatia hao wanasiasa na kukutia rumande ina maana ungesota jela miezi yote waliyokuwa wanafanya huo uchunguzi wao kwa sababu hiyo tuhuma yenyewe kwa sheria za Tanzania haina dhamana. Ni mfumo mbaya sana polisi kupewa maelekezo na wanasiasa jinsi ya kufanya kazi zao ikiwemo amri za kukamata watuhumiwa kutoka kwa wanasiasa.
Hakika kabisa, mambo kadhaa yalinisaidia:

Kwanza nilikuwa na ki-status fulani pale, hivyo umakini ulihitajika kudili nami.

Pili wale green mamba hawakuwa wamejiconnect vyema na hao polisi. Yule OCCID hawakuweza kumwingia na hakutaka kuvuruga CV yake (angekuwa tumbo-oriented kama polisi kata nadhani ningesota kidogo). Kwakuwa ilikuwa enzi za mwendazake, waliamini sana kuwa wao kwakuwa tu ni wa kijani tena kutoka makao makuu madogo ya nchi kwa awamu hiyo basi ni alpha na omega, wangeweza kuamua chochote na dola ikatii, wakafanya kizembe.

Zaidi hawakuwa na ushirikiano na familia ya kibinti kile walichotaka kukitumia, familia ya mchungaji tena mwenyekiti wa CDM. Kwahiyo kupanga dili la kihuni na mpinzani wao ikawa shida wakabaki kuunda mchongo dhaifu gizani.
 
Siku chache baada ya RC Makonda kuelekeza TAKUKURU wamweke ndani Mtendaji Kata ya Bwawani na asipewe dhamana kwa tuhuma za kuchukua rushwa milioni moja; wananchi wa kati hiyo zaidi ya mia mbili wamekodi magari na kwenda ofisi za TAKUKURU kushinikiza mtendaji huyo aachiwe huru kwani mafisadi wakiongozwa na madiwani na viongozi wa CCM waliofisadi kata hiyo wameanza kutumia ulaghai kuwakandamiza wananchi.

Wananchi wamesema mtendaji huyo alipangiwa kufanya kazi kata hiyo mwaka 2019. Alipoanza kazi mashamba ya kijiji yalikuwa yanatumika na viongozi kulima na kujimilikisha kama ya kwao. Mtendaji aliwanyang'anya mashamba hayo viongozi akiwemo diwani na kuwapa wananchi jambo ambalo viongozi hao wa CCM walichukizwa nalo.

Wakati anapangwa kufanya kazi katika kata hiyo hakuna fedha iliyokuwa inakusanywa kama ushuru kutoka kwenye mali za kata; kwa sasa mashamba yanachangia zaidi ya milioni 30.

Amefanikisha kujenga kituo cha afya na shughuli za maendeleo zinaendelea. Aidha, wakati anaingia wanafunzi walikuwa wanapeleka mahindi na maharage kwa ajili ya chakula ila sasa hivi mtendaji huyo ametenga ekari 20 kwa ajili ya shule na kwa mwaka huu shule imevuna zaidi ya gunia 80 zinazotumika kulisha wanafunzi.

Kuhusu rushwa ya milioni moja inayodaiwa na Mkuu wa Mkoa, wananchi wamesema fedha hizo zilitolewa adharani na hazikuwahi kukabidhiwa kwa mtendaji badala yake zilielekezwa kununua vifaa vya ujenzi na kwamba Makonda alipaswa kuwahoji wananchi kuliko kutoka na taarifa ofisini kwake na kwenda kuwakamata watu wasio na hatia kwa maelekezo ya mafisadi wanaotumia mali za umma kuwaumiza viongozi wenye maono kama mtendaji.

Wananchi hao wameitaka TAKUKURU kufanya kazi kwa utaalamu badala ya kufanya kazi kisiasa. Wamehoji kama kweli kulikuwepo rushwa kwanini TAKUKURU haikuwahi kuchunguza badala yake inapokea maelekezo? Wamehoji kwanini TAKUKURU wameshindwa kufika kijijini kufanya mahojiano na wananchi badala yake wamejazana kumweka mahabusu mtendaji ambaye dhamana ni haki yake?

Mwisho, wananchi wanadai mambo aliyoyafanya mtendaji wa Bwawani yanastahili pongezi na siyo kuadhibiwa kama mkuu wa Mkoa anavyofanya. Kama mkuu wa mkoa ana vyombo alipaswa kubaini mapema kwamba viongozi wa CCM wa kata wanatumia ofisi yake kupambana na watendaji wa serikali wanaowatumikia wananchi kwa haki.
Tatizo la Arusha wahuni walishaipiga copy serikali sasa Makonda anawapiga spana hadi watanyooka.
 
Back
Top Bottom