KERO Wananchi wa Kata ya Kitongo Sima, Wilayani Magu hatuna maji kwa wiki ya tatu, ila bili kila mwezi tunapewa

KERO Wananchi wa Kata ya Kitongo Sima, Wilayani Magu hatuna maji kwa wiki ya tatu, ila bili kila mwezi tunapewa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba kupaza sauti yangu kama mkazi wa Kata ya Kitongo Sima, Wilaya ya Magu, Mkoa wa Mwanza. Tumekaa takribani wiki tatu sasa bila kupata maji. Hali ni ngumu sana na wananchi tunateseka kwa kukosa huduma hii muhimu.

Tunaomba Serikali kupitia Wizara ya Maji itusaidie kufuatilia na kukagua mradi wa maji katika eneo letu. Inashangaza kuona maji yanapatikana takribani kilomita mbili kutoka ziwani, lakini sisi wananchi bado tunahangaika kutafuta maji.

Kinachotuumiza zaidi ni kwamba bili za maji zinatolewa kila mwezi na zinaendelea kupanda, wakati maji yenyewe hayatoki. Hili linatupa mzigo mkubwa sisi wananchi ambao tunalipa bili bila kupata huduma.

Tunaomba mamlaka husika zisikie kilio chetu na zichukue hatua za haraka kuhakikisha huduma ya maji inapatikana katika eneo letu.

Tunaomba maji, si bili pekee.
 
Back
Top Bottom