Wananchi wa Kata ya Mbezi, Dar es Salaam: Hatuna maji, Wanawake na Watoto tunateseka

Wananchi wa Kata ya Mbezi, Dar es Salaam: Hatuna maji, Wanawake na Watoto tunateseka

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876

Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Mbezi, jijini Dar es Salaam, wamelalamikia ukosefu wa maji katika mitaa yao, hali wanayosema imekuwa changamoto kubwa kwa wananchi, hususan Wanawake na Watoto.

Wananchi hao wametoa wito kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Mbunge wa Kibamba, Angela Kairuki, pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), kuhakikisha wanatatua changamoto hiyo ili huduma ya maji irejee katika maeneo yao.

Aidha, Diwani wa Kata ya Mbezi, Pius Nyantori, amesema wananchi wanakumbana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji. Ameeleza kuwa wakati mwingine watoto hushindwa kwenda shule kwa sababu hulazimika kwenda kuchota maji. Pia amesema wanawake wamekuwa waathirika wakubwa zaidi wa changamoto hiyo.
 
Kwa jiografia ya Tanzania, hatukupaswa kulia na shida za maji. Haya ni matatizo ya kujitakia kama nchi
 
Back
Top Bottom